Nini faida na hasara za nyumba za mawe? Bongo kuna wataalamu wa kujenga kwa mawe namna hii?

Nyumba za mawe ziko imara zaidi kuliko za tufali (ni nadra sana kuwa na ufa kwenye ukuta). Lakini gharama zake ni kubwa kidogo kwenye kunyoosha kuta ili upate usawa kwani simenti inakwenda nyingi.

Zanzibar ziko nyingi tu hasa katika maeneo ya karibu na pwani.

Kabla ya ujenzi wa tofali kushika kasi ujenzi mkuu ulikuwa kwa kutumia mawe. Lakini fundi lazima awe mweledi wa kunyoosha kuta za nyumba bila ya hivyo inakaa upande.
 
Uhimara wake unapatika kwa ubora wa mjengaji. Hizi zikikosewa katika kuyaunganisha mawe zinaweka ufa mwingi tu na ubaya wa mawe ikitokea ufa mkubwa ni rahisi sana yakalazimisha kuporomoka kutokana ya kuwa jiwe haliwi na kitako nyoofu.
 
Ujenzi wowote unahitaji utaalamu hilo halina shaka. Aidha aina ya mawe yanayotumika kujengea pia kuna utaalamu wake.

Angalia yale majumba ya stone town Unguja mjini, yale ya asili yote yamejengwa kwa mawe na chokaa na yamekaa kwa miaka mingi sana. Sasa hivi baadhi yameanza kuanguka kwa vile hakuna uhudumiaji.
 
Kuna kitu kama chainsaw kinachonga mawe ukubwa unaotaka na linachongwa jiwe linakuwa kama tofali lakini yote haya kufanyika kuna bei yake.
 
Nyumba za mawe ni nzuri ila ni gharama sana yaan unahitaji expert wa kufanya hiyo kazi (Fundi), pia huhitaji plaster wala rangi ukijenga umemaliza,

Maeneo ambayo mawe yanapatikana kwa urahisi kama Dodoma, Mwanza au Iringa kutakua na uafadhali katika ujenzi, ukijenga Dar jiwe unalitoa Lugoba utajua hujui
 
Ukifanya finishing madirisha ya vioo inapendeza sana
 
Uhimara wake unapatika kwa ubora wa mjengaji. Hizi zikikosewa katika kuyaunganisha mawe zinaweka ufa mwingi tu na ubaya wa mawe ikitokea ufa mkubwa ni rahisi sana yakalazimisha kuporomoka kutokana ya kuwa jiwe haliwi na kitako nyoofu.
Hapo kwenye wataalamu naona ndiyo changamoto. Nimefanya utafiti inaonekana kuna mambo mengi sana ya kuzingatia, hasa unapojenga kwenye kona.
 
Nyumba za mawe ni imara sana, mawe yana sharabu jua hivyo siku za jua kali inaweza kuwa joto kali nje lakini ndani hakuna joto.
Zingetufaa sana huku nchi za joto. Vipi kwenye baridi? Si unakuwa kama upo kwa friji?
 
Kuna kitu kama chainsaw kinachonga mawe ukubwa unaotaka na linachongwa jiwe linakuwa kama tofali lakini yote haya kufanyika kuna bei yake.
Yale wanachonga na kama chainsaw yanakuwa sandstones. Siyo magumu sana. Yanatoa tofali nzuri sana. Bila shaka hata yale ya baharini unaweza kuchonga. Kuna haya ya volcano, granite. Magumu balaa, yapo kama chuma.
 
Hapa Rorya kuna secondary imejengwa Kwa mawe tuu inaitwa Waningo sec school. Nasikia na fundi aliyenga bado yupo hai mpaka Leo hii yupo Musoma na bado anajenga nyumba za dizaini hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…