Mlolongo
JF-Expert Member
- Jul 4, 2019
- 3,483
- 6,257
Baadhi ya nchi afrika kumiliki gari ni anasa au utajiri ila, nasema ila ukiweza kununua gari nunua inakupa nafasi ya kukimbizana na shilingi.
Wakoloni a.k.a mabeberu wao usafiri ni sehemu ya maisha siyo anasa.
Kaka naomba unishauri. Najichanga nifikishe 5 mil. nitafute gari ndogo kati ya Passo, Vitz, Starlet (najua kupata IST kwa bei hiyo mtihan).
Je, naweza kupata kweli kwa bei hiyo?
Halafu nataka hiyo milioni 5 ijumuishe hadi BIMA ya gari (sijui ndio mnaita licence).
Nitaweza kweli ama najidanganya niendelee kusugua malapa?
Kati ya gari hizo ndogo unanishauri nitafute ipi (ukizingatia sijawahi kumiliki gari)
Natafuta gari ya mizunguko hapa mjini Dar. Kwenda UDSM, kurudi nyumban, kwenda kuwasalimia dada zangu Bunju!