..Machi 11, 1979 ndiyo siku ambayo majeshi ya Tanzania yalitoa kipigo kikali kwa majeshi ya Uganda, Libya, na Wapalestina, ktk eneo linaloitwa Lukaya.
..Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema vita vya Tanzania dhidi ya Uganda iliamuliwa Lukaya. Kama Amini angeshinda ktk mapigano ya Lukaya basi angeweza kuyarudisha majeshi ya Tanzania mpaka Kagera na kushinda vita ile.
..Lakini hali ilikuwa tofauti, majeshi ya Tanzania, haswa Brigedi ya 201 iliyokuwa ikiongozwa na Brigadier Imran Hussein Kombe yaliweza kuyasambaratisha majeshi ya Amin na washirika wake na hivyo kufanya njia ya ushindi wa Tanzania kuwa nyeupe.