Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Ni mtanzania. Maana yangu TISS mzawa, aliekulia ndani. Naamini hili la diwani wengi wazee mle tena wakongwe kama hawakulipenda ila hawakuwa na namna. Na nifikiri pia mteuaji alikuwa na mashaka ya kuteua DG ambae ni zao la mtangulizi wake au watu wa watu
hapa nimekusoma. maana mtu ambae amekua na amekulia akiwa kwenye taasisi anakuwa na ethics fulani. anakuwa na hofu fulani.. haendeshi taasis kisiasa.
Maybe rais aliogopa kuteua mtu from the system maana wanaweza kugomea kutekeleza jambo fulani.. the only key ni kumuweka mtu ambae atakuwa rais kuwa controlled.
 
R.I.P Imran, Mdogo wake alitaka aje kufanya postmoterm Yeye Mwenyewe akitokea Zimbabwe ambako alikuwa akihudumu kama Daktari

Alisahau this is Tanzania
acha uongo sheria za kidaktari haziruhusu.alisoma kweli huyo? Au alikurupuka tu km unavokurupuka kutoa tamko?
Umesomea wapi kwanza tuanzie hapo
..
 
Asante sana mkuu, nimeelewa kabisa, hapa hii ilikuwa ni mpango huyu jenerali auawae tu, na wahusika wakaachiwa huru
Marehemu alikuwa mnoko sana uchaga mwiiiingi eti watawale wao sababu anajua nusu ya utawala ulivo. Tukamuonyesha kazi.
 
Holy Man,

..huyu jamaa angejua jinsi Imran Kombe alivyoongoza brigedi yake wakati wa vita vya kagera asingetoa kashfa hizo.

..na kudhihirisha kwamba alikuwa kamanda mahiri aliporudi toka vitani aliteuliwa kuwa mnadhimu mkuu wa jwtz.

Huyo jamaa nime mshangaa sana, kama ni mstaafu kweli kama anavyo jinadi. Nchi yenyewe hadi kumpa nafasi ya juu kabisa jeshini na badae kuwa mkuu wa idara ya usalama, maana yake walitambua uwezo wake.
 
..Machi 11, 1979 ndiyo siku ambayo majeshi ya Tanzania yalitoa kipigo kikali kwa majeshi ya Uganda, Libya, na Wapalestina, ktk eneo linaloitwa Lukaya.

..Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema vita vya Tanzania dhidi ya Uganda iliamuliwa Lukaya. Kama Amini angeshinda ktk mapigano ya Lukaya basi angeweza kuyarudisha majeshi ya Tanzania mpaka Kagera na kushinda vita ile.

..Lakini hali ilikuwa tofauti, majeshi ya Tanzania, haswa Brigedi ya 201 iliyokuwa ikiongozwa na Brigadier Imran Hussein Kombe yaliweza kuyasambaratisha majeshi ya Amin na washirika wake na hivyo kufanya njia ya ushindi wa Tanzania kuwa nyeupe.
 
Waslaam wakuu.

Swali langu linahusu mauaji ya huyu bwana ambaye alishawahi kuwa shushushu mkuu.

Yalikuwa mauaji ya kutatanisha kweli, mpaka leo hapajawahi kuwa na majibu ya kisomi na ya kueleweka juu ya nani yule alimfyatulia risasi na kumuua yule kachero.

Vyanzo vyangu vinaniambia bwana DIWAN ATHMAN NDIYO ALIFYATUA RISASI ZILE KWA EMRAN KOMBE JE NI KWELI
 
waslaam wakuu.
swali langu linahusu mauaji ya huyu bwana ambaye alishawahi kuwa shsushu mkuu.
yalikuwa mauaji ya kutatanisha kweli, mpaka leo hapajawahi kuwa na majibu ya kisomi na ya kueleweka juu ya nani yule alimfyatulia risasi na kumuua yule kachero.
vyanzo vyangu vinaniambia bwana DIWAN ATHMAN NDIYO ALIFYATUA RISASI ZILE KWA EMRAN KOMBE JE NI KWELI
Lodilofa ndiye aliamuru auwawe
 
Back
Top Bottom