Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Wewe umepatia, haikuwa Sheikh Issa Ponda, kulikuwa na Sheikh Shabani MAGEZI na Mwenzie nimemsahau jina,ila nakumbuka kitu kama (MAZINGE), mmoja kati yao alikatwa mguu akaachana na mihadhara kabisa. Msikiti wa mwembe chai ndio ulikuwa base yao.

Walikuwa wanashindana na kikundi cha BIBLIA NI JIBU kiliongozwa na Simbaulanga na Ndimbo.

Huyu ponda alikuwa na kitu walikiita BALKUTA lilikuwa linafadhiliwa na waturuki fulani kama sikosei. Hawa walikuwa na ugomvi wao na Bakwata na Serikali.

Miaka hiyo nilikuwa naishi Mtaa wa Matombo jirani na msikiti wa sheikh Yahaya, bondeni kuelekea Mburahati.

Mwembe chai ilikuwa mwembe chai kweli, migahawa ya chai mingi na mama ntilie wa kumwaga, Gereji za kumwaga na zile deal za Magomeni zilifanyikia hapo mwembe chai hiyo.
 
Ok kwahiyo kumbe kulikuwa na majibizano kati Askari na wahisika,na hao wahusika walikuwa wakishambulia kwa silaha gani?
 
Ok kwahiyo kumbe kulikuwa na majibizano kati Askari na wahisika,na hao wahusika walikuwa wakishambulia kwa silaha gani?

Kwa kweli sikupata muda wa kuchunguza,kwanza tulikanyagana tukatoka mbio Tena pekupeku,mwenzangu alipigwa na jiwe,kulikua na polisi kalala chini anavuja damu wenzake walimbeba,pasko mwenyewe alikua akiripoti akisikia mlio anainama.

Nadhani baada ya Askari kazaa kuzidiwa nguvu ndo tukasikia vyuma vya mzungu vikinguruma.

Changamoto ni kwamba km taifa hatukuwai kuwa na uzoefu wa vurugu namna ile.kila mtu alihamaki

Upande wa pili kuna hoja za extremists...yaani wananchi wenye hasira Kali,je unakua na hasira Kali kwa jamhuri halafu unadhuru mwenzako?

Km una hasira Kali nenda kwenye majengo ya Serikali kawashikishe adabu mtamalizana huko ila suala la kumvunjia nyumba,bucha,gari mwenzako ni kurudishana nyuma.

Hoja ni mfumo mbovu wa kuwasilisha hoja,pia hata mm nilikua na ndg yangu anaenda kwenye mihadhara hiyo sijui wanabishana vikundi huku waislam huku wakristo sijui yesu Ni jibu na Akina she juma(km sijakosea).Marehemu baba akamwambia yakikukuta huko yatakuwa yako,sijakulea na nikakufundisha dini mkazozane.

Aliwekwa rokapu baba hakwenda kumtoa,walitoana wenyewe huko.
 
Watu wengi tunajadili matokeo Bila kujua chanzo,
Chanzo ni malezi mabovu katika jamii,ubaguzi,Dora kujisahau au kupotezea viashiria vya migogoro,ufukara na fikra za kimaskini.
Kwa wanaokumbuka Mambo mengi yalianza kuweka kimfumo badala ya kimazoea pale BWM alipochukua inchi,mabadiliko hayo yakiambatana na mihemko ndo tukaibukia tulipotokea.
 
Mhenga mwenzangu, upo sawa sawa kabisa. Nakumbuka kwenda na kurudi kazini (nilikua naishi Kimara those days/years) tulikua tunapitia Buguruni, vijana wasichanganye na hi root ya sasa hivi ya Ubungo Posta via Buguruni, those days it wasn't there. Cartoonist wakachora katoto eti kamemuona askari ana bunduki, katoto kusema bunduki kanaita eti Limwembe chai.
 
Kwahiyo tunaweza kusema ni kuhamaki tu kwa Askari na kujikuta wakitumia nguvu zaidi kihasira.
 
Kwahiyo tunaweza kusema ni kuhamaki tu kwa Askari na kujikuta wakitumia nguvu zaidi kihasira.
Wangezembea wangekufa Askari wale jamaa wamejipanga...mwanzon walijaribu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi...hayakufua dafu je unashauri wangefanyaje?wangewaacha wengine waendeelee kupigwa au?pia vurumai hizo zimehatibu pia Mali za raia wema na wengine wasioweza kujitetea...Nani angewafidia?pia unapoanzisha vurumai ukiwa mtu mzima jamii inajifunzaje?
 
Kwahiyo hukuweza kujua silaha walizokuwa wakitumia hao wahusika kuwashambulia Askari ila unajua kuwa Askari wangezembea wangekufa kwa mashambulizi ya hao wahusika? Bado inaonesha hili tukio lilikuwa na utata sana.
 
Mawe,manati,visu,panga,pinde niliona vinaruka hivyo ndo niliona
Kwahiyo hukuweza kujua silaha walizokuwa wakitumia hao wahusika kuwashambulia Askari ila unajua kuwa Askari wangezembea wangekufa kwa mashambulizi ya hao wahusika? Bado inaonesha hili tukio lilikuwa na utata sana.
 
OK Mimi ninavyojua Ponda alikuwa na kundi lake linajiita simba wa mungu.
 
Lakini kwa hayo mauaji ya Mwembechai yalituliza mambo lakini, maana hali kama hiyo haijawahi kujitokeza tena, ama?
 
mpaka leo hajatokea kichaa yeyote wa kiislamu akijifanya kavuta bangi.
 
Nilikuwa nakuja likizo toka Morogoro, Abood ikatushushia Mwenge badala ya Magomeni. Lakini, mwenye majibu mazuri ni Mwenyekiti wa Kanda wa Chama cha Ufipani. Wenye hicho chama walimtuhumu sana kabla hajawa mwenzao kuwa ndio aliwatuma waliotumwa.
Umeandika kishabiki sana. Mwaka 1998 chama kikuu cha upinzani unakifahamu? Kawaulize akina Maalim na Hamad Rashid na kesi zao za uhaini
 
mpaka leo hajatokea kichaa yeyote wa kiislamu akijifanya kavuta bangi.
Ukimya wao sio sababu ya uoga wa kuuawa kama mwembechai..... Huwezi jua next time wakaja kwa style gani kujibu mapigo!! Yataweza jitokeza ya kibiti ama Al Shabaab unafikiri utapata kiburi cha kuja kuwakejeli humu??
Violence sio suluhisho zaidi imeongeza chuki na visasi siku watu wakisema inatosha kama wahutu 1957 ama walendu 2000 huko DRC basi hutopata hata wasaa wakuandika humu JF

Time will tell!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…