Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?


kusilimisha hivi bado hipo.maana ndio ilivutia kuwavuta
 
Huo sasa ni uongo uliopitiliza Kanisa na Karate wapi na wapi???
Duh! Miaka hiyo karate ilikuwa ni YWCA na YMCA. Ushahidi...

Phillip Chikoko sited looking at Madaraka tie his
Brown belt just after their grading at YMCA 1987

Soma zaidi...
 
unakaidi amri ya kutokuandamana ukirusha mawe na mishale,unategemea diplomasia gani?
 
Huyo ni mfia dini hata andiko lake lilikuwa la kuvutia upande wake hivyo hakuna ukweli hapo!!!!.
Echoma,
Tujaalie mimi ni kama ulivyoniita lakini kwako itakuwa bora usome nilichoandika ili uelewe upande mwengine.

Nakushauri usome kwa sababu itakuongezea wewe nguvu ya kujua lile ambalo hulijui na hii itakuwezesha wewe kufanya mjadala ukiwa katika hali ya ujuzi kuliko huku kujadili ukilijua lile lako tu.

Mohamed Said si mwandishi yule unaekutananae kila siku hapa Majlis.

Afisa wa Polisi Zahaki alishuhudia yote akiwa Kituo cha Kati Cha Polisi Dar es Salaam na alifukuzwa kazi kwa kile kilichochukuliwa kama ''kutoenea'' katika jeshi kwa kuonyesha kupinga mauaji yale.

Aliwaendea wahariri wa magazeti yote ili aeleze anachokijua kuhusu Mwembechai lakini wote walimkatalia.

Ndipo aliposhauriwa kuja kwangu.

Mimi nilifanya mahojiano na yeye na nikamrekodi na cassette ya mazungumzo yetu nilimpatia Prof. Hamza Mustafa Njozi na viongozi wengine wa Kiislam kwa ushauri nini kifanyike.

Mahojiano haya yapo kwenye moja ya vitabu vya Prof. Njozi.
Tunahitaji kusikia pande zote mbili, za Serikali na Waislam, ila serikali huwa haitaki kabisa huu mjadala uwepo
 
Tunahitaji kusikia pande zote mbili, za Serikali na Waislam, ila serikali huwa haitaki kabisa huu mjadala uwepo
Chinchila,
Serikali yetu toka uhuru imekuwa na hofu kubwa pale linapokabiliwa na lolote kuhusu Waislam na Uislam kwa hiyo hukataa kabisa kujadili tatizo lililopo.

Mifano ni mingi lakini hapa nitaleta miwili tu.
Lipo tatizo la shutuma ya Waislam kuhujumiwa katika elimu.

Historia yake ni ya miaka mingi na hadi leo hakuna lolote lililofanyika kurekebisha hali hii.
Tatizo la Mwembechai na mauaji yaliyotokea.

Sheria inataka ifanyike, ''Inquest.''
Serikali imekataa.

Kwa nini hili linawezekana kuwa jambo lolote la Waislam halipati haki inayostahili?
Hii ni kuwa Waislam hawako katika nafasi za maamuzi.

Waislam wako nje ya serikali.
Walioshika madaraka wanafanya maamuzi kwa maslahi ya dini yao.

Serikali zote zilizopita hakuna hata moja imekuwa na ujasiri wa kulileta tatizo hili kwenye meza ya majadiliano na kujadili tatizo la Waislam nchini petu.

Ndiyo unaona hata historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imefanyiwa majaribio ya kutaka kuifuta isiwepo kabisa.

Inaogopewa itakuwaje ikifahamika kuwa mchango wa Waislam ulikuwa hauna mfano katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Swali litakalo kuwapo ni kuwa Waislam walijiotelea kwa kiasi kile kwa kutaka iwe nini?
Waje kuwa raia daraja la tatu?

Jibu ni hapana.
Walitaka ukoloni uondoke ili haki na usawa utamalaki katika jamii.

Haki hii imepatikana kwao?
Jibu wanalo serikali yetu.
 
serikali kukandamiza raia wake kwa misingi ya kidini ili iweje? wapate faida gani?

Japo sijasikia maelezo ya upande wa serikali kuhusu hili la Mwembechai inaonyesha kuwa Polisi walikuwa na makosa kwa kutumia nguvu iliyopitiliza ndio maana hawataki hata kutoa maelezo au hata kuruhusu uchunguzi au mijadala yake

Lakini pamoja na hilo serikali imekuwa ikitumia nguvu nyingi kwenye mambo mengine na wala hayahusiani na Uislam, mfano kuna maadamano ya kisiasa yanafanyika na serikali kutumia nguvu nyingi kupita kiasi na kuuwa,so sio sula la kuwa inakandamiza Waislam bali serikali imekuwa ikitumia nguvu kupita kiasi kwenye masuala mengi tu ambayo hayahusiani na Uislam kabisa

Pia kingine mijadala ambayo inahusu Dini huwa inaamsha hisia sana na inaweza kuleta utengano ama uvunjifu wa amani, so ndio maana serikali inalipotezea la Mwembechai sababu kuliamsha litaleta mabaya zaidi kuliko mazuri, hapa ndio unatakiwa uvae viatu vya serikali kuelewa. Pia katika hicho kitabu cha Njozi nimeona mwandishi aliandika kuwa Mkapa alikutana na Waislam kwenye baraza la Idd kusikiliza malalamiko na kero zao na kuziundia timu za kuyafuatilia, ambayo hiyo naona ilikuwa ni njia ya kusema ''samahani'' kwenye suala la Mwembechai

Pia unaposema Waislam wapo nje ya Serikali sijakuelewa maana kila serikali ni lazima viongozi wakuu wa chama na Serikali inakuwa na Waislam mfano sasa hivi serikali ya Magufuli ambayo ndio inadaiwa inawatenga sana Waislam, lakini Makamu wa Rais ni Mwislam na kila mwaka anakuwa Mwisalm, Katibu Mkuu wa CCM ni Mwisalam, Waziri Mkuu ni Mwislam, Rais wa Zanzibara pamoja na Makamu wake wote wawili ni Waislam, sasa utaasemaje hawapo serikalini?

Waislam kwenye uhuru mbona naona wanawekwa pia, maana kitabu cha Historia cha shule ya msingi kilikuwa kimeweka baraza kuu la Tanu wakati wa uhuru nikaona Waislam wengi waliwekwa pale

Mkuu nakubali serikali kukosea mara kadhaa kukandamiza raia wake ikiwa ni pamoja na hilo la Mwembechai lakin i madhambi mengine unaisingizia,
 
Chinchilla,
Naweka hapo chini yaliyo muhimu sana katika yote uliyoandika ili iwe wepesi kufanya rejea:

''Pia unaposema Waislam wapo nje ya Serikali sijakuelewa maana kila serikali ni lazima viongozi wakuu wa chama na Serikali inakuwa na Waislam mfano sasa hivi serikali ya Magufuli ambayo ndio inadaiwa inawatenga sana Waislam, lakini Makamu wa Rais ni Mwislam na kila mwaka anakuwa Mwisalm, Katibu Mkuu wa CCM ni Mwisalam, Waziri Mkuu ni Mwislam, Rais wa Zanzibara pamoja na Makamu wake wote wawili ni Waislam, sasa utaasemaje hawapo serikalini?''

Hayo hapo juu haijafanya serikali kuwa na mizania sawa.

Mizania sawa inataka nchi itawaliwe na wote kwa ushirikiano pasiwe na jamii moja inahodhi fursa zote za nchi na nafasi zote katika elimu, serikali na mashirika yake na sehemu nyingine katika taifa.

Mathalan ukiangalia nafasi katika elimu kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu ni wao, Bungeni ni wao Baraza la Mawaziri ni wao, Makatibu Wakuu ni wao nk. nk.

Hili tatizo ni zito sana na halikuanza leo.

Hoja zako ulizotoa ni kwa kuwa hujui historia ya tatizo hili.

Matatizo haya na hofu ilianza toka mwaka wa 1958 wakati Tanganyika inapigania uhuru wake na mara tu baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu likatokea tatizo ndani ya TANU na kusabisha Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kufukuzwa chama.

Umeuliza, ''Ili iweje?''
Jibu lako liko hapo chini:

Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).
Kitabu cha Njozi kikapigwa marufuku na serikali.

Hayo mengine ya mijadala kuhusu dini sijaona umuhimu wa kuyasemea.
 
Sina shaka yoyote huu utakuwa ni mchango wako wa kipekee kabisa ninaokubaliana nawe mia kwa mia.

Hasa nakazia hapo penye "wewe ni mTanzania".

Tukilifanya hili litoke huko kwenye dini pekee, na kulipeleka hadi kuwa juu ya siasa na vyama vyake; wewe na mimi tutakuwa "Mapacha..." (identical twins) (Kiswahili chake ni nini).

Basi tuanzie hapa..., achana na ulevi wa kumwabudu mtu mmoja, hata kama ni rais.

(Nimesema na ambayo sikutaka kuyasema, lakini umeiamsha sehemu ya ubongo ambayo ni nadra sana kuishughulisha, kutokana na maneno uliyoandika hapo juu).
 
Chinchilla, nadhani huwa humwelewi huyo unayemjibu na wengine wa aina yake, kila wanaposema "waislam".

Maana yao ya 'waislam' ni wale ambao hawapo kwenye mlengo wa BAKWATA. Wengi, kama sio waislam waliowahi kuwa viongozi serikalini, hawa watu hawawatambui kuwa ni 'waislam.' kwa vile wameegemea ndani ya BAKWATA au hawatambui kundi la waislam wanalolikubali wao.

Tatizo lipo hapo na litaendelea kuwepo hapa nchini kwa sababu sioni njia ambayo serikali ya aina yoyote hapa Tanzania itakubali wanayoyasimamia wao.

Lile kundi la wazee wa Dar es Salaam, analolipa sifa ya "mchango wa waislam ulikuwa hauna mfano...); tatizo lilianzia hapo ilipogundulika kuhusisha dini ndio iwe inaongoza siasa. Na hili ndilo linalohitaji kuelezwa watu wajue.
 
Kalamu1,
Nakushukuru sana kwa kuwaleta BAKWATA katika mjadala huu kwani umenipa mimi fursa ya kukueleza ilikuwaje hadi BAKWATA ikaundwa.

Nitajaribu kueleza kwa ufupi kwa kuwa kisa chake ni kirefu mno na ikiwa unakitaka kukisoma chote unaweza kukipata hapo chini na ni ''research paper'' (1989):


Naomba nikutahadharishe.

Hili si suala la kutaka kulifanyia haraka ni tatizo linalotaka mtu kujituliza ukasoma historia kwanza ya uhuru wa Tanganyika na si usome historia rasmi kwani hiyo ni katika moja ya matatizo ya wengi wanaojaribu kuwajadili Waislam wakija na historia rasmi ndani ya vichwa vyao.

Uniwie radhi kwa kujifanyia mimi mwenyewe rejea.

Historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo inaweza kukuweka katika hali ya kulielewa zaidi hili tatizo ipo imeandikwa na inasomwa sasa huu mwaka wa 20 (Said 1998).

Sasa tuendelee.
Unapozungumza BAKWATA si watu bali taasisi na viongozi wake na wala hakuna asemae kuwa BAKWATA si Waislam.

Muhimu sana ufahamu kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam kwa maana ya kuwa Waislam wenyewe waliitaka iwepo.

BAKWATA imeundwa na kikundi cha masheikh na wanasiasa waliokuwa ndani ya TANU wakipewa msaada na serikali na vyombo vyake vyote.

Historia ya BAKWATA imeandikwa na watafiti wawili tu hadi sasa miaka 50 baada ya kuundwa kwake Kiwanuka (1973) na Said (1989).

Kiwanuka kaandika akieleza kwa nini serikali iliamua kuuunda BAKWATA na Said akaja kujibu (rejoinder).

Sasa ikiwa utawasoma hawa wote utakuwa umejiongezea elimu ya kutosha kuelewa tatizo la BAKWATA na Waislam.

Kwa nini serikali iliamua kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA?

Baada ya uhuru mwaka wa 1961 EAMWS illikuwa imeanza mipango ya kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam kutokana na maazimio ya Muslim Congress ya mwaka wa 1962 iliyoweka mikakati ya kuwainua Waislam katika elimu kwa kujenga shule kila jimbo Tanganyika na kumalizia na kuwa na Chuo Kikuu.

Kuna watu walitishika na juhudi hizi za Waislam na njia pekee ya kuvuruga mipango hii ya elimu ilikuwa ni kuivunja EAMWS.

Hawakutaka Waislam waelimike kwani wakielimika watashiriki katika kuongoza nchi hapa kilichokuwa kinatafutwa ni ''maintenance of status quo.'' hali ile ile ya ukoloni iendelee kwa Waislam kuwa daraja la chini wasio na elimu.

Haingii akilini kuwa Waislam waliotoka katika dhulma za ukoloni uliowanyima elimu wataamua kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu.

Baraza la Wazee wa TANU hata siku moja haijataka kuona kuwa Uislam ndiyo unaoongoza serikali.

Unasema jambo ambalo wewe huna ithibatinalo na ingeikuwa ni hivyo Nyerere asingeungwa mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wale wa 1950s.

Sikulaumu unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Waislam hawajasimamia lolote ila kutaka haki na usawa.
Naomba nisimame hapa.

Nakusihi soma kwanza historia ya uhuru wa Tanganyika ndipo utakuwa katika hali ya kujadili ukiwa na elimu ya kutosha vinginevyo itakuwa ni mimi kurejea hapa tena na tena kukusahihisha na kukueleza ukweli kama nifanyavyo hivi sasa.
 
Sasa mkuu ulitegemea uwiano wa Waislam wawe sawa na Wakristu Serikalini wakati idadi yao haipo sawa? Wakristo Tanzania ni wengi kuliko Waislam so hata Serikalini Wakristo ndio watakuwa wengi, naturally
 
Asante sana kwa kunifanya nimuelewe mzee Said. Siku zote namsoma nashangaa mbona sometimes anawapinga waislamu, kumbe yeye ndo wale wasio BAKWATA!!
 
Mohamed Said Some how unaeleweka lakini tatizo lenu kubwa wa upande huo mnapenda kilalamika sana na kujiona mnanyanyasika kwa kila mnalolitenda hivyo kusababisha vurugu nyingi kwenye nchi ambazo ninyi mko wengi.Nchi nyingi sana zenye waislamu wengi zina matatizo makubwa sana ya Amani.Haya yote ni kutokana na kujiona na kujihisi kila wakati mnaonewa kwa sababu tu eti ni waislamu kitu ambacho si kweli wakati mwingine.
Kuhusu waislamu kuwa nje ya serikali ni hisia zenu tu potofu tuhuma hizi toka enzi za JK waislamu wanalalamikia hili wakati kwenye serikali wamejaa tele hata awamu hii ya Tano wako kibao lakini bado tu ndugu zetu hawa wanadai hawako serikalini labda ili wajisikie kuwa wako serikalini basi waisilimishe Tanzania iwe nchi ya kiislamu??.Ushauri wangu kwao wawe wavumilivu kwenye nchi kubwa kama hii yetu si rahisi kila mmoja apate anachokihitaji.Malalamiko mengi namna hiyo ya kutaka kuonewa huruma yatatupeleka pabaya maana yake mnataka mwishowe muonewe huruma na ALSHABAB au BOKO-HARAM nawaomba tuvumiliane tusipende sana kufukua makaburi yaliyopita yamepita tusiwe watu wa visasi.Istoshe tukio hilo lilitokea miaka mingi iliyopita na wengine tulikuwa watoto wadogo sasa mnapokuja kuamsha hisia za watu si vizuri.tukio hilo libaki kwenye historia tu wala si kufukua makaburi!!!!.
 
walipata tabu sana,walipigwa wakachakaa,kipigo chake kilikuwa ni cha mbwa koko,ukitaka sheikh ponda akuchape makofi mwambie habari za kuandamana saivi uone,kabaki kuwa mwanaharakati tu kama mange,what happened was NECCESARY maana watu walianza kujisahau na kuleta UDINI,serikali had to send a CLEAR MESSAGE,hapo ndo ninapompendeaga mzee BENJA,hanaga masihara ktk maamuzi
 
Sasa angalia upuuzi unaoandika hapa, na unataka kabisa watu wenye akili za kufikiri waamini haya...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…