Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Sasa angalia upuuzi unaoandika hapa, na unataka kabisa watu wenye akili za kufikiri waamini haya...!
Kalamu 1,
Umeghadhibika unanitukana, ''Sasa angalia upuuzi unaoandika hapa, na unataka kabisa watu wenye akili za kufikiri waamini haya...!''

Ilikuwa wewe ni wa kunijibu ukasema huamini haya niliyoandika ni maneno ya uongo na ukaeleza ukweli.

Dr. Kiwanuka alieleza yasiyo kweli mimi nikamueleza yaliyo kweli.
Hajarejea kunijibu.

Hapana huu si uongo huu ni ukweli mtupu na ndiyo maana waliofanya haya wako kimya kwani kama wakifungua vinnywa vyao waliotendewa bado wa hai watazungumza.

Walioshiriki katika njama hii katika vyombo vya usalama wanafahamika kwa majina yao na nimetaja majina yao katika kitabu cha Sykes.

Walioshiriki katika vyombo vya habari kwa ajili ya propaganda na kuwashambulia viongozi wa EAMWS baadhi wametangulia mbale ya haki na wengine bado wako hai.

Walioshiriki katika masheikh wanafahamika na majina yao nimeyataja kwenye kitabu.

Ukipenda unaweza kuisoma tasnifu ya Dr. Kiwanuka imeeleza mengi ipo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam: K. Mayanja Kiwanuka, ‘The Politics of Islam in Bukoba District’ (1973).

Nakala ya tasnifu hii iko vilevile Maktaba ya Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD).

Usipandishe hamaki na mori bila ya sababu.
Tafuta hizi rejea usome upate kuelimika.

Mimi sikutukana mtu na nimesoma uongo nimekaa kitako nikasoma kila kitu katika historia hii na kuandika kitabu na elimu hii ndiyo hiyo wote leo mnaisoma hapa Majlis.

Nyote mkiona jina langu mnakuja kunisoma kwani mnajua hakuna kejeli, matusi ila elimu tupu.
Natoa elimu bila khiyana.

Maalim wangu aliyenisomesha elimu ya mjadala (mnakasha) alikuwa akisema ukiona mtu anatoa lugha chafu jua kashindwa hana hoja.

Mwenye hoja anarejesha hoja harejeshi matusi.
 
Ila kutwa mtu anawaza madrasa na kuoa mke wa 5, mtoto atasoma saa ngapi? Ada ya shule utatoa wapi?
Francis...
Penye tatizo katika jamii baadhi mbili zinazokinzana lazima wazungumze hii ndiyo njia salama na ya kistaarabu ya kutatua tatizo hilo.

Mimi nakujibu kwa sababu lazima tuzungumze.
Haifai kukejeli mada iliyopo mezani iko wazi tuijadili kwa heshima.
 
Faru Rajabu,
Haya uliyoeleza si kweli.

Maandamano ya Waislam ya mwisho dhidi ya serikali yalikuwa mwaka wa 2012 na Waislam waliandamana kupinga dhulma ambazo zilikuwa zinafanyika Baraza la Mitihani (NECTA) dhidi ya wanafunzi wa Kiislam.

Maandamano haya yalinyimwa kibali na Polisi lakini Waislam waliamua kuandamana bila ya kibali cha Polisi.

Maandamano haya yalianzia Msikiti wa Kichangani na Sheikh Ponda Ponda alizungumza na Waislam baada ya sala ya Ijumaa akaeleza kwa nini ni lazima Waislam waandamane.

Sheikh Ponda alisema kuwa umekusanywa ushahidi wa kutosha kuhusu Baraza la Mitihani chini ya Dr. Ndalichako kuwa kuna njama dhidi ya vijana wa Kiislam katika shule ambazo Waislam wamejenga katika jitihada za kujikwamua katika elimu.

Sheikh Ponda akasema kuwa tumenyimwa kibali lakini ndugu zangu tumeamua kuandamana bila kibali ili dunia isikie kilio chetu na ikiwa tutakufa katika kupigania haki yetu kupinga dhulma hii basi basi watakaokuja baadae wataendelea pale tulipoachia.

Nje kulikuwa kumetanda askari na silaha pamoja na magari na juu helikopta zilikuwa zinaruka na onyo la kutoandamana lilikuwa limeshatolewa toka asubuhi na mapema.

Ndani ya msikiti walikuwapo pia makachero.

Sheikh Ponda baada ya kumaliza kuwahutubia Waislam aligeuka kawapa mgongo akaelekea kibla akanyanyua mikono yake juu akawa anaomba dua.

Nilikuwapo pale msikitini.

Wakati Sheikh Ponda anaomba dua ile kimya kimya jirani yangu niliona vijana wamenyanyua mikono na wao wanaomba dua huku machozi yakiwamwagika.

Niliingiwa na hofu.

Nilijua hii leo ikiwa Waislam watauliwa katika haya maandamano kwa kukataa kudhulumiwa sasa tutaingia katika hatua nyingine.

Machozi yanasema mengi ambayo kinywa hakiwezi kusema.

Sijui kilichotokea.

Maandamano yale yalianza na umma ulikuwa mkubwa sana.

Ghafla magari ya Polisi ykaonekana mbele ya Sheikh Ponda na waandamanaji taarifa zikaenea kuwa maandamano yanasindikizwa kwa amani hadi Kidongo Chekundu na yakifika hapo Waislam wanaombwa watulie hapo na Sheikh Ponda na viongozi wa Waislam watachukuliwa na gari ya Polisi hadi Wizara ya Mambo ya Ndani ambako barua ya Waislam itakabidhiwa hapo kwa wahusika.

Waislam baadhi walikubali kubaki Kidongo Chekundu na wengine waliandamana hadi Wizara ya Mambo ya Ndani.

Baada ya kukabidhi barua Sheikh Ponda alirudishwa Kidongo Chekundu huku akipokewa kwa takbir.

Huu ndiyo baadhi ya ukweli katika maisha ya Sheikh Ponda wala si kama ulivyoandika.
 
Sasa mkuu ulitegemea uwiano wa Waislam wawe sawa na Wakristu Serikalini wakati idadi yao haipo sawa? Wakristo Tanzania ni wengi kuliko Waislam so hata Serikalini Wakristo ndio watakuwa wengi, naturally
Chinchilla,
Nadhani kwa bandiko hilo lako umeelewa tatizo lililopo.
Sina haja ya kuzungumzia kuhusu ''religious distribution.''
 
Ilikuwa wewe ni wa kunijibu ukasema huamini haya niliyoandika ni maneno ya uongo na ukaeleza ukweli.
Nilishakwambia siku nyingi kuwa wewe ni 'con artist' aliyekubuhu, labda hukumbuki tu.
Unayoyaweka hapa ni 'ngonjera' zisizokuwa na miguu wala kichwa, lakini kazi ya 'con artist' siku zote ni kuwanasa wenye akili zilizolala.

Sasa, wewe kuitegemea aina hii ya watu kuwa siku moja utafanikiwa kuleta mapinduzi unayoyatafuta ni kujipa matumaini yasiyokuwepo.
 
Nyote mkiona jina langu mnakuja kunisoma kwani mnajua hakuna kejeli, matusi ila elimu tupu.
Natoa elimu bila khiyana.
Eeenh, unahusisha watu usiowajua kabisa hapa. Mimi nipoteze muda wangu kusoma hadithi zako?
Hata huku kujibishana nawe mara moja moja hii ni kukupa picha ya dharau niliyonayo juu ya yote unayoyasimamia na kutaka kuyaeneza.

Nadhani inatosha usije ukadhani nakupa heshima kutokana na majibishano haya..
 
Mungu mbariki Sheikh Ponda
 
Ukweli mtupu !
 
Kalamu 1,
Unaandika umeghadhibika na ghadhabu huondoa adabu na umakini.
Mimi nitakuhakikishia kuwa si mwandishi wa riwaya.

Kama kueneza kalamu yangu unanilaumu kwa hilo ningependa kukuarifu siko peke yangu katika hilo kwani wako wachapaji vitabu, taasisi za utafiti na vyuo vikuu ambao wote hao wanashirikiana na mimi.

Wewe hujibishani na mimi.
Hapa mimi nakusomesha.

Sasa sijui kama una makamo ya kuwadharau hao hapo chini:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  5. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  6. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  7. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  8. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  9. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  10. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  11. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  12. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  13. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  14. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  15. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  16. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  17. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  18. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  19. Awards: Several Awards
  20. Visiting Scholar: (2011)
  21. University of Iowa, Iowa City, USA
  22. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  23. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  24. OTHER COUNTRIES VISITED
  25. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Kalamu 1,
Unazungumza kuhusu ''con artist?'

Kukusaidia kuelewa unachosema nakushauri usome kitabu hiki: ''Count Victor Lustig: The Man Who Sold the Eiffel Tower.''



Nyuma yangu ni Eiffel Tower, Paris​

Unazungumza kuhusu mapinduzi?
Kitabu cha Abdulwahid Sykes kimepindua historia nzima ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kiko ndani ya Cambridge Journal of African History na kinasomeshwa kote Marekani na Ulaya na kwengineko kama rejea katika political history ya Tanzania.
​
 
Francis...
Hapana soma tatizo utalielewa hakuna suala la dini hapa.
Tunazungumza kuhusu dhulma.
Hii mijadala ni hatari sana popote pale hata kama inafanyika kwa nia njema. Cha msingi kila mtu ajitathmini na kujiboresha kwa kadri ya uwezo wake na si kumlaumu mtu mwingine.
 
Mkuu tafaaadhali saaana malizia hili sakata kwa mapana zaidi.
 
Mkuu zidi kumwagika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…