Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

Mkongwe mwenzangu, habari ya kuadimika ndugu Mkandara ?
Karibu tena barazani hapa.

Kwani kuna mpango wa kumuondoa Mbowe madarakani au ni uchaguzi kutimiza demokrasia ukizingatia CHADEMA ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo!!??
Iweje kutimiza suala la kidemokrasia uwe mpango ( ambao kwa mujibu wa maandishi yako ni mpango wenye nia ovu)!!??
 
Inabidi umsome mtu kwanza uelewe anasimamia wapi. Hoja za kwa nini Lissu anagombea Uenyekiti ndizo nimezungumzia. Tuhuma.ntingi zimesemwa ambazo zingeweza kuzunfumzwa toka 2021 na hata kuweka katazo la.Mbowe kuendelea na Uenyekiti.
Usichukulie Uenyekiti kama ni Urais. Mwenyekiti anasimamia tu Chama hana madaraka ya Urais wala Uchief. Hata Uchaguzi ndani ya Vyama.vya Siasa sii lazima kwa sababu ni kazi ya kujitolea hawalipwi mshahara. Kwa hiyo ukiwasoma jamaa hawa unaona kabisa tatizo ni NJAA. Akili yao Mwenyekiti ana source za kucuta mkwanja na Mbowe kavuta sana CCM. Sasa ni zamu yao na wao wavute!. Ikiwa sivyo walivgodhani unadhani Chadema itapona? Yaliwakuta NCCR na CUF kwa mtindo huu huu, ugonvi juu ya UENYEKITI leo wako wapi?
 
Ccm wameweza kumingia Mbowe wakifikiri wakisha muweka Mbowe mfukoni hata Chadema itakuwa imeingizwa mfukoni. Kitu ambacho ccm hakutegemea ni mbowe kupoteza ushawishi na kuaminika kwa wanachadema.

Sasa tegemeo la ccm ni kumfanya Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti kwa njia za mahakama au kutumia nguvu ya serikali.
Bila hivyo Mbowe anakaa pembeni . Chaema chini ya Tundu Lissu na heche ccm watajuwa kuwa hawajui ndani ya mwaka mmoja tu. Watu ccm ilio waandaa kuanzisha vyama vya upizani wanaanza kuisha taratibu.
 
kuhusu sheria ya bunge inasemaje, iwe ilisema hatakiwi kupata au anapata, cha muhimu ni kwamba Lisu alikuwa anajiuguza kila mtanzania anajua, na kile alichopewa na samia haikuwa hisani, ilikuwa haki yake kiubinadamu. sasa mtu ukimpa haki yake unataka akulambe miguu tena, au hujui maana ya haki?
 
Uchaguzi sina tatizo nalo isipokuwa ukiwasikia madai yao ndio utajua ni kampeni. Mgombea ni Lissu kwa nini kila mtu anataka Mbowe aondoke, sijui asigombee, mara mla rushwa, Mbowe ni CCM!
Kweli ndio denokrasia inavyotakiwa? Kwa nini Tundu Lissu asingeweka nia ikaisha bila kuwa na kundi la washabiki nyuma kummaliza kisiasa hata kabla ya Uchaguzi wenyewe? Halafu yanayozungumzwa sii kwamba mapungufu ya itikadi, sera wala misimamo ya Chama bali MBOWE hafai, Mbowe CCM, mzee n.k. Chama cha Siasa hakiongozwi kwa mihemko ya Wanaharakati bali huongozwa na Wanasiasa. Kugombea Urais shauri jingine lakini sio timu moja kumnanga captain wenu. Lissu anazungumza kama Wakili mwanasheria na kesi ya Mbowe ipo mahakamani, kitu ambacho kinaharibu kabisa Demokrasia

.
 
Tumestuka

Lakini pia ungemuuliza museveni, nini hasa lilikua lengo lake kutaka kumuondoa Lissu kwenye nyazifa zote na kukataa asigombee Uraisi?
Sisi huu mpango tuliujua kutoka mwaka 2022 mwishoni. Mbowe aliandaa mazingira mazuri kwa mama Abdul
 
Sasa wewe kwa Akili zako unadhani CCM wamemtuma nani Kati ya hawa wote wanaogombea nafasi pale CHADEMA wasaidie watanzania wenzako tena ukiwa na Akili TIMAMU kabisa isiyo na chembe ya uchawa wa mtu yeyote.
 
Mbowe aloiongoza Chadema kwa miaka 20 na miaka yote watu wamekuwa wakisema Mbowe ni CCM. Mbona Chadema imekuwa chama Kikuu cha Upinzani kwa miaka yote hakijashuka? LIssu mwenyewe kaingizwa Chadema na Mbowe na kumwingiza moja kwa moja Kamati kuu. Mbowe wa CCM angetaka kuona watu kama Lissu, Wangwe, Heche, Wenje, Lema, Zitto, dr.Slaa, Msigwa, Sugu, Kina Halima Mdee na wengine wote woitikisa CCM ambao hawakuwepo miaka ya nyuma? Acheni matusi jamani Mbowe kawapokea kawavusha leo hana maana yoyote..
 
Wakati mbowe anavuta huo mkwanja chadema haikufa ila chadema ikiwa chini ya lissu itakufa ila uchawa mwingine pumzika mzee ulee wajukuu
 
Wakati mbowe anavuta huo mkwanja chadema haikufa ila chadema ikiwa chini ya lissu itakufa ila uchawa mwingine pumzika mzee ulee wajukuu
Upuuzi kama huu ndio ulonifanya nipumzike #Jamiiforums kwa sababu hamsomi content mkazielewa bali mnakurupuka na kutukana watu wazima pengine wazazi wanu. Na ndio.maana sidhangai kuona watu kama wewe mnashangilia Lissu bila kujiuliza uwezo wake bali kwa sababu analipiza kisasi.
 
Unamshauri lissu atukalipie siye wafuasi wake tusimseme mbowe ni mzee
 
Mzee pumuzika lea wajukuu umepitwa na wakati nyie ndiyo wazee mmeifikisha nchi namna hii ya ovyo bado unatetea uzee wako.
Nani amekuita urudi
 
Nimegundua baadhi ya watanzania wanapenda sana ugomvi.Lisu amefanikiwa kukuza kisasi chake na Mbowe na kila mtu asiyetafakari anafurahia kila anachosema Lisu.Hii ni hatari
 
MKuu kilichonifanya niandike makala hii ni kuitakia mema Chadema badala ya kushughulika na Mbowe. Chama ni kikubwa kuliko Mbowe ama hiyo nafasi ya Uenyekiti.
Wakati huu Chadema ya Wanasiasa wangekaa na kutunga mikakati ya kuiondoa CCM madarakani, na wale Wanaharakati wangepiga majungu Serikali ya Mama Samia toka wakati huu ili ikifika November wamevuta hisia za Wapiga kura zaidi, badala yake Chadema wanaanza kupotezana wenyewe.

Jiulize kwa nini? Kaanzisha nani hizi tuhuma jambo ambalo walitakiwa tu kutangaza Uchaguzi wao Mkuu tukasubiri kuona Wagombea. Infact nilisikia Mbowe hakutaka kugombea tena Uenyekiti isipokuwa Lissu ndiye kaingia na gia kwamba Mbowe kamtuma Wenje agombee nafasi yake na hivyo yeye atagombea nafasi ya Mbowe!

Think my brother, kwa hiyo ndio tuseme kama Mbowe asingemtuma Wenje ina maama Mbowe angebakia mru safi, Mwenyekiti hana udhoofu wanao usema leo? Lissu ana run kuwa Mwenyekiti sii kwa sababu ya kuongoza Chama bali kumkomoa Mbowe! Does this this sound right?
Well, kuhusu Kundi la watu wanaotaka Tanganyika, nenda vijiwe vyao utajua nasema nini. Binafsi niliwahi kuwepo huko nikaona chuki na upuuzi mtupu unaoendelea.
Kama sababu ya kudai Tanganyika ni Mama Samia sio Katiba basi dawa ilikuwa kuhakikisha anaondoka yeye, sio kumjengea hoja ambayo pengine yeye Rais anataka kuigawa Tanzania. Hizi ndizo Siasa za haki na kujenga na sii kubomoa.

Nguvu kubwa ya Chadema ingewekwa kwenye Upinzani wa itikadi, sera na sheria zinazowakwaza Watanzania ili ifikapo November, Chadema inajiweka katika.nafasi ya Ushindi lkn msikie vema Lissu ni ugonvi tu nani agombee Urais, nani awe Mwenyekiti nani Makamu na nafasi zote anataka yeye! Demokrasia ipi unayozungumzia?
 
Kwani hujui kuwa uchaguzi wa mwenyekiti CHADEMA ni mwaka huu?

Ulitaka wamuondoe mwenyekiti bila kufuata katiba kabla ya mwaka wa uchaguzi?

Katiba ya CHADEMA haina option ya recall.
Uchaguzi ungefanyika pasipo haya madudu ya kudhalilishana maana wote wako timu moja, sijui kama unanielewa? Hapakuwa na sababu wala haja ya Mimi kujua kinachoendelea huko Chadema. Aidha tungesikia wagombea kina nani kisha matokeo maana ni jambo lao - Upo?

Hata kama Mwenyekoti angekuwa Lissu halafu Mbowe akaibuka na hoja kama hizi na wapambe zake ningempinga na kuandika haya haya nayo andika leo. Wrong move is wrong haijalishi nani kafanya.

Leo hii mimi nasikia za ndaaani kabisa msemo wa Kadomomo. Hii ni vita vya ndani ya Chama kama ilivyokuwa kule NCCR na CUF inanipa hofu ya matokeo hili naliweka wazi na mtakuja nambia. Historia ipo wazi Yuko wapi Mbatia NCCR na Lipumba CUF leo hii wamebakia historia. Huko ndiko Chadema inakoelekea
 
Sehemu ya demokrasia ni uwazi, wanatekeleza jina la chama chao.

Tatizo ni uongo tu, kama jambo kweli uwazi si tatizo katika demokrasia.
 
Sehemu ya demokrasia ni uwazi, wanatekeleza jina la chama chao.

Tatizo ni uongo tu, kama jambo kweli uwazi si tatizo katika demokrasia.
Uwazi kwa wahusika tu, hata ukiwa na mkeo unafunga milango na madirisha, uwazi unabakia kwenu pekee 😁😁
 
Uwazi kwa wahusika tu, hata ukiwa na mkeo unafunga milango na madirisha, uwazi unabakia kwenu pekee 😁😁
Kama unaona habari hazikuhusu zipotezee tu. Hujalazimishwa kuzifuatilia.

Wanaoona zinawahusu watafuatilia.

Hizi ni habari za kuendesha chama cha kitaifa, si habari za mke na mume kulala.

You are comparing apples to oranges.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…