Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

Hakuna harakati za kumuondoa Mbowe bali kuna mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa Chadema. Box la kura ndiyo msema kweli,mengine uliyoelezea ni upambe na matamanio yako.
 
Mleta uzi bila shaka yoyote ni nyumbu wa Mbowe
 
Kama unaona habari hazikuhusu zipotezee tu. Hujalazimishwa kuzifuatilia.

Wanaoona zinawahusu watafuatilia.

Hizi ni habari za kuendesha chama cha kitaifa, si habari za mke na mume kulala.

You are comparing apples to oranges.
Mkuu hujui kama ukituma clip ya mambo ya chumbani kwako itatazamwa na kila mtu na ita trend na kuzungumziwa sana? Ndio hayo yotokea kwa Chadema
 
Tunajua maccm mnataka Mbowe aendelee kwa vile amefika bei.
 
Mkuu hujui kama ukituma clip ya mambo ya chumbani kwako itatazamwa na kila mtu na ita trend na kuzungumziwa sana? Ndio hayo yotokea kwa Chadema
CHADEMA ni chama cha kitaifa, si habari za chumbani.

Unapolinganisha vitu, linganisha vinavyolinganishika.

Again. You are comparing apples to oranges.
 
Mkuu hujui kama ukituma clip ya mambo ya chumbani kwako itatazamwa na kila mtu na ita trend na kuzungumziwa sana? Ndio hayo yotokea kwa Chadema
Hiyo ni minyukano ya ndani tu ndani ya vyama nyakati za uchaguzi
 
Umeandika as if ni hila, No ni utaratibu wa chama, itapigwa kura kuona nani atafaa kuwaongoza

Mbowe amefanya kazi nzuri, but kwa sasa chama hakihitaji mwanasiasa wa taratibu, kinataka aggresive politics, ili watoke hapo
 
Na nyumbu wa Sultan Mbowe mnajiona hii Chadema kama kampuni yenu binafsi.
 
Ukipumzika jamii forums hiyo ni hasara kwa nani?
 
Kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu hakutaisha 2025, kuna 2030, 2035, 2040 etc. Je mleta mada unata Mbowe aendelee kutawala mpaka afie kwenye kiti simply because kuna uchaguzi nchini kila baada ya 5years?
 
Kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu hakutaisha 2025, kuna 2030, 2035, 2040 etc. Je mleta mada unata Mbowe aendelee kutawala mpaka afie kwenye kiti simply because kuna uchaguzi nchini kila baada ya 5years?
Kuongoza Chama sii sawa na Kuongoza NCHI. Nitarudia kusema Kujenga Chama ni sawa na contactor wa ujenzi wa nyumba ya kujitolea. Haihitaji kubadilisha Mwenyekiti au safi na viongozi maana ni kazi ya Kujitolea haina malipo. Na kama kuna mmoja wao hafai ataondolewa na Mkutano Mkuu au Kamati kuu kama walivyoondolewa kina Zitto, Kitila, Dr. Slaa na wengineo, labda nikuulize alipoondoka Dr.Slaa au Zitto Chadema kulifanyika Uchaguzi? Kifungu gani cha Sheria kilimuondoa Zitto lakini hakiwezi kumuondoa Mbowe?

Halafu unasikia watu wanasema Mbowe asingeweza kuondolewa bila Uchaguzi.
Rudini nyuma issue ya kija Zitto nani alokuwa mpambe wa Mbowe? Sii huyu huyu Lissu mpaka wakatukanana matusi mazito, Zitto akisema haongei na kitu kama mbwa bali mwenye mbwa au nakosea? Issue ya Dr. Slaa alokuwa akimpiga madongo Slaa muda wote nani kama sio Lissu huyu huyu?

Leo Lissu kamgeuka Kiongozi wake tena basi aliomba kikao cha faragha yeye Mbowe na Mnyika wagawane vyeo. Mbowe alikataa, yeye akataka sijui Urais, Uenyekiti au vyote. Yote haya yanavuja sasa hivi na Lissu atakataa yote mbele za watu kwa sababu anajua sana kujifanya mhanga. Labda nianze kuwamiminia clip zake mpime wenyewe..
 
lengo kuu ni ili wapate mtu ambaye hatakuwa analamba asali. uwepo upinzani halisi utakaoiwajibisha serikali inayouza nchi kwa mwarabu.
Lakini nchi ikiuzwa vatican au kwa mjrumani au kwa mbelgiji hakuna nenoi.
 
Ni bora CCM iwe marakani milele kuliko wakina Mbowe ndio wao wawakilishi wa demokrasia mavi.
Chama kimejaa ukabila,kazi kubwa ni kula ruzuki, hadi leo hamna ofisi,............yeye mbowe KAZI yake ni kuona namna gani nzuri anapaya pesa kupitia siasa na sio kuwakomboa wananchi,.
Yes tunataka kuona wakina Lissu wanavunja huu upumbavu,ama CCM iendelee kutawala milele na sio eti kushabikia SACCOS YA kina mbowe
 
Diligency
 
Kwani uchaguzi wa CDM unafuata ratiba ya uchaguzi mkuu wa nchi? Kama wana uchaguzi wao kwanini ushangae muda kuwa sasa kama muda wake umefika?
 
Kwani uchaguzi wa CDM unafuata ratiba ya uchaguzi mkuu wa nchi? Kama wana uchaguzi wao kwanini ushangae muda kuwa sasa kama muda wake umefika?
Uchaguzi upi wa CCM? Mkuu wangu CCM Uchaguzi wa Mgombea Urais ndio hufanyika na anayeshinda ndiye automatically anakuwa Mwenyekiti wa Chama kwa sababu mgombea ni yeye pekee. Anapigiwa kura ya ndio au Hapana. Kwa hiyo ni baada ya kuwa rais ndio unapata Mwenyekiti wa CCM, siku wakishindwa Urais sijui Mwenyekiti atakuwa nani..😁😁😁
 
Uwazi kwa wahusika tu, hata ukiwa na mkeo unafunga milango na madirisha, uwazi unabakia kwenu pekee 😁😁
Acha hizo mzee mwenzetu, tumefika hapa tulipo kama taifa kwa sababu ya UNAFIKI. Unafiki umekuwa kama ugonjwa wa kuambukiza na muda umefika wa kuiita kolea kwa jina lake na si kijiko kikuubwa!

Hii ni JF where we dare, remember? Umesahau jinsi baadhi yetu nyakati zote tumemkoma nyani giledi bila kumuangalia usoni? Hizo siasa zako kwa sasa zimepitwa na wakati...Unafiki basi, CCM has to go!
 

Wapi nimeuliza uchaguzi wa CCM? You lack comprehension skills.

Nimesema uchaguzi wa CHADEMA (CDM) ni kila baada ya muda gani? Huu uchaguzi wa sasa ni muda wake au wameforce kufanya uchaguzi muda wakati muda haujafika?
 
Kwanza nitoe shukran zangu kwako kumbe bado mpo? Mkuu nadhani unakumbuka sana kwamba mada nyingi zamani mlikuwa mnakataa mwisho wa siku mnakutana na ukweli nilousema. Toka wakati ule kina Zitto, January, Maria Sarungi, Kitila, Nape, Mnyika wakiwa hapa mara nyinti nilikuwa upande msoupenda.

Sasa kumkoma nyani sii lazima iwe Mbowe wakati najua fika Lissu ndiye hafai kuwa Kiongozi bali ni Mwanaharakati na wakili mtetezi wa hata Jambazi. Lissu anaweza mtetea jambazi alokamatwa na nyala za Serikali na akashinda kesi. Ni mjuzi wa kujenga hoja za UONGO na akashinda.


Mimi mwananchi siwezi kutetea Ushindi huo, nitasema Ukweli ninao uona na naoujua. Siandiki kitu kama sina hakika nacho. Niliwahi sema humu zamani kuwa namjua Lissu kuliko mnavyodhania. Alisomeshwa Marekani na LEAT ambayo wafadhili wake ni Ford Foundation ni tapeli mpenda sifa na majivuno kuwa yeye ndiye Alfa na Omega hakuna zaidi yake.

Hata wakati wa Magufuli, Lissu alipinga Sheria mpya ya mikataba ya madini na nishati akisema mikataba hiyo ni ya Kimataifa hatuwezi kuivunja. Lakini haada ya mwendazake akarudi nchini tukaanza kudaiwa madeni hayo ili mradi tu muendelee kumchukia Magufuli - Nawaelewa.

Kule west Bukina Faso, Chad, Mali n.k wamefuta mikataba ya zamani, wamekubali kulipa madeni yote, leo wako HURU na mfano bora kwa viongozi wa KiAfrika kila mtu anawaona hawa ndio Viongozi tunaowataka.
Senegal inafuata na baadhi ya nchi chini ya Wafaransa wanafuata njia hiyo ya Magufulification. Huku kwetu sisi ni malumbano tu wenyewe kwa wenyewe. Haya kama sii matunda ya Umaskini na Ujinga kitu gani kimetusibu?
 
Wapi nimeuliza uchaguzi wa CCM? You lack comprehension skills.

Nimesema uchaguzi wa CHADEMA (CDM) ni kila baada ya muda gani? Huu uchaguzi wa sasa ni muda wake au wameforce kufanya uchaguzi muda wakati muda haujafika?
Samahani nime qoute vibaya, hoja sii Uchaguzi nachozungumzia ni haya malumbano baina ya Lissu na Wapambe wake kumshusha Mbowe kiasi hiki hata kabla ya kusimama mbele ya wapiga kura na kuomba kura zao. Mbona zamani haikuwa kutokea hivi? Kuna mgombea alikatazwa kugombea? Sioni sababu kabisa ya malumbano na character assassination ndani ya Chama kimoja
Hakutakuwa na AMANI baada ya Uchaguzi Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…