Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

None sense. Sasa kama sio ccm miaka inspiring na moja ya uongozi wake haijamtosha kweli?
 
Kwangu mimi Lissu ni shujaa, ameonesha uozo mkubwa sana ulioko CHADEMA. Kama hatuutaki huu ukweli huu ndani ya CHADEMA basi hatuko entitled kuutaka ukweli kuhusu CCM na Serikali yake!
 
Uchaguzi ni harakati? Kutia nia ni dhambi?
 
Na nyumbu wa Sultan Mbowe mnajiona hii Chadema kama kampuni yenu binafsi.
Team Lisu kaanzisheni chama cha wanaharakati na wapiga kelele tuone mtakifikisha wapi.

Ni mtaalam wa sheria, akaanzishe chama, mkarundikane huko tuuone uwezo wa Lisu.
 
Nadhani lengo ni kukirudishia chama makali yake!
 
Team Lisu kaanzisheni chama cha wanaharakati na wapiga kelele tuone mtakifikisha wapi.

Ni mtaalam wa sheria, akaanzishe chama, mkarundikane huko tuuone uwezo wa Lisu.
Pumbavu wewe Chadema ni ya wanachama siyo mali binafsi ya Mbowe na nyumbu wake,tutabanana humo humo na Lissu ndiye mwenyekiti ajaye. Tuna mchango mkubwa sana kwenye chama hicho na yaelekea wewe ni mccm hakuna mwanachadema anayeombea mgawanyiko, mtaji wa chama ni wanachama na kwa taarifa yako baada ya uchaguzi Chadema itakuwa imara zaidi na moja zaidi.
 
We unamsanifu mbowe huku ukidhani unamfagilia ila hujui kwasabb ww ni mjinga!
Kati ya Lissu na mbowe nani ana uchu wa madaraka??.
Yaani mtu aliyekalia kiti miaka 21 bado anataka tena miaka mingine mipya mi5 akiamini kuna jambo hakuliweza kwa kipindi chote cha nyuma hakulifanikisha lakini atalimudu kwa miaka 5 ijayo wakati dalili zote kwamba kwasasa kawekwa mfukoni na ma ccm kwamba akiendelea ndio hali itakuwa mbaya zaidi ziko wazi kabisa hivyo inatakiwa awekwe kando kwa faida ya chama!.
Lissu anaungwa mkono na wanachadema wengi zaidi tena walio smart vichwani tofauti na upande wa mbowe, chunguza vizuri!!..
 
Ujinga mtupu, Huyo Lisu na usmart wake akaanzishe chama kisha mkafanye usmart wenu huko.

Mnakuwa smart halafu mnataka kufanya mapinduzi ya kukiuwa chama, halafu mkikipindua ndio mnadhani mtapata wanachama wapya chadema, mtawatoa wapi kwa ujinga huu mliouanzisha?

Huyo smart analiye upande wa Lisu ni nani hasa?

Mnampasifa asizokuwa nazo, mnajiona mnaakili wakati wajinga watupu.

Na hamuendi kokote na mihemko yenu ya kitoto hii.
 
Hahaha mihemko ya kitoto hii halafu ndio mnatafuta muwe ndani ya chadema?

Bora kife tuone mnasnzisha chenu mkajazane huko tuwaone mnavyohangaika na mihemko yenu.

Mnaropoka hovyo kuanzia mgombea wenu, nanyi ndio balaa, muingie chamani kwa lipi?

Subiri tarehe 18 CCM wameitisha mkutano, utamuona Lisu anavishwa skafu na kofia ya ccm ndio utajiona usivyojielewa.
 
Maadam nimejieleza vya kutosha na bado naona kuna upotoshaji juu ya kauli zangu kuhusiana na vijembe wanavyotupiana viongozi wa Chadema tena kwa tuhuma nzito ambazo kiuhalisia hazikushughulikiwa miaka miwili au mitatu nyuma kupitia vikao vya baraza la Maadili, Kamati kuu na Baraza kuu kama navyoisoma Katiba ya Chadema isipokuwa inakuja kuibuka mitaani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Chama na kuwagawa wanachama katika makundi ya uhasama.
Nachelea kusema yaonyesha wazi Chadema hawakujifunza kuputia yalotokea kule NCCR wala CUF, AMA Huko Chadema Mdudu kaingia ndani ya kokwa.. Maasalaam
"Chicken have come home to roost"
 
Miaka inashirini na moja ni mingi sana. Hata kama wewe ni baba mtoto wako wa mwisho akifikisha miaka 21 inakuwa ni wakati sahihi wa kuaanza kuwapa watoto majukumu yako. Kwanza kwa kiongozi mwenye akili hawezi kukaa kwenye nafasi moja kwa zaidi ya miaka ishirini. Hata Salum kikeke alivyo ona amekaa BBC kwa mda mrefu aliamuwa kuondoka. Sasa Mbowe ni kitu gani kinamfanya aendelee kung"ang'ania uenyekiti ? Kama kweli niya yake ni kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa manufaa ya watanzania anaogopa nini kumpa mtu mwingine jukumu hilo.
 
Tukuulize wewe, Mbowe ana faida gani chamani?
 
Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa TAA toka mwaka 1953, Chama kikabadili jina na kuitwa TANU mwalimu bado akawa Mwenyekiti, wakabadilisha tena jina kuwa CCM, Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti na wala hakujiuzuru Uenyekiti 1984 bali alijiuzuru Urais, akaendelea kuwa Mwenyekiti kwa mwaka mmoja au miwili kabla Ally Hassan Mwinyi hajachukua Uenyekiti wa Chama kulingana na mfumo wa Uongozi wa CCM.

Sasa labda nikuulize wewe kwa nini Mwalimu alikuwa Mwenyekiti wa Chama kwa miaka zaidi ya 30? Ukiweza nambia sababu nitarudi tuendelee na mjadala.. Kisha hii sio hoja yangu mimi pengine hamuwezi kusoma hoja zangu mnachukua maelezo kama yalivyo na kuongeza yenu juu yake.

Hoja yangu ni hii, Kwa nini Viongozi wa Chadema wanavuana nguo hadharani kwa TUHUMA NZITO ambazo zingeweza shughulikiwa toka miaka ilopita (2021/22 - 2024) kupitia vikao vya ndani vya Chama? Kama Mbowe ni CCM walishindwaje kumuondoa karika Uchaguzi uliopita ama kuitwa na kamati ya maadili kujibu tuhuma hizo ila wamesubiri Uchaguzi unakaribia na Uhasama kuanza kutokea baina ya Wagombea?

Lissu kaeleza wazi kwa nini anagombea Uenyekiti ni Kumkomoa alomtuma Wenje kugombea Umakamu. Hii statement pekee inawapeni picha gani kama sio katangaza vita ya wenyewe kwa wenyewe?

Hivi UMAKAMU ilikuwa nafasi yake peke yake au? na kwa nini anasema tena bila aibu wala kuficha ati alikuwa na Kikao cha siri baina yake na Mbowe ili kugawana nafasi za kugombea? Mbowe alikataa akisema bado hajaamua - Hii kweli ndio Demokrasia?

Wakati Vyama vya Siasa nchi nyingine wanapanga mbinu kujua Strength na Weekness za Chama tawala, Chadema wanapambana wenyewe WHY?

Nikidhani Uongozi wa Chama ni KUJITOLEA, hii vita ya nini? Ina maana moja tu, KUNA ULAJI ndani ya Uongozi wa Chama. Na kama Mbowe kweli hupokea FEDHA kutoka CCM kukiendesha Chama ama zake, basi bila shaka hao wengine pia wanataka kupokea hizo FEDHA maana wanajua zinatokaje kwa Ushahidi walonao.

Vita ya Chadema sio MBOWE wala LISSU bali vita ya Chadema ni CHUMIA TUMBO hali ambayo haikuwepo miaka mingi nyuma and it seems Viongozi wengi hawana source of income baada ya kukosa Ubunge, imebakia ndani ya Chama kuna vijisenti vinatembea. That's my perception na huu utakuwa mwisho wa Chadema kama Chama Kikuu cha Upinzani.
 
Wewe ni mwehu mwingine kwa kweli. Ndio demokrasia
 
Mkuu Mkandara,
Nashangaa sana, wewe ndio umeandika hayo?
HAkuna mwingine, nisubiri nitarudi February hapa kijiweni tujadili, kwa sasa naishia hapa๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Nyerere alikuwa dictator kama dictator wengine. Tafauti yake na madictator wengine ni kwamba Nyerere alipenda nguvu ya madaraka tu . Hakutaka nguvu ya pesa kama madictator wengine. Ukitowa hilo tu la kutojilimbikizie mali. Vingine vyote ni sawa na kagame, Mseveni au wengine kama hao. Hiyo ndio sababu ya Nyerere kutawala nchi miaka 24, na kuwa mwenyekiti miaka 30.

Sasa kama na Mbowe anataka kuingia kwenye orodha ya madictator kama hao aendelee kuwa mwenyekiti wa maisha wa chadema tuone chadema itaishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ