Umeandika vyema mkuu japo huu utaratibu wa kupimwa pressure,sukari n.k bila kupenda ni tatizo jingine. Umejikata kidole cha mguu, unaenda pimwa pressure. Pia binafsi nijuacho, ugonjwa kama pressure watu wengi wanatembea nao na pale uendapo kupimwa bila kupenda ndio unazidi kwani watakujengea hofu na pia madaktari wetu wengi sana hawana hekima ya kuongea na wagonjwa wa pressure.
Mama yangu kuna siku nilimpeleka hospitali kwa ajili ya kuumwa miguu. Pale masijala wakampiga Pressure. Ikakutwa kubwa, wakaanza kujiita madaktari wakawa watatu na kuanza mjadili. Tena wakaacha kuangalia tatizo la miguu, wao wakaanza mueleza kuhusu pressure ilihali haumwi sehemu yoyote wala hajawahi kuwa na tatizo hilo.
Wakamtengenezea hofu sana yule mama. Nashauri huu, utaratibu sio mzuri. Mtu atibiwe tatizo alilonalo na sio kuanza chokonoa pressure na UKIMWI kilazima.