Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Nimeipenda hii.
Mleta mada pia asante. Leo nimepata kitu kipya kumbe Yuda alikuwa mtunza fedha! Na kumbe Yesu kuna kipindi aliagiza hela zikachukuliwe kwa samaki... Tumboni/mdomoni mwa samaki!!.
 
Mkuu nakuelewa ila hii argument kuwa waligawana lile vazi sababu ya umaskini wao hivyo walitaka kwenda kulivaa ndio nina mashaka. Nadhani kugawana kwa kile vazi kulikuwa na maana nyingine maana ukumbuke kwanza lilikuwa lishachanika nankuchakaa kutokana na mijeledi ya maana ya hao hao askari.

Sasa vazi ambalo lishachakaa wangelitaka vipi kulivaa tena.? Kumbuka pia wale jamaa walikuwa ni askari wanaolipwa mshahara hivyo hawawezi kuwa maskini kihivyo.
 
Fuatilia kwa miaka 3 aliyofanya kazi ya kueneza neno la Mungu hakufanya kazi nyingine zaidi. Alikuwa ni nenda huku au huku. Hakuishi kwao tena. Mpaka wazee wa familia (ndugu zao) wakamwita kumuambia aachane na kuhubiri injili amtunze mama yake. Na ndio sababu ya muujiza wa Kana, maana hata nduguze walikuwa hawa mwelewi! Ule muujiza ulisaidia sana ndugu kuanza kuelewa kuwa huyu si binadamu kama wengine, na ana mission maalumu!

Wale thenashara na wafuasi wengine walikuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida muda mwingi. Alikuwa anakuwa nao "occasionally". Ila mara zote hakuwa pekee, alikuwa ana andamana na 2 au 3. Jaribu kuchimba zaidi utajua.
 
Na Yesu alikuwa akivaa viatu vya uhakika vya thamani ya juu vya kufunga na kamba hadi Yohana akasema sistahili hata kugusa Ukiona filamu yeyote au picha yoyote ikimuonyesha Yesu yuko pekupeku miguuni hana viatu ujue imetengenezwa na wasiomjua Yesu wanaoamini Yesu alikuwa Maskini!! Yesu alikuwa na viatu vya nguvu

Marko 1:7​

YOHANA AHUBIRI

''Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.
 
Mkuu nakuelewa ila hii argument kuwa waligawana lile vazi sababu ya umaskini wao hivyo walitaka kwenda kulivaa ndio nina mashaka. Nadhani kugawana kwa kile vazi kulikuwa na maana nyingine
Lete hiyo maana ya zaidi ya kwenda kuvaa waligawana za nini? Kwanza mali ya marehemu ni mirathi ilitakiwa mali za marehemu Yesu ikiwemo hizo nguo ilitakiwa wakakabidhi kwa warithi.Wao wakaamua kugawana!!! Mirathi ya marehemu kabla haijafunguliwa.Kama hawakwenda kuvaa waligawana za nini?
 
Anaenda mgahawani, anaagiza mikate miwili na kikombe cha divai.
Yeye na wafasiri wake wanakula na hakiishi hadi watakapo Shiba.
 
Zaka na sadaka walikuwa wanakula wakina kayafa.

Yeye hekaluni alikuwa anakagua tu watoa sadaka. Akampenda sana bibi mmoja aliyetoa senti yote na kuwaponda matajiri waliokuwa wanatoa sadaka kwa mbwembwe.


Hakuwa kwenye payroll ya Hekalu
Ahahahah
 
Kuna mstari nakumbuka aliwaambia waende wakanunue vitu kwa ajili ya kalamu na walikuwa hawana kitu.
Akawaambia nendeni tu, Hii naonesha alikuwa na maisha ya kuunga unga tu. Na hakuwa mkwasi.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hapa nadhani ni pale alipotaka Punda kuingia Naye Yeriko Kifalme. Aliwaambia mumchukue mkimkuta mwenye Naye akiwauliza wamwambie Yesu anamtaka.


Hapa nadhani alimrudisha na hakuwa na haja ya kumiliki punda wakati kesho yake anaanza suluba.
Ahahahah
 
We jamaa usitupige kamba😆😆, ni wapi panaonyesha Yesu alikuwa anaweka pesa kwenye matumbo ya samaki!
 
We jamaa usitupige kamba😆😆, ni wapi panaonyesha Yesu alikuwa anaweka pesa kwenye matumbo ya samaki!
Angeenda kuchukua pesa kwenye hilo tumbo la samaki kama hakuweka? Alikuwa ana witdraw pesa yake aliyo deposit kwenye tumbo la samaki
 
Baada ya kufa nani alilithi Mali zake?
 
Kwahiyo Yesu hakuwa Masikini kama tunavyoaminishwa?
Wewe jiulize anakwambia Yesu alikuwa maskini wakati alilisha chakula maelfu ya watu wakala na kusaza .

Maskini mlo wake tu shida .Maskini aweza lisha maelfu hadi wakasaza chakula? Shituka mafundisho kama hayo

Mafundisho ya uongo hayo.Yesu hakuwa maskini
 
Haa haa haa Mungu aliamua kukupa hiyo

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…