Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Biblia ipo wazi kuwa.
Baada ya Yesu kufa alienda kuzimu, napo alipofika aliwahubiria injili wale ambao walikuwa kule..

Na ukiona calculation za ki mbingu, Yuda kama alitengenezwa kumsaliti Yesu na kusudi apate kutubia ikabidi ajiue kitendo cha kujiua akawa amejitanguliza kuzimu na probably Yesu alivyofika kuzimu ni lazima Yuda aliiomba toba na akawa mmoja ya waaminio wapya kutoka kuzimu.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
Kweli alishuka kuzimu na ndiyo maana Bible inasema iliibuka miili ya watakatifu watu wakawaona, ila habari ya Yuda hiliishia pale alipo jinyonga huko kwingine sijui, ujue kuna watu wabishi huenda hata huko kuzimu wapo waliokataa kuamini.
 
Naona

Unaanza kumfitini Yesu.
Yesu aende kuzimu kutubisha watu enzi za Yuda alafu sisi huku tukidedi tunapambana na hali zetu.

Hapana

Yesu alikuwa amenyooka
Angebaki huko huko hadi Leo ili kuonyesha consistency.
Kweli alishuka kuzimu na kumnyang'anya shetani funguo za ufalme wa mbingu, soma Bible utayaona maanadiko hayo, Na Ile sala ya Nasadiki inasema hivyo!
 
Kwahiyo Yesu hakuwa Masikini kama tunavyoaminishwa?
Wewe jiulize kiongozi anakwambia Yesu alikuwa maskini wakati alilisha chakula maelfu ya watu bure .Wakala na kusaza .

Maskini mlo wake tu shida .Maskini aweza lisha maelfu ya watu bure hadi wakasaza chakula? Shituka mafundisho kama hayo akili kichwani unayo

Kanisa linalifundisha mafundisho kama hayo kuwa Yesu alikuwa maskini unatakiwa kuondoka spidi hata bila kuaga uongo wamezidi mno wamepitiliza.

Mafundisho ya uongo hayo.Yesu hakuwa maskini
 
Hata mazishi yake alizikwa na Tajiri Bilionea Yusuf wa Alimataya kwenye kaburi la matajiri.Hakuzikwa na malofa

mafuta tu ya kujipaka Yesu alikuwa akijipaka ya bei mbaya hadi Yuda Iskariote akashangaa, Maria Magdalena alipokuwa akimpaka yale mafuta akasema mafuta ghali haya Yesu unapaka loo.Yesu akamwambia mwache anipake wewe yuda iskariote kama umezoea kujipaka mafuta ya nazi utajijua akaendelea kujipaka
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]yaani nimecheka hadi tosha kwenye mafuta ya nazi.
 
Hata mazishi yake alizikwa na Tajiri Bilionea Yusuf wa Alimataya kwenye kaburi la matajiri.Hakuzikwa na malofa

mafuta tu ya kujipaka Yesu alikuwa akijipaka ya bei mbaya hadi Yuda Iskariote akashangaa, Maria Magdalena alipokuwa akimpaka yale mafuta akasema mafuta ghali haya Yesu unapaka loo.Yesu akamwambia mwache anipake wewe yuda iskariote kama umezoea kujipaka mafuta ya nazi utajijua akaendelea kujipaka

Hahaha

Dah
 
Kweli alishuka kuzimu na ndiyo maana Bible inasema iliibuka miili ya watakatifu watu wakawaona, ila habari ya Yuda hiliishia pale alipo jinyonga huko kwingine sijui, ujue kuna watu wabishi huenda hata huko kuzimu wapo waliokataa kuamini.
Nakuambia hivi...
Mission ya Yesu ilikuwa planned KWA kila kitu.

Yuda si mpumbavu ku msnitch Yesu.
Na Mungu angeonekana hayupo fairly kama Yuda asingepata nafasi ya kutubia uovu wake.

Baada ya Yuda ku msintch Yesu.
Alijitundika na akatangulia kuzimu.
Na Yesu alimkuta Yuda kuzimu.

Probably Yuda alisaidiki Tena KWA Yesu na akapata neema ya wokovu.
Ni mpumbavu pekee kama hasingefanya hayo.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Yesu alikuwa na Pesa nyingi sana kuliko watu wa dini wanavyotueleza.

Ushahidi.
1: Alikuwa na Muhasibu. MTU binafsi bila kampuni wala biashara kufikia hatua ya kushindwa kutunza kipato chako hadi Uwe na Muhasibu basi utakuwa na Pesa nyingi sana.

2: Aliwazuia mitume wasifanye biashara zao. Aliwakuta jamaa wakinapetro ni wakokozi na wavuvi nguli akawaambia waache alafu wamfuate.
Kulisha breakfast, lunch na dinner wanaume 12 wasio na Kazi miaka mitatu mfululizo inabidi Uwe na Pesa. Ushahidi Baada ya kufa Petro aliwashawishi warudi kwenye Biashara zao.

3: Hakuna kifungu Yesu kaishiwa Pesa au kashindwa kufanya muamala wowote kisha hana salio. Aliwahi kudaiwa kodi ya hekalu, akamtuma Petro akavue samaki aliyekuwa na Pesa tumboni.

4: Muhasibu wake alikuwa mwizi na mwenye uchu wa Pesa. Huku tunaona makampuni maduka Yenye wahasibu wezi huwa yanafirisika. Yuda hakuwahi kufirisi mkoba wa pesa za mwalimu wake Yesu.

Wakuu Yesu alikuwa yuko vzr kiuchumi.

Sasa najiuliza nini nilikuwa chanzo chake cha fedha ikiwa

Alikuwa hana biashara
Hakuwa na gawio LA sadaka masinagogini na hekaluni?

Je alikuwa anawafadhili?

Je alikuwa anakusanya Sadaka kwenye mihadhara yake?

Je Alikuwa anashushiwa kimiujiza.?
Hata kanzu hajawahi kununua nyingine maisha yake yote, wala hatukuambiwa alipokuwa anaifua anatoa wapi ya kubadilisha, hakuwa na nyumba lakini alilala kila siku tena miji tofauti. NB Ukibarikiwa na Mungu vyote utapata.
 
Sasa mara ya mwisho wajuba wanaogombania kanzu yake ilikuwa haina sehemu iliyoshonwa angenunua wapi kanzu kama hiyo
 
Nimeipenda hii.
Mleta mada pia asante. Leo nimepata kitu kipya kumbe Yuda alikuwa mtunza fedha! Na kumbe Yesu kuna kipindi aliagiza hela zikachukuliwe kwa samaki... Tumboni/mdomoni mwa samaki!!.
Kama saizi unavoweza mtuma muhasibu bank
 
Yesu alikua na mpunga wa maana maandiko yanaonesha kwenye Luka 7 au 8 kuwa yule mwanamke Maria Magdalena alikuw Ni tajiri Sana inasemekana eti..
Alikuwa malikia wa magda na alimsponsor Jesus kila kitu.
Hv naeleweka naposema "kila kitu" nasikia pia Yesu alimwelewa Sana mpaka akamfanya mkuu was harakati za injili baada ya yeye kubanwa na warumi....
Baadae warumi wakamsaka Magdalena akakimbia mpaka ufaransa,mpaka akajifungua katoto ka kike kakaitwa Sarah Sasa hapa Bado Kuna tongotongo kama iyo mimba ilikuwa ya Jesus au laah.
Bhasi Petro alivyojua Magdalena kakimbia akaamua kuchukua jukumu ila ukweliii Ilo jukumu akupewa yeye Kwanza alikuwa ashamzingua Jesus.

Ila Yesu huduma yake ilikuwa na masponsor wengi ila ye mwenyeee alikuwa wa kawaida Sana .
 
Hii mpya kwangu.
 
Alikuwa mjanja mjanja tuu mzee wa kubumba
Kama hana credible sources za income
 
1petro 3:18-20

18 Kwa maana Kristo naye aliteswa Mara moja kwa ajili ya dhambi,mwenye haki kwa ajili yao wasio na haki,ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa,Bali roho yake akahuishwa,
19 ambayo kwa
hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

hapo tunaona mission
ya Yesu baada ya kwenda kuzimu,alihubiri injili kuanzia watu waliokuwa tangu kipindi cha nuhu hadi ambao siku anakufa..

baada ya hapo injili imefungwa na tumebakiwa na kipindi cha neema pekee. Means kwamba hivi SASA injili tunaipata kabla ya umauti tukishakufa hatuwezi kupata injili Tena.!

Mkuu maandiko yanasema mtu akifa roho inarudi kwa Mungu na mwili unaenda kaburini sasa ilikuwaje tena Roho wa Yesu aende kuhubiri kuzimu?
Andiko tena linaeleza roho waliohubiriwa ni watu wasiotii kipindi cha Nuhu, hivyo basi Roho wa Yesu alihubiri kipindi cha nuhu lakini watu hawakutii kwa kuwa walikuwa katika vifungo vya dhambi na ndio maana waliangamia na mambo hayo ni sawa na sasa ambapo watu wanahubiriwa kuhusu ubatizo na toba, wanaotii wataokolewa na wasio tii wataangamia kama ilivyokuwa kipindi cha nuhu kwa kuwa Roho aliyekuwa akihubiri kipindi cha nuhu ndio huyo huyo kwa wakati huu.
 
Duh.
I wish Jf ingekuwa na sehemu ya voice.

Mbona maandiko yapo wazi hapo kabisa??

Hebu Soma Tena na tena.. uhitaji kutumia rocket science kuelewa.

Maana yapo wazi mnoo

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom