Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #201
Prince...tembo wakigombana zinazopata tabu ni nyasi siku zote....ebu ngoja....nikae kimya
Wala mimi si tembo wala sina ugomvi na mtu.
Nimeandika historia ya kuundwa kwa TANU kama nilivyoelezwa na wazee wangu bahati mbaya kuna watu hawawajui wazee wangu wala historia yao wanaipinga.
Sawa.
Sina tatizo na hilo nimeandika iko kwenye kitabu na wala simlazimishi mtu kuikubali.
Wala mimi sijafanya ugomvi na Chuo Cha CCM Kivukoni kwa kuandika historia yao ya TANU iliyowafuta wazee wangu.
Wao wameanza historia ya TANU na Julius Nyerere 1954.
Mimi nimeanza historia ya TANU na Kleist Sykes 1929.
Vitabu vyote viwili ni historia ya TANU.
Sasa tatizo liko wapi?