Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Ni kweli kabisa!
Mimi nilijaribu kueleza ni kitu gani wakati ule kilisababisha pesa yetu ishuke thamani 🙌👍 Wakati ule !
 
Kwa hiyo ndiyo kusema Wachumi wote waliojazana serikalini wamekosa kabisa suluhu ya kuirejesha thamani ya shilingi yetu!! Yaani miaka inavyozidi kwenda na thamani nayo inazidi tu kushuka!!
Utawala wa Rais Benjamin William Mkapa kwa kiasi chake ulijitahidi Sana katikà ku-deal na suala hili la stability ya sarafu ya nchi hii ya Tanzania. Rais Mkapa alijitahidi Sana kwenye suala hili, na Mpango huo wa ku-stabilize shilingi ya Tanzania aliuita kwa Jina la "Kurekebisha Uchumi."

Bei za bidhaa mbali mbali zilibaki stable katika kipindi chote Cha Utawala wake, hazikubadilika badilika, japokuwa pesa ilikuwa ngumu Sana kupatikana. Pesa ziliadimika mitaani.
 
Economic development vs Economic growth 📈
Wachina wanajitahidi sana pesa yao isipande thamani.

Ikipanda wanaishusha kwa makusudi.

Kimkakati, ili uchumi wao unaotegemea exports ufanye vizuri.

Wanaona pesa yao ikiwa na thamani ndogo ndiyo itachochea uchumi wao kuwa mzuri. Kwa kuchochea exports zaidi.

Pesa kuwa na thamani kubwa au ndogo si tatizo.

Tatizo ni, una mkakati gani wa kuitumia thamani yoyote ya pesa yako ili uwe na uchumi mzuri.

Tatizo hatuna strategy hata ya kutumia hiyo pesa isiyo na thamani kuwa na uchumi mzuri.

Tungekuwa na strategy kama ya China, tungeweza kuipigania pesa yetu isipande thamani na vile vile kujenga uchumi mzuri wa export.

Tatizo si thamani ya pesa, thamani ys pesa hata Benki Kuu inaweza kuibadilisha siku moja tu.

Tatizo ni uzalishaji, tatizo ni mkakati.
 
Lakini thamani ya pesa pia ni kigezo mojawapo katikà kupima Uchumi wa nchi.
China wanafanya makusudi pesa yao iwe na thamani ndogo ili wachochee exports.

Thamani ya pesa haipimi uchumi wa nchi.

Benki Kuu inaweza kusema Shilingi moja ya Tanzania ni sawa na dola moja ya Marekani.

Je, hilo litafanya uchumi wa Tanzania uwe sawa na uchumi wa Marekani?

Thamani ya pesa si kipimo cha uchumi wa nchi.

Ingekuwa hivyo, Chinese Yuan (US $0.14) na Japanese Yen (US $ 0.0064) ingezifanya China na Japan ziwe na chumi mbaya sana.

Wewe unaelewa kwamba shilingi ya Kenya ina thamani kuliko pesa ya Japan, Yen?

Japanese Yen moja ni sawa na senti 85 za Kenya.

Shilingi moja ya Kenya ni sawa na Japanese Yen 1.18

Je, hilo linamaanisha Kenya ina uchumi mzuri kuliko Japan?
 
Mkapa alikuwa anauza nchi na kupata madolari ndiyo maana dola haikupanda sana. Yaani aliowauzia viwanda, benki na mali zingine za serikali walileta dola nchini na kufanya ipatikane na hivyo isipande thamani.
 
Imports vs exports japo pia Kuna ishu ya kutumia zaidi hela ya kigeni kwenye malipo ndani ya Nchi badala ya Fedha yenu.
 
China kuendelea kung'ang'ania pesa yake iwe na thamani ndogo Kama inavyofanya hivi sasa ni kwa sababu inataka kuendelea kukwepa Vikwazo vya Kibiashara vya Kimataifa vilivyowekwa na Mikataba ya UN chini ya Taasisi ya Kibiashara ya Umoja wa Mataifa (WTO). Soma hizo Sheria/Mikataba ya UN iliyoanzisha WTO ndio utaelewa sababu za kwa nini China haitaki pesa yake iwe na thamani kubwa, sambamba na nchi hiyo ya China kukataa kuitwa kuwa ni "Developed Country," badala yake inataka kuendelea kubaki kuitwa kwa jina la "Developing Country" wakati ina uchumi mkubwa sana duniani pia Ina maendeleo makubwa.
 
Na kwa kuongezea tu, wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikivunjika mwaka 1977, pound moja ya Kiingereza ilikuwa sawa na shilingi ishirini za Tanzania.

Shilingi yetu ilianza kushuka thamani baada ya vita mwaka 1979 na Rais Ali Hasan Mwinyi alipoingia madarakani mwaka 1985 ikaendelea kushuka kwa spidi ya kutisha.

Kwa kipindi cha miaka mitano kufikia mwaka 1990 tayari hela yetu ilikuwa inabadilishwa kwa kiwango cha dola moja ya Marekani kwa shilingi mia moja na ushee.

Kilichofuatia ni kwamba hata hela ya jirani yetu Kenya iliyokuwa na thamani sawa na hela yetu ghafla bin vuu nayo ikawa haikamatiki...and the rest is history!
 
Jimbo ni kwamba ikiacha hela iwe na thamani kubwa itaumiza exports zake zitakuwa expensive so ikiwa na thamani ndogo inakuwa less expensive
 
Watu wasomi kama wakina Mwigulu sijui kwa nini hawaoni mambo kama haya? Anafanya kazi kama mhasibu kuliko kama mchumi!! Hata kitendo cha kuimarika tu kwa Sh ya Kenya hivi majuzi kilitakiwa kifanye tuwanyang'anye watalii na manufacturing jobs, cha ajabu kimetuongezea gharama za bidhaa tunazoagiza huko!
 
Hapa tunaona kuwa.

1. Pesa inaweza kufanywa iwe na thamani ya chini kimkakati kwa njia ambayo haina uhusiano na uzuri wa uchumi wa nchi.

2. Thamani ya pesa si kipimo kizuri cha uchumi wa nchi.

Nimetoa mfano wa Japan na Kenya. Shilingi moja ya Kenya ni sawa na Yen za Japan 1.18.

Yen moja ya Japan ni sawa na senti 85, yani shilingi 0.85 za Kenya.

Sasa hapo utasema Kenya ina uchumi mzuri zaidi ya Japan kwa sababu pesa ya Kenya ina thamani kuliko ya Japan?
 
Watanzania wengi wanataka majibu rahisi kwa maswali magumu, kufanya uchambuzi wa kina ulio na habari nyingi zinazokinzana ni tatizo.

Ndiyo maana hata hapa unaona watu wengi wanalalamika kuwa shilingi ya Tanzania kuwa na thamani ndogo ni jambo baya.

Wakati, kiukweli, kama unapanga mikakati mizuri ya kiuchumi, shilingi ya Tanzania kuwa na thamani ndogo kuliko kwa mfano shilingi ya Kenya, au dola ya US, inaweza kuifanya Tanzania iwe na advantage katika biashara na uchumi.

Watu hawaelewi uchumi mzuri unaweza kuwepo kwa kutumia pesa yenye thamani kubwa, na vilevile uchumi mzuri unaweza kuwepo kwa kutumia pesa yenye thamani ndogo.

Thamani ya pesa si hoja. Si tatizo. Unaweza kuwa na uchumi mzuri kwa thamani yoyote ya pesa.

Hoja ni, tatizo ni, una mkakati gani wa kuitumia hiyo thamani ya pesa yako, ikiwa kubwa au ndogo, ili upate uchumi mzuri?

China wamejua kuwa wakiwa na pesa yenye thamani kubwa, hilo litafanya exports zao zishuke. Ndiyo maana mpaka leo China wanaifanya pesa yao iwe na thamani ya chini, kwa makusudi. Ikitaka kupanda wanaishusha kwa makusudi.

Kwa sababu wanajua faida ya kuwa na exports nyingi ni kubwa kuliko hasara ya kuwa na pesa isiyo na thamani. Wamejua wenyewe ku balance mahesabu yao.

Tatizo letu si kwamba shilingi yetu haina thamani, tatizo letu ni, hatuna mkakati wa kuwa na uchumi mzuri kwa kutumia pesa isiyo na thamani (mfano uchumi wa kufanya exporrts sana kama China unaweza kufaidika na pesa isiyo na thamani sana, kwa kutegemea volume ya exports ambayo itakuwa promoted na pesa isiyo na thamani kubwa).

Watu wengi hawaelewi hili
 
Fungua kiwanda Cha midoli,makasha ya sabuni,tooth pick nk.. unasubiri nani afungue!?
 
Na mpaka Leo wahuni wa zamani 20 tunaita pauni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…