Nini kimeifanya Rwanda ipunguze kupitishia mizigo Tanzania na kugeukia Kenya?

Nini kimeifanya Rwanda ipunguze kupitishia mizigo Tanzania na kugeukia Kenya?

Ulic
Issue ni Tanzania imeongeza Kodi kwenye bidhaa za maziwa kutoka Rwanda hiyo ndio sababu kubwa tafuta Habari acha kupiga siasa.
Unadhani ongezeko la kodi kwenye maziwa ndio sababu pekee ya Rwanda kuipunguzia Central Corridor umuhimu?
 
Watu wasichokielewa ni ufanisi katika bandari ya.mombasa ni.wa.muda mrefu. Wazambia wengi magari yao.yanashukia mombasa sababu.ya straight.forward and affordable rates.

Hakuna kusimaishwa matochi sijui vari ikishakuwa cleared bandarini inatembea tuu hakina porojo njiani za kusimamishana mara.onesha hichi mara kile. Business should mean business
 
Tamko la mkuu wa majeshi ni story za vijiweni?!

Yes. Nilisema CDF karopoka kipindi kile na hadi leo nasimamia msimamo wangu. Matter of fact, I've been proven to be right maana toka CDF katoa ile kauli hadi leo nani kaachishwa kazi au kuwajibishwa? Taja wawili tu ambao wametolewa kwa tuhuma za kutokuwa raia?

Wakati CDF anatoa ile kauli maza alipuuza ile kauli pale pale kwa body language yake tu. Haya madai yanaendelea kuwa story za vijiweni until proven otherwise.
 
Hivi ukiwa ccm lazima uwe mpumbafu kiasi hiki,mizigo ya bandari inapungua wewe unasema hatuna hofu,atoke rwanda,atoke zambia,atokea malawi atoke congo uonre hali itakavyokuwa mbaya,hivi hujui ni mapato kiasi gani yanapatikana bandarini kwa sababu ya upitishaji wa bidhaa kwenda au kutoka kwenye hizo nchi.

Punguani wa head wewe.

Wekeni mipango imara,ondoeni urasimu boresheni barabara.
Punguani waheed ni wewe unayesikiliza stori za mitaani, Bandari imeongoza kwenye gawio lililokwenda hazina mwaka huu wa 2024 unasema eti mizigo inapungua!, ufanisi wa kuifanya isikae sana bandarini ndio umeongezeka.
 
Yaani tuko bize kujadili uingizwaji wa goods ambazo hatujui zimetengenezwa wapi! BADALA ya kuhoji uhalali wa WanyaRwanda waliopenyezwa kwenye idara nyeti za nchi hii
Kama raia tu anajua kuna wanyarwanda kwenye taasisi zetu nyeti, idara ya usalama wa taifa wao wanasemaje kuhusu hili?
 
Watu wasichokielewa ni ufanisi katika bandari ya.mombasa ni.wa.muda mrefu. Wazambia wengi magari yao.yanashukia mombasa sababu.ya straight.forward and affordable rates.

Hakuna kusimaishwa matochi sijui vari ikishakuwa cleared bandarini inatembea tuu hakina porojo njiani za kusimamishana mara.onesha hichi mara kile. Business should mean business
Mazingira ya rushwa
 
Mazingira ya rushwa
Ukiiangalia Tanzania yetu kwa jicho la kizalendo kabisa, utagundua kwamba sisi (siyo wote) kwenye utendaji wetu wa majukumu ya kikazi ni wababaishaji sana. Mfano ni hapa idara za maji, mabomba mengi yanayokatisha mito kipindi hiki cha mvua yamesombwa na maji sababu unakuta bomba hazijawekewa nguzo imara za zege kuhimili nguvu ya maji. Ni aidha yamepitishwa tu juu au yamesimishwa na vinguzo vya bomba za kuchomelea! Ukienda ofisini kila mtu ni mhandisi!
 
Hata maji nayo yamekuwa.ya shida sana.na.nobody is.responsible anyway
 
Unaweza kutoa gawio kwa lengo fiche na kujipendekeza kwa mamlaka kuu lakini ukweli uko bayana. Bandarini hakuna usomi uadirifu wala weredi. Bandarini ni kufanya kazi kwa mazoea na kurithishana uzoefu kutoka kwa makuli wazoefu.
Punguani waheed ni wewe unayesikiliza stori za mitaani, Bandari imeongoza kwenye gawio lililokwenda hazina mwaka huu wa 2024 unasema eti mizigo inapungua!, ufanisi wa kuifanya isikae sana bandarini ndio umeongezeka.
 
Unaweza kutoa gawio kwa lengo fiche na kujipendekeza kwa mamlaka kuu lakini ukweli uko bayana. Bandarini hakuna usomi uadirifu wala weredi. Bandarini ni kufanya kazi kwa mazoea na kurithishana uzoefu kutoka kwa makuli wazoefu.
Maoni yako ni yale ya vijiweni kwenye mabenchi ya wauza kahawa.
 
Yes. Nilisema CDF karopoka kipindi kile na hadi leo nasimamia msimamo wangu. Matter of fact, I've been proven to be right maana toka CDF katoa ile kauli hadi leo nani kaachishwa kazi au kuwajibishwa? Taja wawili tu ambao wametolewa kwa tuhuma za kutokuwa raia?

Wakati CDF anatoa ile kauli maza alipuuza ile kauli pale pale kwa body language yake tu. Haya madai yanaendelea kuwa story za vijiweni until proven otherwise.
Ni kazi ya CDF kufukuza hao watumishi wa umma? Huyo mama kutochukua hatua ni ishara alichosema CDF ni uongo? Kwani CDF alichosema ni maoni yake binafsi, au ni tamko la taasisi?
 
Maoni yako ni yale ya vijiweni kwenye mabenchi ya wauza kahawa.
Mkuu nafahamu ninachokiongea, hizo bandari zote nazijua utendaji wake tangu enzi za East African Harbours Cooperation. Halafu gundua tu kuwa kijiweni kuna taarifa za ukweli zisizo rasmi.... Hiyo ndio tofauti!.
 
Wewe wakati unataka tujadili wanyarwanda waliopo serikali ulitegemea sisi ndo tunachukua hatua? Una akili ndogo kama funza.
Bora hata funza. Heri yako wewe mwenye nyingi
 
Uelewa wako mdogo dogo sana kama ubongo wa kuku.

Dubai, Singapore hazizalishi vitu vingi tu ila ni transportation hubs.
Dubai na Singapore hakuna machawa na wasakatonge wasio na uelewa kama wewe na wale wenzako!
 
Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.

Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.

Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.

Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.

Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.

Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.

Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.

Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.

Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .

Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.

Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.

Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.
Rwanda imepunguza matumizi ya bandari ya Dar es Salaam kwa baadhi ya mizigo na kuelekeza sehemu kubwa kupitia bandari ya Mombasa, Kenya, kwa sababu za kiufanisi na kimkakati.

1. Ufanisi wa Bandari ya Mombasa

Bandari ya Mombasa inahusishwa na muda mfupi wa kushughulikia mizigo ikilinganishwa na Dar es Salaam. Wakati wastani wa kushusha mizigo ni siku 1.25 huko Mombasa, Dar es Salaam inachukua siku 5 kwa wastani.

Ufanisi huu wa Mombasa umesaidia kupunguza gharama za usafirishaji na muda wa kusafirisha mizigo kuelekea Rwanda.

2. Mfumo wa Kufuatilia Mizigo (ECTS)

Kenya, Uganda, na Rwanda zinatumia mfumo wa pamoja wa kufuatilia mizigo wa kielektroniki (Electronic Cargo Tracking System - ECTS), unaosaidia ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati halisi na kupunguza ucheleweshaji.

Tanzania bado inatumia mfumo wa kitaifa usiofanana na ule wa EAC, hali ambayo inaleta changamoto za ucheleweshaji mpakani na gharama za ziada kama ada ya kifaa cha kufuatilia.

3. Gharama za Usafiri

Gharama ya kusafirisha mizigo kupitia Dar es Salaam inasemekana kuwa kubwa kutokana na changamoto za miundombinu, kama reli inayosafirisha asilimia ndogo ya mizigo.

Mombasa imekuwa ikipunguza ada za bandari na kuongeza vivutio kwa wateja, jambo ambalo limeifanya ipendelewe zaidi na wafanyabiashara wa Rwanda.

4. Mikakati ya Kenya Kuvutia Wateja

Serikali ya Kenya imeimarisha miundombinu kama reli ya SGR na huduma za mwisho wa safari za mizigo, hatua iliyovutia Rwanda.

Vilevile, Kenya imeboresha muda wa kuhifadhi mizigo kwenye bandari bila malipo na kupunguza ada za ziada, ikilinganishwa na Tanzania.

5. Upanuzi wa Miundombinu ya Usafirishaji

Bandari ya Mombasa imeongeza uwezo wake wa kushughulikia mizigo kupitia miradi ya kupanua maberthi na kuongeza vifaa vya kisasa.

Hili limeongeza uwezo wa kushughulikia meli kubwa zaidi na kupunguza msongamano, ikilinganishwa na Dar es Salaam ambayo bado inaboresha uwezo wake kwa kupanua baadhi ya maberthi na miradi mingine.

Kwa ujumla, Rwanda inatafuta njia ya kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo yake.

Hii ndio sababu kuu ya mabadiliko haya, lakini Tanzania inaendelea kuboresha miundombinu yake ili kuimarisha ushindani wake katika kanda.

Ova
 
Back
Top Bottom