Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.
Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.
Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.
Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.
Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.
Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.
Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.
Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.
Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .
Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.
Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.
Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.
Rwanda imepunguza matumizi ya bandari ya Dar es Salaam kwa baadhi ya mizigo na kuelekeza sehemu kubwa kupitia bandari ya Mombasa, Kenya, kwa sababu za kiufanisi na kimkakati.
1. Ufanisi wa Bandari ya Mombasa
Bandari ya Mombasa inahusishwa na muda mfupi wa kushughulikia mizigo ikilinganishwa na Dar es Salaam. Wakati wastani wa kushusha mizigo ni siku 1.25 huko Mombasa, Dar es Salaam inachukua siku 5 kwa wastani.
Ufanisi huu wa Mombasa umesaidia kupunguza gharama za usafirishaji na muda wa kusafirisha mizigo kuelekea Rwanda.
2. Mfumo wa Kufuatilia Mizigo (ECTS)
Kenya, Uganda, na Rwanda zinatumia mfumo wa pamoja wa kufuatilia mizigo wa kielektroniki (Electronic Cargo Tracking System - ECTS), unaosaidia ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati halisi na kupunguza ucheleweshaji.
Tanzania bado inatumia mfumo wa kitaifa usiofanana na ule wa EAC, hali ambayo inaleta changamoto za ucheleweshaji mpakani na gharama za ziada kama ada ya kifaa cha kufuatilia.
3. Gharama za Usafiri
Gharama ya kusafirisha mizigo kupitia Dar es Salaam inasemekana kuwa kubwa kutokana na changamoto za miundombinu, kama reli inayosafirisha asilimia ndogo ya mizigo.
Mombasa imekuwa ikipunguza ada za bandari na kuongeza vivutio kwa wateja, jambo ambalo limeifanya ipendelewe zaidi na wafanyabiashara wa Rwanda.
4. Mikakati ya Kenya Kuvutia Wateja
Serikali ya Kenya imeimarisha miundombinu kama reli ya SGR na huduma za mwisho wa safari za mizigo, hatua iliyovutia Rwanda.
Vilevile, Kenya imeboresha muda wa kuhifadhi mizigo kwenye bandari bila malipo na kupunguza ada za ziada, ikilinganishwa na Tanzania.
5. Upanuzi wa Miundombinu ya Usafirishaji
Bandari ya Mombasa imeongeza uwezo wake wa kushughulikia mizigo kupitia miradi ya kupanua maberthi na kuongeza vifaa vya kisasa.
Hili limeongeza uwezo wa kushughulikia meli kubwa zaidi na kupunguza msongamano, ikilinganishwa na Dar es Salaam ambayo bado inaboresha uwezo wake kwa kupanua baadhi ya maberthi na miradi mingine.
Kwa ujumla, Rwanda inatafuta njia ya kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo yake.
Hii ndio sababu kuu ya mabadiliko haya, lakini Tanzania inaendelea kuboresha miundombinu yake ili kuimarisha ushindani wake katika kanda.
Ova