Ameonyesha uwezo mzuri kwenye Wizara aliyopewa mara ya kwanza kabisa kuiongoza na ndio maana wizara hii mpya ya Sanaa, utamaduni na Michezo nayo ni mpya hivyo yawezekana Rais ana maana yake .
Angeweza kumpa kokote Ila amempeleka kama Waziri kamili anajua pale hakuna kelele sana apumzike ale kimya.
Hata ingekuwa mimi ningefurahi kupelekwa kwenye michezo kwanza panakuweka karibu na wananchi kupitia michezo yaani unakutana na watu wakiwa kwenye raha tupu ni fulu kuwapa shangwe unajipatia umaarufu bila jasho.
Huko kwenye mambo magumu utakutana na majungu kila siku. Hapo anakula kimyakimya na mshahara ni wa Waziri hauna presha.
Hata madili yapo Kuna ujenzi wa viwanja vya watoto, Makumbusho nk hizo ni deal hazina presha hakuna atakayelalamika kuhusu tozo.