LGE2024 Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ule ushenzi aliofanya Magufuli 2019/2920 ndiyo umewavunja moyo watu wanaona kumbe sanduku la kura siyo linalotoa mshindi bali matakwa ya mtawala.
 
Tatizo ni maji ya mgao Yani mtu aache kukinga maji na anajua mda wowote yanakatika akahangaike kujiandikisha🤣Kwani wanagawa na Alkasusu
 
Kuna vituo mawakala wa ccm wameshaandaa majina feki ya wapiga kura. Sasa kujiandikisha kuna maana gani? Hayo majina feki yakapige kura tu.
 
Hawataki kutegemea matokei kwenye jambo wanalo lijua, wanalolijua ni kwamba CCM wataenda maporini kuchimba dawa bila kutumwa na serikali, (chama dola)
 
Waache umayaimayai. Wakajiandikishe na wahakikishe hakuna ujanja ujanja. Hiyo ndiyo njia pekee. Vinginevyo watawekewa viongozi wa hovyo.

Nikuwa na msimamo tu awe ccm, cdm sijui act mhm kumpata kiongozi anayekubalika.
 
I will never ever waste my time

Kama wanataka watu walundikane waweka tume huru ya uchaguzi
 

Dhalimu magufuli ndio alikuja kufunga ukurasa wa kuendelea kushiriki chaguzi zinazoamuliwa na ccm. Hakuna kuendelea kushiriki chaguzi ambazo matokeo yanapangwa na viongozi majizi ya ccm. Ni aidha machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ili kurejesha heshima ya box la kura.

Na hakuna kujitokeza kwenye mikutano ya viongozi watakaochaguliwa kwenye chaguzi hizi za kipuuzi. Akija kiongozi akitaka nyomi amwage hela ya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…