Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?


Hizo tools tatu tulizoongea hapo juu ndio chanzo cha yote hayo kutotokea Africa..

Elimu iko limited na bepari ili isimkomboe Mwafrica maana wao pia wanafahamu elimu inaweza kuwa prime mover na push ya vitu vingi.

Technolojia, ukilimit elimu na technolojia pia haiwezi kukua, hata wale wenye vipaji nje ya elimu wako limited na mifumo ambayo iko controlled na mabepari wa dunia..

Utamaduni, kupitia media ambazo wao ndio controller wanahakikisha tamaduni hazikui zaidi ya zao za magharibi kukua na kutumeza huku...hili ni sambamba na entartaiment kuhakikisha wote tunacopy kwao kwa wao kubland vya kwao na kupuuza vyetu.. Lugha kuu ya dunia kiingereza na wote lazima tusome tuongee kienglish na elimu zote lazima zitumie hiyo lugha....na mkakati ni kutokomeza hata hizi lugha za makabila kwa watu kuoana huku na kule na automatically kuziua lugha na kubaki na kiswahili ambacho kitamezwa na kienglish..
 
Unajua biashara ya utumwa iliendelea kwa miongo mingi, watu waliingiwa na woga hata wa kufanya shughuli za uzalishaji kwa hofu ya kukamatwa utumwani. Matokeo yake jamii zilianza kuwa na uhaba wa chakula.
Haya tuseme tatizo ni utumwa, vipi sasa miaka 60 baada ya uhuru?
 
Haya tuseme tatizo ni utumwa, vipi sasa miaka 60 baada ya uhuru?
Hatujakubali kuyafanyia tathimini makosa na kujifunza jinsi ya kuyarekebisha. Kwakifupi nchi yetu sasa ina focus kwenye ushindi wa uchaguzi tu na kujipanga jinsi ya kushinda uchaguzi ujao.
 
Kuhusu lugha hili waliliona siku nyingi na ndiyo maana Ulaya watoto wote ni lazima wajifunze Kijerumani, Kispaniola, Kifaransa na Kiingereza.

Tukubali mapema kuwandisha watoto wetu Kiingereza mapema wakielewe kama wanavyoelewa Kiswahili. Nyerere alisema Kiingereza ndiyo Kiswahili cha duniani.

Entertainment industry duniani kote wanajua Waafrika hawana mpinzani. Hollywood waliwabania sana mpaka hawakuwaalika kwenye Emmy Awards lakini wenyewe waliunda BET awards.

Nigeria wametambua hilo na wameinject pesa nyingi Nollywood. Uzuri wa Nollywood lugha inawabeba. Cinema zao zinaonyeshwa Sky na Al-Jazeera. Ni muda na sisi kupanga mikakati ya kufika huko. Bongo movie wawe na graduates wa movie production kutoka vyuo vinavyotambulika. Hapa tunarudi kwenye Elimu.
 
Miaka ya 90 vilikuwepo viwanda vya azam? Zaidi ya serikali nani alikuwa ananunua ngano?
Wewe kwenu wapi Dar.

Unaijuwa Unga Limited Arusha, au unaisikia tu? Unafikiri ilikuwa inanunua inasaga unga wa bwimbwi?Dar pale gerezani kuna wahindi hakuna zao ambalo walikuwa hawanunui na kulisaga. Uko wapi wewe? Ushaona unga wa ngano wa serikali? Hiyo 90 unayoongea wewe hata NMC ya serikali ilikuwa imeshakufa.

Msitake kudanganya watu kijinga, hii ni JF mkadanganyane jobless corner zenu huko.
 
Ngano zamani sana ilikuwa inanunuliwa sehemu mbili, Unga Limited Arusha na serikalii NMC pale oppossite na TAZARA ambapo kwa sasa ni Bakhresa. Hizo zilikufa hata Nyerere hajang'atuka.
 
Umeongea kwa uchungu sana..ila huu ndio ukweli..huoni south ilivyoendelea.

#MaendeleoHayanaChama
 
elimu,teknolojia ongeza na utamaduni....hivi vyote kwa sasa ndio tools kubwa inayotumika kumfanya Mwafrica kuwa mtumwa bado...

Huu mtego mpaka sasa hakuna dalili za kuukwepa..
Umesahau dini...ndio nyenzo iliyo mmaliza mwafrika kiakili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni kweli kabisa mkuu hii mada ingepelekwa pia kule Twitter ili Mhe Husein Bashe aione yuko very positive and open minded Kwenye issues kama hizi...
 
Huo ni mfano wa viongozi wanavyoandaliwa,mashamba ya Hanang yaliharibiwa/yalifilisiwa na viongozi wanaosimamia
Hawezi kukuelewa maana akili yake it seems
imetawaliwa na u CCM Vs u CDM badala ya maslahi mapana ya taifa.
 
The best post tokea kuanza kwa mwaka huu hapa JF hongera sana mkuu [emoji106][emoji106][emoji1666][emoji1666]
 
Huyu atakuwa anazungumzia enzi za National milling, ambayo ilikuwa ya serikali...
 
Kwani nchi kama Malaysia hazikutawaliwa?
 
Hii tabia ya kuendekeza wanyonge ni utoto,kila mtu amesoma the so called agrarian revolution ilivyoleta mapinduzi..

Mpango wa kilimo kwanza ulikuwa unaenda kuanzisha mashamba makubwa ya mabepari au ushirika wa kibepari Ili kuleta tija kwenye kilimo..

Unfortunately kila kitu kimekufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…