Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Mimi naombea waanze hiyo mikutano.
 
Mkuu watanzania nima-snitch yaani mtu anavunja kitu muhimu kwa ustawi wa taifa alafu Kuna kundi la mazwazwa linaona ni sawa
 
Kumbe na wewe unajuwaga kuandika hivi!??? 🙂 Huwa nadhani unachofahamu tu ni kulaiki 🙂
 
Kama katiba ya sasa inavunjwa ni vipi hiyo mpya itaheshimiwa?

Nadhani ungeanza usimamizi thabiti wa katiba ya sasa kabla ya kudai mpya.

Aidha CHADEMA wanadai katiba mpya ili iwasaidie kushika dola ila sio kumsaidia mwananchi wa kawaida katika shughuli zake za kila siku.
 
Hivi unajua hio haki mnayotaka kuidai kwa ubabe itaambatana na mkong’oto wa FFU?

Hakuna asiyetaka kudai haki ya katiba ila je umejiandaaje na kichapo hicho maana lazma utata utakuwa mkubwa! Kama ulikuwepo zama za Mwembechai 1996 basi kile kilichotokea ndio hasa kitatokea maeneo mengi ya nchi katika kizazi hiki mayai mayai nani yupo tayari kwa ule uharibifu?

Nikiangalia hio katiba haininufaishi moja kwa moja bado! Nimesema ntapambania katiba kama kuna kipengele cha mwananchi kupewa gawio lisilopungua 5M kila mwaka wa serikali unapoanza ili kupunguza makali ya maisha! Siwezi kupambania ndoto za wanasiasa wao wakabunye zao Burj Khalifa kila December wakati mie naganga njaa!
 
Na wakati ni katiba hiyo hiyo ndo iliyo mpa madaraka akisha pata oath basi katiba ni takataka kwake ila mawazo yake ndo yafuate utadhani Mungu ndo kamuweka
Hahahahah raisi akifata kila mnachotaka nchi itatawalikaje? Halafu mnataka katiba ambayo nyie mnachofikiri ndio raisi afanye huyo atakuwa raisi au mdoli!? 😅 Mfano mwepesi tu wewe ndio baba mjengoni kwako ila mtoto wako wa darasa la 4 ndio akupangie utaratibu wa kuendesha nyumba we uliskia wapi? Eti baba usioe nimesema hatutaki mama wa kambo humu 😂😂😂 na we mzee unakubali unaanza kupiga nyeto! We uliskia wapi hilo???

Acheni kuota hata huyo Mbowe akipewa nchi pamoja na katiba mpya hamna kitu atafanya ambacho kitampa ugumu kuwatawala! Mkileta ujinga atatumia polisi na majeshi kama kawa!!!
 
Wakati was msukuma mwenzio JPM ulikuwa unasifu na kuabudu
 
Leo naona umewaamkia; umewachomolea koki kabisa!!! Hatari na nusu!!! Bi Mkubwa anaweza kukupatia cheo hata leo au kesho, ngoja tungojee siye 🙂 🙂 🙂
 
Kunapokuwa na mushkeri kwenye mfumo wa maisha hasa uminywaji wa fursa na haki ndipo vuguvugu hujitokeza.
Mifano ni mingi, wanawake wanadai 50/50, walemavu wana madai yao, wapinzani nk. Nk.
Ni nani hasa anayedaiwa? Je, wanaona hayo mapungufu? Ni kwa nini wanagugumia kama wanayaona.
Ni hivi, mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
Watawala duniani wamejitwalia haki zote hawana cha kudai zaidi ya utii na heshima na warudishe hisani ikiwapendeza.
Eti raia wanakiri, neno la mfalme ni amri wakati la raia ni ombi.
Kwa jinsi hii dunia itachelewa sana kuendelea. NENO LA MFALME LIWE OMBI NA NENO LA RAIA LIWE AMRI hapo watawala watageukia haki na nchi itaendelea.
Iweje kilicho haki kitafutwe kwa maombi ilhali kisicho haki chatendwa kwa amri?
 
Wewe ni Mpuuzi unayedhani Katiba ni Takwa la CHADEMA
 
Watu kama Zitto na Mbowe ni wajanja wajanja sana. Wanaijua mamlaka ya Rais wa Tanzania vizuri.

Ndio maana sometimes Zitto huwa anapata mihemko anaandisha harsh sana mtandaoni, halafu baada ya dakika 2 unakuta kafuta.

Ukishampa mtu madaraka hata akiwa chizi, ndio imetoka hiyo. Lazima utumie busara sana.

Ni sawa na mtu kwenye nchi yenye madereva wasiotii sheria za barabarani kutembea kwa madoido katikati ya zebra ukijua una haki zote.

Ukigongwa ukafa au ukavunjwa miguu, hata wakileta traffic police 3,000 wakapima na kuonesha umeonewa na dereva ndio mkosaji, wewe miguu yako au uhai hauwezi kurudi.

Zitabaki stori tu.
 
Yeah nobody care ushaumizwa kesi inamalizwa chap chap inabaki story!
 
Umerudishiwa akili zako mkuu!!
 
Katiba na Sheria!
Suala hili liliishafikia hatua ya kupiga kura kwa mujibu wa sheria? je tupige kura ?au tuanze upya na rasimu ya Warioba tuiache rasimu ya Sita? Na je tuliisha kubaliana nini kuhusu Muundo wa serikali mbili au tatu? Kama taifa kwa vile viongozi wa siasa hapo ndipo kwenye mvutano mkubwa. Hatutapoteza fedha za wananchi kwa kuanzisha mchakato usio na tija. Tuwe wazi kama sheria zinatuongoza turejee maswali haya muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…