Nini kinachotuongoza? Sheria na Katiba au hila na fadhila za Rais?

Watu wanahangaikia mipango ya hela nyie mnalazimishia Agenda ya kisiasa iwe ishu ya wananchi!
Utapataje hela katika nchi ambayo haiongozwi kwa mujibu wa sheria na katiba?Unaelewa kuwa wakati wa magufuli watu wa bureau de change walipewa clearance na BOT ila magufuli akaenda kuwafilisi kinyume na sheria?

Unaelewa kuwa mahakama ilizuia watu wa kimara wasibolewe nyumba zao ikiwa ni pamoja na waliokuwa na biashara zao ila magufuli akaenda kubomoa nyumba zao kinyume na sheria?Unaelewa kuwa Magufuli alikuwa anatumia vibaka(the so called task force) kukusanya kodi badala ya TRA kitu ambacho kilikuwa ni kinyume na sheria?

Katika mazingira kama hayo utafanya mipango gani ya hela?Haya mambo mbona ni madogo sana kuelewa?Unakwama wapi?Unahitaji kuwa profesa ili kuelewa mambo simple namna hii?Yaani unahitaji kuwa profesa ili kujua kuwa bila utawala wa sheria mipango ya hela ni haipo?!
 
Nimekuelewa vizuri Sana mkuu Kama kitu ni kwa maslahi makubwa ya taifa basi viongozi hawana haja ya kushupanza shingo maana wapo katika nafasi zao kwa maslahi ya taifa ila Kama wapo kwa maslahi ya matumbo yao basi kutakuwa na gharama ya harakati hizi.
 
Hamna ambaye yuko madarakani bila kuhusisha tumbo ukimuondoa Nyerere aliekuwa muasisi wa hiki chama tawala! Hakunaaa!!!
 
Hamna ambaye yuko madarakani bila kuhusisha tumbo ukimuondoa Nyerere aliekuwa muasisi wa hiki chama tawala! Hakunaaa!!!
Kama taifa bado tuna Safari ndefu Sana naungana na kauli ya mwandishi wa Ghana wa kitabu" the beautyful one are not yet born"
 
Katiba Ni mfumo wa uongozi katika jamii. Katiba huamua kila kitu. Mfano upate kiasi gani katika mahangaiko yako hayo nk. Katiba hii ya Sasa Ni mbovu kupita maelezo hata malaika hawezi kuisimamia. Mwl. Nyerere angalau alisema Ni ya kidikteta.
 
Hapo ndio ujue Chadema mko peke yenu.

Laiti kama kweli wananchi wangekuwa wanaihitaji katiba mpya iwe mvua, liwe jua ingekuwa imeshapatikana.
Nakubaliana na wewe Chadema wamebaki peke yao maana wengine wote wamekubali yaaishe kwa kutiishwa na watawala.
 
Pure CCM propoganda. I now know you at work.
 
Tartiib mkuu. Kinachodaiwa ni mchakato wa kuunda katiba mpya. Si uamuzi/matakwa ya Mbowe au mtu yoyote. Ni katiba itakayozingatia maslahi ya kila Mtanzania ambayo kwa katiba ya sasa ama yamekaa tenge au hayagisiwi kabisa.

Si katiba ya kumuingiza Mbowe madarakani. Kura za wananchi ndio zitakazoamua. Wadau wote watashirikishwa na rasimu itakayokubaliwa itapigiwa kura na wananchi.

Lengo ni kuepusha mtu mmoja kuwa na uamuzi hata juu ya uhai au mauti wa kila mwananchi.

Tuko kwenye hatua ya kuamua mchakato wa katiba mpya; uwepo au usiwepo? Rais anasema hayuko tayari wakati huu hadi baadaye - haijulikani lini. Wewe unasemaje?
 
Leo naona umewaamkia; umewachomolea koki kabisa!!! Hatari na nusu!!! Bi Mkubwa anaweza kukupatia cheo hata leo au kesho, ngoja tungojee siye πŸ™‚ πŸ™‚ πŸ™‚
Hizi ndio akili za Vijana wa kitanzania hasa wa ccm. Ni kujipendekeza tu kwa rais ili mpate vyeo.
 
Chadema wanashirikiana na kundi gani kudai katiba mpya mpaka sasa ?
Hujasikia juzi Mbowe amesema anawakaribisha wadau wote ikiwemo taasisi za dini ili washirikiane kudai katiba mpya. Na pia alisisitiza katiba bora ni kwa faida ya wananchi na si Chadema kama wengi mnavyopotosha huku
 
STK ndio inatuongoza.

Sheria (Katiba)
Taratibu (Utashi)
Kanuni.
 
Hapo ndio ujue Chadema mko peke yenu.

Laiti kama kweli wananchi wangekuwa wanaihitaji katiba mpya iwe mvua, liwe jua ingekuwa imeshapatikana.
WanawezA kuwa peke yao Sawa ila wanatumika kama wake up call kuwaamsha Watanzania. Mdogo mdogo tu kitaeleweka.
 
WanawezA kuwa peke yao Sawa ila wanatumika kama wake up call kuwaamsha Watanzania. Mdogo mdogo tu kitaeleweka.
Basi kama watanzania bado wamelala, kuwaamsha lilitakiwa kuwa jukumu lao la kwanza.
 
Hujasikia juzi Mbowe amesema anawakaribisha wadau wote ikiwemo taasisi za dini ili washirikiane kudai katiba mpya. Na pia alisisitiza katiba bora ni kwa faida ya wananchi na si Chadema kama wengi mnavyopotosha huku
Too late.

Unaanzisha vuguvugu lako mwenyewe kivyako halafu ndio unaalika makundi ya kushirikiana nayo ?
 
Basi kama watanzania bado wamelala, kuwaamsha lilitakiwa kuwa jukumu lao la kwanza.
Exactly ndio wanachokifanya sasa, kupitia makongamano, midahalo kwenye vyombo vya habari na pia hata mikutano ya kisiasa.
 
Exactly ndio wanachokifanya sasa, kupitia makongamano, midahalo kwenye vyombo vya habari na pia hata mikutano ya kisiasa.
Kuna makongamano yoyote kuhusu katiba mpya wameshafanya kwa kushirikiana na wananchi ?
 
Isa 43:26 SUV
"Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako".

Mwenyezi Mungu Baba wa Mbinguni anatuambia hivyo hapo juu,sasa binadamu ni nani hata tushindwe kumkumbusha na kumuhoji!!??

Mungu Muumba anatutaka tumkumbushe na tumuhoji, iweje sisi binadamu tuogope kumkumbusha na kumuhoji binadamu mwenzetu!!???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…