Nini kinasababisha wanaume kukimbia familia zao?

Kwa hizi comment utaona jinsi gani kama jamii hakuna tena accountability
Yaani mwanaume anatekeleza familia lakini bado lawama anapewa yule mama ambaye yeye anaamua kulea watoto.
Kama jamii itaendelea kulea watoto wa kiume kwa mitazamo hii ni wazi itakuwa kawaida kwao kwani wanajua mwisho wa siku hata jamii pia ipo upande wao.
Hakuna sababu yoyote ya kutelekeza familia kwa mtu yeyote yule!
 
uko kwenye ndoa umefika mbali, kwenye talking stage tu, wanaume wengi wakiombwa elf 20 wanakimbia, na urafiki hawataki tena, hili swala hadi miss natafuta alilianzishiaga uzi realMamy
 
Siku hizi kwenye magroup ya wanawake, Wanalalamika sana wanaume kuwa achia watoto,

Na wao kutokomea kusikojilikana na kwenda kuanzisha family Nyingine huko. Je ni ugumu wa maisha,au gubu la mke,? Au ndo kuchokana?
Anakimbia familia moja na kwenda kuanzisha familia nyingine?Tafakari!
 
It’s not as simple as that mdau. Mara nyingi wanakimbizwa, kicked out like dogs! Poor men, who’s there to help them?! Lord have mercy on us men….
Vitendo hivyo vya mwanaume kutimuliwa(Kukimbizwa)aghalabu hufanywa na wale wamama waliojipata kiuwezo na hufanywa indirectly kwa wamama kufanya vituko visivyo na sababu maalum e.g. kuchelewa kurudi nyumbani, kumjibu mwanaume kijeuri, kulazimisha aina/mtindo fulani wa maisha, kuwa na marafiki wasioeleweka na kuwakaribisha nyumbani bila taarifa kwa baba mwenye nyumba, kuweka hali ya ukimya au nununu kwa baba, kumkatalia baba unyumba ikiwemo kuzusha tetesi za uongo juu ya mienendo ya baba kimahusiano huko nje eti ana michepuko kibao n.k.n.k. Hapo mwanaume hata uwe mvumilivu kiasi gani utayield au kusurrender na kujiondokea zako. Cha kufia nnini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…