Nini kinasababisha wanaume kukimbia familia zao?

Nini kinasababisha wanaume kukimbia familia zao?

Hawataki kuwapikia 🤣
Feminism inamtaka mwanaume aendelee kutoa traditional sacrifices, at the time apoteze traditional benefits zote zinazokuja na sacrifices anazotoa.

Rudini Beijing mkakubaliane feminism inatakiwa kuwa applied vipi kwenye suala la mahusiano na ndoa.
 
Siku hizi kwenye magroup ya wanawake,
Wanalalamika sana wanaume kuwa achia watoto,
Na wao kutokomea kusikojilikana na kwenda kuanzisha family Nyingine huko.
Je ni ugumu wa maisha,au gubu la mke,??
Au ndo kuchokana??
Jiulize, kwanini waanzishe familia zingibe na wamekimbia familia?
 
Hao ni wavulana sio wanaume,kuna tofauti kubwa hapo,
Pia uvulana na uanaume haupimwi kwa umri wa muhusika bali kwa responsibility and wisdom of a mature man,

Mwanaume anaye jielewa hawezi kuwatelekeza watoto wake kisa Mwanamke aliyenae,
Unaweza kumuacha Mwanamke ila sio watoto wako,wanao utawahudumia hata kama hauishi na huyo Mwanamke,

Ni kweli kuna wanawake hua wanawakera wanaume zao mpaka kuichukia familia yao But huwezi kuwatupa wanao kisa mwanamke uliyekutana nae tu ukubwani,Damu ni nzito kuliko maji,matatizo hayakimbiwi bali hutatuliwa.
 
MKE
Mwanamke anataka simu nzuri Iphone 15..........
Anataka mafuta ya mwilini kuanzia laki Moja......
Kusuka kuanzia 50k........
Kuvaa vizuri
Kula vizuri
Outing za maana.
Pesa ya matumizi.
Bado kusaidia wazazi wa mke😜

WATOTO
Watoto wavae vizuri kwa ajili maonyesho mtandaoni.
Kushindana na kina Zuchu.
Ada
Chakula kizuri.

MUME
Kodi
Mafuta ya Gari/Nauli
Gesi
Umeme
Maji
King'amuzi
Shopping ya Chakula
Vocha
Kuvaa
Pombe
Kuhonga
Kusaidia Familia yake


Kwa nini wasikimbie šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…
 
šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…
Subiri subiri kidogo šŸ˜…
Hapana aiseeee...
Mimi nakata tamaaa mapema kabisa an hapo tuu hatujafunga ndoa mtu anakwambia anacheza mchezo wa vyombo, ujakaa vizuri anasema anataka tv nchi 43 kama ya mariamu rafiki ake.

Hapo unasema ngoja nijipange anasema tanga kuna kikao cha familia sijui must aende an

Mi nachoka šŸ™ŒšŸ™ŒšŸ™ŒšŸ™ŒšŸ§
 
MKE
Mwanamke anataka simu nzuri Iphone 15..........
Anataka mafuta ya mwilini kuanzia laki Moja......
Kusuka kuanzia 50k........
Kuvaa vizuri
Kula vizuri
Outing za maana.
Pesa ya matumizi.
Bado kusaidia wazazi wa mke😜

WATOTO
Watoto wavae vizuri kwa ajili maonyesho mtandaoni.
Kushindana na kina Zuchu.
Ada
Chakula kizuri.

MUME
Kodi
Mafuta ya Gari/Nauli
Gesi
Umeme
Maji
King'amuzi
Shopping ya Chakula
Vocha
Kuvaa
Kuhonga
Kusaidia Familia yake


Kwa nini wasikimbie šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…
Sio kukimbia..
Wanaacha ndala
 
SABABU AMBAZO LABDA ZINASABABISHA WANAUME (HUSUSAN VIJANA) KUKIMBIA FAMILIA ZAO, MKE NA MTOTO/WATOTO

Hii ni mada mseto lakini kwa hapa, nitaorodhesha chache tu, bila maelezo zaidi.

SABABU ZA KIMFUMO
  1. Kufifia au kupungua kwa Mfumo Dume; mara nyingi sana Mfumo Dume umekuwa ukiongelewa vibaya, lakini ni mfumo ambao kabla ya kutengeneza upendeleo kwa Mwanamume, ulimpa majukumu; na jukumu moja wapo ni kulea watoto na familia, ilikuwa ngumu sana kwa sababu "MTOTO NI WA BABA" hivyo hakuna namna mtoto atalelewa nje ya mkono wa baba. Siku hizi hakuna mfumo wa kutuwajibisha, ila zamani ukikimbia familia utaikuta kwa baba yako, hususan watoto. Umetaka, hujataka, mana utagombana na baba wakubwa/wadogo, mashangazi na hata wazazi wako kwa sababu tu umelaza damu nje. Fikra hizo siku hizi hakuna, so imekuwa rahisi sana kwa sababu hakuna mfumo wa kutuwajibisha.

  2. SEXUALIZATION; vijana wengi siku hizi tupo sexualized, sio Wanaume, au wnawake. Jambo hili limetufanya kuwa watu tunaofanya sana ngono kama starehe, jambo ambalo linasababisha kutokuwa tayari kuwajibikia matokeo yake ambayo kimsingi ni mimba. Imekuwa mara kumi rahisi zaidi kupata ngono siku hizi ukishakuwa na hela, hata kama ni kidogo. Na mbaya zaidi wanao umia ni watoto wenye wazazi wa matabaka ya kati na chini, yaani masikini.

  3. Ongezeko la fikra za uonevu kwa Wanawake na mseto wa fikra za Ukombozi; Wanawake wengi bado wapo kwenye VICTIM MENTALITY, yaani anachoamini yeye muda wote anaonewa, hii ni hangover ya mfumo dume na stories zake, ndio mana nikasema awali hapo; jamii imeusimulia vibaya tu mfumo huu ndio maana imefika wakati Wanawake wanajiona ni wahanga muda wote hata kama kosa akifanya yeye. Hali ambayo inasababisha asiwajibikie makosa yake, na atake nafasi au heshima ya upendeleo hata kama kakosa yeye. Kuna heshima MAMA amepewa kutoka kwenye jamii, heshima hii ina muungusha, anapoteza hadhi yake kama mwanadamu na anakumbatia UUNGU, jambo linalomuweka mbali na makosa yake. Sidhani kama kuna Mwanamume anaweza kuvumilia mtu asiyetaka kuwajibikia makosa yake.
SABABU ZISIZO ZA KIMFUMO
  1. Kundi kubwa la Wanaume, leo hii lina changamoto na ujuzi na uelewa wa kuwa baba. Dunia inaimba sana kuhusu mapenzi na si familia, tuna taarifa nyingi kuhusu namna ya kuwa mpenzi wa Mwanamke wako, na si baba wa familia, YES!! namaanisha FAMILIA, sio baba wa WATOTO. Neno BABA kama lilivyo MAMA, lina maanisha malezi ya familia, sio watoto. Baba inaanzia kwenye mji na miliki, sio WATOTO. Kwa mfano, tukija kuulizia BABA MWENYE NYUMBA, usidhani tutajali kama una watoto ama LAH!! yeyote, anayeishi kwenye himaya yako, yupo chini yako na unapaswa umuwajibikie kama jukumu lako, hizi taarifa tunazo chache au hatuna kabisa kama zile za style gani ukimbinua huyo mwanamke atakojoa!!

  2. Hollywood, mitandao ya kijamii na Watu binafsi hususan Wanawake wenye uchumi mkubwa wameanza kuuza dhana ya ndoa kama UTUMWA na kuishi bila Mwanamume ni FLEX au ukombozi, naam!! shida kubwa inaanzia hapa. Mwanamke akishakuwa na dhana hii, anaanza kuvuta heshima kwake na si kwa mwenzie (selfishness) anahisi anastahili heshime yeye, hususan akishakuwa na uchumi mkubwa na si mwenzie. Hivyo basi, single motherhood inauzwa kama lifestyle. Hili ni jambo la kimkakati, ambalo hata mimi kwa fikra zangu za Kibepari zilizojaa ushetani ndani yake naziunga mkono, nadhani tunahitaji single mothers wengi zaidi ili wachache tuwe na uchumi mkubwa zaidi (Kama nitanufaika) kwa sababu kupitia MAMA ndipo tunajenga consumerism culture, na uchumi unazidi kukuwa kwa watu wachache. Akiwemo BABA, kunakuwa na order. Kutafifia.
Sababu nyingine za ziada, ni pamoja na uchumi dhaifu, na migogoro ya chuki kati ya familia, na kadhalika.
 
SABABU AMBAZO LABDA ZINASABABISHA WANAUME (HUSUSAN VIJANA) KUKIMBIA FAMILIA ZAO, MKE NA MTOTO/WATOTO

Hii ni mada .
Sababu nyingine za ziada, ni pamoja na uchumi dhaifu, na migogoro ya chuki kati ya familia, na kadhalika.
Hii ni sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom