Nini kinasababisha wanaume kukimbia familia zao?

Siku hizi kwenye magroup ya wanawake, Wanalalamika sana wanaume kuwa achia watoto,

Na wao kutokomea kusikojilikana na kwenda kuanzisha family Nyingine huko. Je ni ugumu wa maisha,au gubu la mke,? Au ndo kuchokana?
Mwanaume utaachaje kujiondokea kwa hali iliyopo kwani:
1. Baba akijaribu kumwonya mtoto hapo nyumbani utasikia Ke anabwatuka " "usimwonee mwanangu" -Hapo inaibuka hoja kwa Me "kumbe huyu siyo mwanangu" halafu sheria zinamlinda kwa upendeleo mwanamke -Ustawi wa Jamii na Dawati la Jinsia ; e.g. Ke akikupeleka huko yan hata hauzungumza, tayari ww Me unachuliwa ww ndo mkosaji- Unamnyanyasa na kumdhalilisha mwanamke.
2. Mwanaume akitaka kufuata Utaratibu wa kisheria ili waachane kihalali (Talaka) mwisho wa siku mali inagawiwa pasu-pasu au kama wapo watoto basi mwanaume inakula kwake.
Ili kuepuka songombingo hilo, mwanaume anajiondokea taaratibu na kumwachia familia Ke ili huyo Ke ajue cha kufanya-kwa sababu mali haijagawiwa na hawezi kujimilikisha mali iliyopo hv-hv bila kufuata sheria. Ni mtihani huo kwa Ke.
3. Ke wengi wanapokuwa kwenye ndoa, huwa na kiburi sana, madharau na kupuuzia mambo hususan maelekezo ya mume na kusahau mume/baba ndiye kichwa cha Familia -huwa wanataka wakupande kichwani kitu ambacho kamwe hakuna mwanaume atakubaliana nacho.Ili kuepusha shari Me hujiondokea na kwenda kutafuta mahali kwingine atakapopewa heshima stahiki.
 
It’s not as simple as that mdau. Mara nyingi wanakimbizwa, kicked out like dogs! Poor men, who’s there to help them?! Lord have mercy on us men….
 
Mwanaume utaachaje kujiondokea kwa hali iliyopo kwani:
1. Baba akijaribu kumwonya mtoto hapo nyumbani utasikia Ke anabwatuka " "usimwonee mwanangu" -Hapo inaibuka hoja kwa Me "kumbe huyu siyo mwanangu" halafu sheria zinamlinda kwa upendeleo mwanamke -Ustawi wa Jamii na Dawati la Jinsia ; e.g. Ke akikupeleka huko yan hata hauzungumza, tayari ww Me unachuliwa ww ndo mkosaji- Unamnyanyasa na kumdhalilisha mwanamke.
2. Mwanaume akitaka kufuata Utaratibu wa kisheria ili waachane kihalali (Talaka) mwisho wa siku mali inagawiwa pasu-pasu au kama wapo watoto basi mwanaume inakula kwake.
Ili kuepuka songombingo hilo, mwanaume anajiondokea taaratibu na kumwachia familia Ke ili huyo Ke ajue cha kufanya-kwa sababu mali haijagawiwa na hawezi kujimilikisha mali iliyopo hv-hv bila kufuata sheria. Ni mtihani huo kwa Ke.
3. Ke wengi wanapokuwa kwenye ndoa, huwa na kiburi sana, madharau na kupuuzia mambo hususan maelekezo ya mume na kusahau mume/baba ndiye kichwa cha Familia -huwa wanataka wakupande kichwani kitu ambacho kamwe hakuna mwanaume atakubaliana nacho.Ili kuepusha shari Me hujiondokea na kwenda kutafuta mahali kwingine atakapopewa heshima stahiki.
Asante kwa uchambuzi wako nzuri
 
Siku hizi kwenye magroup ya wanawake, Wanalalamika sana wanaume kuwa achia watoto,

Na wao kutokomea kusikojilikana na kwenda kuanzisha family Nyingine huko. Je ni ugumu wa maisha,au gubu la mke,? Au ndo kuchokana?
Si sahihi kusema ni ugumu wa maisha pekee, wala si gubu la mke pekee. Wapo wanaume wanaokimbia majukumu kwa hiari, wapo wanaoshindwa kubeba mzigo wa kifedha, wapo wanaochoshwa na migogoro ya ndoa, na wapo wanaozuia kuonana na watoto baada ya kutengana. Lakini jambo moja halibadiliki: mtoto hana kosa. Wazazi wote wawili wana wajibu wa kumlea na kumjali, hata kama uhusiano wao umevunjika. Kila kesi ina sababu zake, hivyo tusihukumu kwa upande mmoja tu.
 
Nadhani imekubalika kwamba wapo wanaume wanaozikimbia familia zao na zipo sababu na sio hv-hv tu. Sasa tunaangalia je, kati ya mwanaume anayekimbia na Mwanamke anayeachiwa mzigo wa malezi kwa watoto nnani amesababisha kuwepo kwa tukio hilo au matokeo hayo yawepo?
Watoto kiukweli ni wahanga tu kwani hawahusiki kwa kiasi kikubwa labda iwe ni wale watoto wakubwa(Waliopevuka akili).
Watoto waliopevuka akili huwasikiliza sana mama yao ; na wamama wengi huitumia nafasi hiyo kama Fursa ya kumdhalilisha baba. Baba anaweza kutoa say fedha za chakula hapo nyumbani lakini mama atawaambia watoto bab'enu hanunui hata chumvi anajidai hana hela eti ananiachia mm ninunue kila kitu lakini kila siku anarudi mlevi, kazi ni kugomba tu. Cjui ntafanyaje na huyu baba yenu. Hapo mwanamke anajenga chuki kwa watoto dhidi ya baba yao. Jambo hilo likisha jijenga na kukomaa; mama anawatumia watoto kama fimbo au ngao dhidi ya baba. Hapo hamna namna kwani jeshi hilo tayari ni kubwa dhidi ya baba na ndipo baba anaamua kukimbia/ kuachana nalo anatokomea kujinusuru na kadhia / usumbufu/ kero hiyo.
 
Asilimia kubwa ni gubu la mwanamke. Asilimia ndogo ni ile inayotekwa "kilimbwata".
Naam. Nakubali hoja ya Gubu la mwanamke ila sio hoja ya kutekwa kilimbwata.
Wanawake wengi huzibomoa ndoa zao kwa mikono yao wenyewe - hata maandiko (Methali 14:1) yanakazia hoja hiyo.
Kwa habari ya limbwata(Limbwata ni kweli lipo) wanaume ndo 100% visababishi kutokana na Tabia zao za kutokutulia njia kuu au kuwa vigeu-geu na kutoaminika e.g. ahadi zisizotekelezwa, majigambo, Dharau, n.k.nk. Mara nyingi limbwata limetumika kama silaha(Kombora) la kumdhibiti mwanaume jeuri. Kumbuka kwamba limbwata pia lina hasara kubwa kwa upande wa wamama wanaoitumia silaha hiyo - haiwaachi salama. Kwa mantiki hiyo, utaona wanawake hufikia hatua ya kutumia limbwata kwa kusukumwa/shinikizo na wanaume.
 
Siku hizi kwenye magroup ya wanawake, Wanalalamika sana wanaume kuwa achia watoto,

Na wao kutokomea kusikojilikana na kwenda kuanzisha family Nyingine huko. Je ni ugumu wa maisha,au gubu la mke,? Au ndo kuchokana?
Gubu la mke ni kichocheo,japo wengine ni kukubali kuwa mateka wa mwanamke anayetaka ammlikiki asiye wake
 
Back
Top Bottom