Nini kinasababisha watu wa Afrika Magharibi kuwa na miili mikubwa kuliko wengine?

Nini kinasababisha watu wa Afrika Magharibi kuwa na miili mikubwa kuliko wengine?

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
719
Reaction score
2,408
Ebwanaeeeee hata kama maisha ni magumu ngoja twendeleeee...

Nchi za afica magharibi, NIGERIA, GHANA, TOGO, IVORY COAST, SENEGAL nk..nk.

Sasa nimekumbuka mwanzoni mwa mwezi wa pili kuna mjomba wangu mmoja ni mfanyabiashara haswa na nilifanikiwa kurula nae sana hizo nchi tajwa hapo juu ambazo ziko upande wa africa magharibi na katika kuzurula huko nikagundua aisee..... wale jamaa wana miili mikubwa mno kuliko sisi tulio chini ya jangwa la sahara.

Unakutana na kijana tu miaka 17 ana futi 6 karibia na inch kama 3 hivi nikajiuliza sababu ni nini nikakosa, nikaanza na kurejea hata wachezaji wanaocheza ligi kubwa ulaya waliotoka hizo nchi wako hivyo ni magiant kuliko kina samata hawa.

Hata yale black basketball giants yanayotamba ligi ya kikapu NBA marekani chimbuko lao ni West Africa, hata ukifuatilia mababu ya kina lebron james yametoka huko huko. Huku kwetu shida nini wazee?

Tusaidiane mapema ili kuwakomboa watoto wetu na hili wimbi la umbilikimo.

BADO NAUMIZA KICHWA HUKU CHINI YA JANGWA LA SAHARA TATIZO NI NINI?

KAMA NI UMASIKINI NAO NI MASIKINI TU ILA SHIDA NINI HUKU KWETU????
 
Wabantu ni mashombe kati ya Wanegro, wa Afrika magharibi, na Wahamiti wa kaskazini Mashariki ya Africa na Wapygmy wa Africa ya kati!

... Wanegro ni mabonge wakati Wahamiti na Wapygmy wana vimiili vidogo'vidogo na hiyo inapelekea mashombe, wabantu, kuwa na vimiili vidogo'vodogo kulinganisha na Wanegro, ukizingatia wastani!
 
Tembelea mikoa ya Mbeya, Shinyanga, Tabora, Mwanza na Mara utaelewa.
Hata hiyo mikoa walikuwa hivyo zamani, watu wa hivyo sasa hivi wapo wachache sana katika hiyo mikoa lakini huko west africa kila unaekutana nae barabarani ni bonge la jitu mpaka wanawake ingawa wanaume ndiyo zaidi.
 
Hawa wa huku kwetu ukimkuta mrefu basi mwembambaaa,tofaut na hao wanao miili ya kiuanaume halisia😊😊🤭🤭🤭,nadhan wao wakakula sanaaa vyakula vya asili kuliko huku
Kabisa, huku ukimkuta tall basi kimbaumbau balaa lakini huko kwa hao jamaa ni tofauti, ni magiant na miili mikubwa pia yani mbavu nene!!!
 
Back
Top Bottom