Nini kinawafanya Watanzania wengi waishi kwa matumaini makubwa sana kuhusu nchi yao ?

Nini kinawafanya Watanzania wengi waishi kwa matumaini makubwa sana kuhusu nchi yao ?

Kizazi kinachokuja Cha watawala ama watoto wa wale watawala wanaoishia Kama Mzee wasira and company ni kizazi dhaifu sana hakitaweza kuhimili mikiki ya gen z lazima kitaanguka tu
Watoto wa watawala si ndio hao wanaingizwa kwenye mfumo wa utawala mdogo mdogo wakina Rizimoko, Wanu, Jesca n.k !
 
Kama hivi ndivyo ilivyo ina maana hizi harakati zote za kupambana na CCM ni kupoteza muda tu kwa sababu ni sawa na kupambana na police, majeshi, usalama, TRA, mahakama na kila chombo !
Hii inafikirisha sana.
Yes kupambana na CCM ni kupambana na mfumo mzima uliopo Tanzania.

Umesahau zamani JWTZ tulikuwa tukisema zidumu fikra za mwenyekiti ?
 
Mkuu ongeza na opposition parties.
Ni ngumu sana kudeal na ccm kwa maneno ya kina Heche na Lissu pekee.
Mbona mwaka jana Oct.29 watu walioneshwa kwa vitendo na majeshi ni njia gani pekee ya kuingoa CCM madarakani.

Bloodshed pekee ndio ubatizo wa kung'oa mizizi ya CCM tofauti na hapo labda tusubiri miujiza ya mwana wa adabu atakapo rejea kwa mara ya pili kama waaminivyo wakristo.
 
Unaonaje badala ya kupambana kuing'oa CCM madarakani watu wote tujiunge CCM tuifanyie reforms kwa ndani iwe kama CCP ya China ?
 
Unaonaje badala ya kupambana kuing'oa CCM madarakani watu wote tujiunge CCM tuifanyie reforms kwa ndani iwe kama CCP ya China ?
Huwezi fika kwenye hizo nafasi za kufanya maamuzi kama sio mwenzao mkuu
 
Uwezekano wa kuendelea kuwa hivi kwa muda mrefu ni mkubwa sana. Mabadiliko wanayoota watanganyika yataleta maumivu kwa watawala wa sasa. Je watawala wa sasa wako tayari kupata hayo maumivu!!.
Pia watanganyika tunataka mabadiliko, lakini hatuko tayari kuyafanya yatokee.
Watanzania wanataka mabadiliko kiroho,wanaandamana kiroho na moyoni
 
Nashangaa sana watu kumshobokea sijui yuda, ccm wote wale wale. Ili mabadiliko yakotee ccm lazima isuguliwe kweli kweli mpaka moto uwake. Tupate silaha na sisi walalahoi tuone kama police wataendelea kuwalinda.
CCM itaanguka wala sio Zaidi ya miaka 25 ijayo
 
Hapo ndo ccm wanachekelea tu kama vile nyani kaachiwa shamba la mahindi. So sad mkuu
Na CCM kwa kulijua hilo,wanachekelea kweli,mbaya Zaidi wanaojua ukweli wa udanganyifu wote huo ni wachache sana hata hao ccm wenyewe wako wengi wanaumia ni vile tu Wana u CCM
 
Niliwahi kufungua uzi nikisema tatizo la hii nchi sio CCM pekee

Watu wakanijia juu na kuniita chawa
Kwa sababu nimesema wasivyopenda kusikia

Ila uhalisia mimi sina chama na sioni umuhimu
naunga juhudi yoyote ninae muona ana hoja

Nilisema hivi hii kampeni ya humu ku ignore ma machawa ili kutosikia wanachosema

Ni kama CCM inavyolalamikiwa kua inatumia nguvu kunyamanzisha watu

So hata hawa wanaohamasisha ku ignore ili kutosikia maneno pinzani wakipewa madaraka wataweza kuvumilia kukosolewa au watakua kama CCM?

Hili taifa linataka utakaso haswa
Wanaojiita wanaharakati wengi tu wa mitandaoni Tanzania wamejikuta wakichukia maoni yangu kisa tu sikubaliani nao na ni wanaharakati wanao fahamika na kuaminika na jamii kubwa ya Watanzania wanaojiita wapinzani huwa nafurahi na kucheka tu huenda hata nao hawajui wanacho pigania.

Lowassa alikuwepo CCM dakika za jioni kwenye kipindi cha uchaguzi akajiunga Chadema ndio siasa na vyama vyetu hivyo vya siasa vilivyopo nchini.

Changamoto za Chadema na vyama vingine vya upinzani hazionekani kwa asilimia kubwa kwa sababu bado hawapo kwenye ulaji wa nchi.

Sisi ni Watanzania tunaojuana na ndio maana hata hizo pesa zilizoitwa za Abdul ziliingia Chadema😀
 
Ukiwasikiliza watu wengi wa Tanzania wanaotamani mabadiliko wako na matumaini makubwa sana, wengi wanaamini kwa dhati kabisa ipo siku moja watesi wao watashindwa na kuanguka na nchi yao itakuwa yenye demokrasia pana na maendeleo tele.

Ni nadra kukuta wenye mtazamo mbadala kwamba Tanzania inaweza kuwa hivi ilivyo ndivyo itakavyokuwa daima. Kwamba Hakuna kitakachobadilika sana kama vile Nicaragua, Korea Kaskazini, Turkemenistan, Mynmar, Misri.
Kwasababu za KIHISTORIA.
 
Wanaojiita wanaharakati wengi tu wa mitandaoni Tanzania wamejikuta wakichukia maoni yangu kisa tu sikubaliani nao na ni wanaharakati wanao fahamika na kuaminika na jamii kubwa ya Watanzania wanaojiita wapinzani huwa nafurahi na kucheka tu huenda hata nao hawajui wanacho pigania.

Lowassa alikuwepo CCM dakika za jioni kwenye kipindi cha uchaguzi akajiunga Chadema ndio siasa na vyama vyetu hivyo vya siasa vilivyopo nchini.

Changamoto za Chadema na vyama vingine vya upinzani hazionekani kwa asilimia kubwa kwa sababu bado hawapo kwenye ulaji wa nchi.

Sisi ni Watanzania tunaojuana na ndio maana hata hizo pesa zilizoitwa za Abdul ziliingia Chadema😀
Niliwahi kusema kuhusu hili pia kaka
Ila mwisho unaitwa chawa
 
Unaonaje badala ya kupambana kuing'oa CCM madarakani watu wote tujiunge CCM tuifanyie reforms kwa ndani iwe kama CCP ya China ?
Nimewahi kuandika uzi wa namna hiyo sisemi CCM isiondoshwe lakini mpaka sasa dalili hizo za kuondoshwa hazipo basi njia pekee iliyobaki ni reforms zifanyike ndani ya CCM hata aina ya wagombea wanaoteua angalau wawe watu wenye akili na wenye kujua nini kimewafanya wateuliwe na chama na sio huu utumbo wa sasa.

Kuwa na kadi ya CCM,uanachama wake na mpaka kuwa kiongozi inapaswa kuwa ufahari sio wa kifedha wala connection bali how great mind you're sio kila mtu anapaswa kuona kuwa CCM ni kitu rahisi rahisi tu.

Leo hii kuwa CCM ni kitu chepesi,kumiliki kadi wala hakuna umaajabu wowote wenzao hao wachina hawajawahi kukichukulia chama chao kizembe hivi sisi huku sasa upuuzi mtupu.

Napata mashaka kama wanaCCM wana akili ya kuwaza haya kama tu mwenyekiti wao ni bogus vile.

CCM sio lazima kiwe chama chenye wanachama million hata wanachama 500 nchi nzima wanatosha as long as hawa ni best minds ndani ya nchii hii watu wengine hao mamilioni wabaki kuwa tu mashabiki wa chama cha CCM kwenye mikutano na kwenye chaguzi.

Kinacho hitajika ni chama cha watu wenye akili na sio kundi la misukule ya mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom