Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Unamaanisha watu wanaabudu mtu? 🙄
 
Huwezi tenganisha Mungu na dini. Ukishaamini katika Mungu tatari una dini, Unaamini vipi katika uwepo wa Mungu bila dini? Halafu una porojo.....
 
Huwezi tenganisha Mungu na dini. Ukishaamini katika Mungu tatari una dini, Unaamini vipi katika uwepo wa Mungu bila dini? Halafu una porojo.....
Porojo zikowapi kiongozi! Umesema Mungu ni wengi nilihitaji kufahamu applications za Mungu hawa wengi katika watu wao.
 
Kipato na kuongezeka kwa ufahamu na matendo ya wanaoitwa wapakwa mafuta.

Kwani hujui Mungu na dini ni vitu tofauti? Dini ziko kiupigaji,hata mimi namuamini Mungu ila dini na madhehebu yenu Nina miaka 6 sasa sijui vinafananaje
 
Kuna mambo hapa umegongelea misumari mithili ya ile ya Bethlehem! Hivi ni mimi tu ninayeona maskini, wasiojiweza, wanafiki, wanaozaa hovyo hovyo na watu wanaoishi tu kwa asilimia 95 ni walioloea katika dini?
Hao masikini,wanafiki,wasiojiweza na wote hao uliowataja kuwaona ktk dini ni kwamba wapo ktk dini hizo just only for their names. Ni Mkristo kwa sababu anaitwa Yakobo,Petero na Nathan au Omar,Yasin na Aisha kuwa mwislamu. Lakini ini reality hawako kwenye dini. Na hao unaowaona wanahangaishwa na mafuta,chumvi na keki kwenye dini hawako kwenye dini bali dini to them religion it has turned to be an opium kwa hayo madhira waliyonayo. Ndugu ni ukweli mchungu lakini ndo hivyo muhimu shikiria unachokiamini utaokolewa kwa rehema
 
Porojo zikowapi kiongozi! Umesema Mungu ni wengi nilihitaji kufahamu applications za Mungu hawa wengi katika watu wao.
mungu ni wengi sababu ni imani, na imani ni dini hivyo mungu=imani=Dini huwezi tenganisha.

Ng'ombe unayemkamua maziwa ni mungu kwa mwengine,

mwingine anaabudu jua ambalo kwako wewe ni sayansi, mwingine anaabudu YESU ambaye kwa mwislamu ni binadamu,

mwingine anaabudu MUNGU ambaye haonekanagi n.k n.k n.k

Kutoamini katika MUNGU asiyeonekana au anayeonekana nayo ni dini kipengele cha upagani.
 
Ilipoteza mvuto baada ya siasa kuchanganywa na dini. Hio ni moja ya sababu.

Pili viongozi wa dini kuacha au kupunguza harakat za kuitangaza injili kuamia kwenye kutangaza biashara.

Kupoteza viongozi wa din wenye uwezo wa kujibu maswali wakiufasahaa baada ya kuulizwa na waumini wao wenye uwezo mzuri wa kifanya reasoning.

Harakat za maisha zimechangia kutufqnya busy zaid kwenye utaftaji wa ugali kuliko kumtafta Mungu
 
Yap,binafsi dini za wazungu sizikubali,napendelea imani zetu za asili maana huko nako Mungu anatusikia,hizi za wazungu zina utapeli mwingi Sana
Wazee wa zamani waliomba na mvua zikanyesha.

Upo sahihi, Dini sio zilizoletwa na wazungu tu, hata imani kwa mizimu kama mungu ni dini na wazungu walizikuta mababu wakizitumia.

La muhimu tupendane pamoja na tofauti zetu za kiimani. Heshima iwepo na tusiuane na kubaguana sababu ya dini.
 
Watu wameanza kuachana na kufuata mambo ya kitapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…