Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Dah!. Binafsi naamini Mungu yupo na ndio aliyenibariki nipo na maisha mazuri kwa Sasa.
Ila sijaenda kanisani miaka na miaka ( Mimi ni RC). Tatizo kwa kweli zile sanamu na mipicha tunayoambiwa ni yesu Kule kanisani zinanikwaza sana. Yaani mtu kachonga mjisanamu wake na mti wa mpingo Leo hii naambiwa kuwa niheshimu kuwa ni mfano wa yesu!!?. Nimeshafafanuliwaga na watu mbali mbali kuhusu hizo sanamu Ila sikuwaelewa hata kidogo.
Nimejaribu kusali makanisa mbali mbali Ila kote kumenishinda.
Ila Kama sio sanamu na mipicha picha kanisani, basi RC is the best.
Unamaanisha watu wanaabudu mtu? 🙄
 
Ahaa! Ndio maana nirudi kusema hujawa na uwezo wa reasoning! Fahamu kutofautisha MUNGU na DINI! Kuna MUNGU na DINI.

Hao wengi wa kweli yupi? Anaweza kujisimamia ukimtoa katika dini? Mungu ndio chanzo cha maisha hao Mungu wengi unaweza kuonesha bidhaa zao?

Nikimaanisha MUNGU wa dini A watu wake wanatofauti zipi na MUNGU wa dini B, C na D etc? Wametumia material tofauti au wapo wanaozaliwa na wengine kushushwa au kutokea katika transition?
Huwezi tenganisha Mungu na dini. Ukishaamini katika Mungu tatari una dini, Unaamini vipi katika uwepo wa Mungu bila dini? Halafu una porojo.....
 
Huwezi tenganisha Mungu na dini. Ukishaamini katika Mungu tatari una dini, Unaamini vipi katika uwepo wa Mungu bila dini? Halafu una porojo.....
Porojo zikowapi kiongozi! Umesema Mungu ni wengi nilihitaji kufahamu applications za Mungu hawa wengi katika watu wao.
 
Habari 👋🏾

Nimefanya tafiti katika vipindi, nyakati na maeneo tofauti na inaonekana wazi ushawishi wa dini unapungua kwa kasi kubwa sana.

Inaonekana wengi kutokuwa na hakika katika dini mbalimbali na wengi wao bado wanajaribu kujionesha katika ngwe hiyo kwa sababu kadhaa ikiwemo kutokataliwa na jamii hizo.

Je, ni ipi sababu ya ukuaji wa kiwango hiki cha watu kutokuwa na dini kama ilivyozoeleka?
Kipato na kuongezeka kwa ufahamu na matendo ya wanaoitwa wapakwa mafuta.

Kwani hujui Mungu na dini ni vitu tofauti? Dini ziko kiupigaji,hata mimi namuamini Mungu ila dini na madhehebu yenu Nina miaka 6 sasa sijui vinafananaje
 
Kuna mambo hapa umegongelea misumari mithili ya ile ya Bethlehem! Hivi ni mimi tu ninayeona maskini, wasiojiweza, wanafiki, wanaozaa hovyo hovyo na watu wanaoishi tu kwa asilimia 95 ni walioloea katika dini?
Hao masikini,wanafiki,wasiojiweza na wote hao uliowataja kuwaona ktk dini ni kwamba wapo ktk dini hizo just only for their names. Ni Mkristo kwa sababu anaitwa Yakobo,Petero na Nathan au Omar,Yasin na Aisha kuwa mwislamu. Lakini ini reality hawako kwenye dini. Na hao unaowaona wanahangaishwa na mafuta,chumvi na keki kwenye dini hawako kwenye dini bali dini to them religion it has turned to be an opium kwa hayo madhira waliyonayo. Ndugu ni ukweli mchungu lakini ndo hivyo muhimu shikiria unachokiamini utaokolewa kwa rehema
 
Porojo zikowapi kiongozi! Umesema Mungu ni wengi nilihitaji kufahamu applications za Mungu hawa wengi katika watu wao.
mungu ni wengi sababu ni imani, na imani ni dini hivyo mungu=imani=Dini huwezi tenganisha.

Ng'ombe unayemkamua maziwa ni mungu kwa mwengine,

mwingine anaabudu jua ambalo kwako wewe ni sayansi, mwingine anaabudu YESU ambaye kwa mwislamu ni binadamu,

mwingine anaabudu MUNGU ambaye haonekanagi n.k n.k n.k

Kutoamini katika MUNGU asiyeonekana au anayeonekana nayo ni dini kipengele cha upagani.
 
Ilipoteza mvuto baada ya siasa kuchanganywa na dini. Hio ni moja ya sababu.

Pili viongozi wa dini kuacha au kupunguza harakat za kuitangaza injili kuamia kwenye kutangaza biashara.

Kupoteza viongozi wa din wenye uwezo wa kujibu maswali wakiufasahaa baada ya kuulizwa na waumini wao wenye uwezo mzuri wa kifanya reasoning.

Harakat za maisha zimechangia kutufqnya busy zaid kwenye utaftaji wa ugali kuliko kumtafta Mungu
 
Yap,binafsi dini za wazungu sizikubali,napendelea imani zetu za asili maana huko nako Mungu anatusikia,hizi za wazungu zina utapeli mwingi Sana
Wazee wa zamani waliomba na mvua zikanyesha.

Upo sahihi, Dini sio zilizoletwa na wazungu tu, hata imani kwa mizimu kama mungu ni dini na wazungu walizikuta mababu wakizitumia.

La muhimu tupendane pamoja na tofauti zetu za kiimani. Heshima iwepo na tusiuane na kubaguana sababu ya dini.
 
Habari [emoji1480]

Nimefanya tafiti katika vipindi, nyakati na maeneo tofauti na inaonekana wazi ushawishi wa dini unapungua kwa kasi kubwa sana.

Inaonekana wengi kutokuwa na hakika katika dini mbalimbali na wengi wao bado wanajaribu kujionesha katika ngwe hiyo kwa sababu kadhaa ikiwemo kutokataliwa na jamii hizo.

Je, ni ipi sababu ya ukuaji wa kiwango hiki cha watu kutokuwa na dini kama ilivyozoeleka?
Watu wameanza kuachana na kufuata mambo ya kitapeli
 
Back
Top Bottom