Nini kitatokea endapo Dunia itaacha kujizungusha ktk mhimili wake na pia endapo itaacha kulizunguka jua?

Ndiyo kiama chenyewe hicho. Ikitokea kusimama ghafla tutarushwa sana na utakiuwa ndio mwisho wa uhai (kiama). Ikitokea kupungua kasi (decelarate) na hatimae kusimama kabisa itakuwa pia ndio mwisho wa uhai wa binadamu (kiama).
 
Ikumbukwe kua jua nalo kuna sehemu linavutwa na lenyewe lina rotation yake na ya namna yake.

Mkuu naomba ufafanuzi zaidi hapo.
Ebu tupatie maelezo kidogo, kwa kbukbu zangu za shuleni jua lilo stationary na heavenly bodies zingine ndio zazunguka jua.
 
Masahihisho:
Majira ya mwaka yanapatikana kwa dunia kuzunguka jua, dunia kujizungusha katika mhimili wake tunapata usiku na mchana tu.
Masahihisho,jua nyota na mwezi ndio vinavyo izunguka dunia.
 
Namba 5,hayo mabomo ya nyukilia nini chanzo chake?
 
Kutenda kuna mipaka ila sio kufikiria. Labda wamaanisha kufikiria na kuyaongea uliyofikiria. Kufikiria hakuna mipaka, iwe kirichofikiriwa chawezekana au hakiwezekani ila kukifikiria hakuna mipaka.
 
hivyo vitu tunafikiria tu lakini haviwezi kutokea kwame,
uhakika huo tunaupata kwenye Zaburi 104: 5 "Ameiimarisha dunia juu ya misingi yake; Haitasogezwa kutoka mahali pake milele na milele."
Tumsifu Yesu Kristo.
 
Itasimama dede....
 
Sisi kabla tulikuwa tunauliza maswali mfano wa hayo. Wasomi wetu wakawa wanatujibu hivi "Subirini itokee kwanza ndio tutawajibu"
Wasomi wenu walikuwa kina nani? Wanahitaji kunyongwa mpaka kufa kwa kutengeneza kizazi chenye uwoga wa kufikiri bila kujari kifikiriwacho kinawezekana au laa.
 
Mfano mdogo tu,panda ndege ruka hewani kisha tua ardhini,kama ingekuwa dunia inazunguka basi ungejikuta umetua marekani au china.
Nami mfano wangu, nzi aliye ndani ya gari inayokimbia 90km/h, je akiruka kutoka siti ya nyuma kwenda ya mbele ndani ya hilo hilo gari akiwa ndani atabamizwa nyuma sababu gari linatembea 'litamuacha' au atafika siti ya mbele?

Au umewahi panda au ona mtu kapanda kwenye pickup nyuma iliyo wazi na inatembea kwa kasi tu, akirusha chungwa juu bado ataweza kulidaka mkononi alipolirushia licha ya kwamba gari linatembea chungwa halitadondoka nyuma sababu lineachwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…