Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Haikuwepo na haja ya kujenga bwawa jipya Hali ya zamani yangeweza boreshwa, kwa kuondoa michanga na matope mabwawani pia kubadili injini za zamani na kufunga za kisasa maji kidogo speed kubwa umeme mwingi
Kufanya maintenance ya jengo au mradi huwa ni gharama zaidi kuliko kununua kitu kipya na kufanya Installation. But all in all uko sahihi kwa maana marekebisho ni muhimu
 
Kwanza nianze tu kwa kukupongeza unastahili PHD ya uongo na siasa sasa twende chin
Kwanza kabisa mrad huo pesa nying zimekopwa na sio pesa zetu za ndan zaid ya 60% ni pesa za mkopo

Sasa tuje kwenye technical specification MEGAWATTS ww umeongea kisiasa siasa tu ila kwa ma ELECTRICAL ENGINEET wanakuchora tu unaposema MEGA means million kwaio unaposema 2115 MW maana yake ni 2115000000 watts
Sasa tuje kwenye watts watts ni S1 unit ya power na neno power lina maana kubwa sn kwenye physics maana mbali na umeme linatumika mpaka kwenye mechanics na thermodynamics

Sasa ili tusilete sound hapa tulete formula ya power kwenye umeme

Ohm's law equation (formula): V = I Γ— R and the power law equation (formula): P = I Γ— V. P = power

Kifaa chochote kile cha umeme lazima kiandikwe kinatumia nishati kiasi gan mfano TV kubwa sn inatumia 400watts
Kwa maana km bwana linazalisha 2115 watts basi litaweza kuwasha tv 5287500 au tuseme TV million 5

Kwa hesabu hzo tu nan kakudanganya km mgawo utaisha nan kakudanganya km umeme utashuka bei

Niliitaka nikuumbie pia kwenye swala bei ila nimeona bora nikukaushie tu maana sio ww ni buku 7 io
 
Mwambie uyo naenda kukojoa narud
Mh Rais Dr. John Pombe Magufuli leo akiwa Kinyerezi, Dar es salaam amesemasualala ajira kwa vijana awamu ijayo litatatuliwa tu. Lakini pia hii miradi itaajiri sana ndiyo maana kwa sasa serikali inapambana kutengeneza miradi mikubwa ya kudumu yenye kutoa ajira za kudumu
 
Hizi ni zile hesabu kama za motivesheni spika, kiufupi msitegemee jipya lolote.

Panapo majaliwa, huenda 2025 tutakuwa tukipigia kampeni umeme wa makaa ya mawe au mionzi ya jua.
 
Niambie kwa sasa nchi nzima Tanzania tunatumia MW ngapi kwa matumizi ya ndani,.. na MW ngapi kwa matumizi ya viwandani.

I rest my case here.
 
Hakuna Jengo lolote ambalo linaweza likatumia hata Megawatt moja duniani usitufanye sie wajinga . Kwenye jengo hilo na Mkapa kuna furnace za kuyeyushia dhahabu au chuma punguzeni uongo wewe unaonekana umesomea siasa tu na kukaa kwenye keyboard kuleta uongo huku ukibadili ID zako.
 
Anza hata leo gesi asilia kwenye gari

Wakati unakuja na mambo ya gesi taf pitia comment no. 3 tupate ukweli. Kwa kukumbusha tu mtungi wa kawaida unasimama Tshs 45,000/- mpaka 49,500/= (ORYX) kwa bei ya sasa.
 
Kwani haukuwepo kwenye zile Ajira milioni 6 za miaka mitano iliyopita...Serikali imesema imetengeneza ajira milioni 6 kwa mwaka 2015 - 2020. Sasa kama umekalia vyeti vyako unasubiria yajayo yanayofurahishwaa shauri yako.. πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€.

Alafu mdogo wangu usiwasikilize wanasiasa na kuamini wasemacho..nakumbuka ile ahadi ya kila kijiji aliyoitoa mgombea wetu October, 2015?? We waache waongee tu jitahidi ujiajiri kama wanavyotushauri wenyewe wanasiasa wakati wao wanapambana wapewe kura wapate ajira kwa kutumia midomo tuu..au teuzi kwa kusifia sanaa...kujiajiri hawawezi kamwee..
 
Halafu huu wa kinyerezi na vyanzo vingine vya maji tunaupeleka wapi?kama tunauza uhakika wa soko upo? Je wataumaliza wote au?...vyanzo vingine kama mtera,nyumba ya mungu nk vingeboreshwa je tusingeweza fikia megawatt hizo za stigler?..kama zingefikiwa hudhani kwamba ingekua busara kiuchumi hii hela ya stigler zingejengwa skimu za umwagiliaji vijana wangepata ajira huko?..ukiweka na viwanda vyepesi vya kuchakata hayo mazao yatokanayo na skimu huoni tungekua tumeyagusa maisha ya raia moja kwa moja na serikali ingepata kodi chapu?
 
Tuna safari ndefu kwa uelewa huu.
Palitakiwa pajengwe skimu za umwagiliaji kuajiri watu kwenye kilimo na viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo,ina tija kwa tra na raia kuliko kihangaika na umeme wakati wa vyanzo vingine upo,ile sgr sioni hata haja yake maana pana mtandao mkubwa barabara za lami
 
Kwani huo mradi una tofauti gani na kidatu? Je Kidatu imeishia wapi?
Je bwawa la Mtera limeishia wapi?

je gas ya Mtwara imeishia wapi?

tumechoka kudanganywa kila siku.
 

Mataga umechanganyikiwa
 
Umeme pekee hauwezi kumwagilia bila uwepo wa scheme hizo.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Labda hukunisoma vizuri. Kushuka kwa bei ya umeme inaweza kuwa motisha kwa wanaotaka kuanzisha hizo scheme. Mimi ninayo micro scheme, gharama za umeme kuvuta maji toka kisima kirefu zinafanya mapato ya mradi kuwa kidogo sana hasa mikoa ya kanda ya kati yenye ukame mkubwa.

Umeme ukipunguzwa bei tukalipa kwa mfano sh 100/unit, itawavutia wengi ku-invest kwenye schemes ndogondogo za umwagiliaji kwakuwa zitalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…