Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Inategemea anasumbuq kuhusu nini, jeuri, kiburi, dharau, si mnyenyekevu, si msikivu, mzinzi, hakaliki nyumbani, hana uaminifu labda pesa anaiba, udanganyifu au uongo, urafiki na mashosti mashankupe, mlevi wa simu na tv, mchafu hapendi usafi, anajiamulia vitu bila kuomba ruhusa, nini hasa ukiweka bayana ni vizuri hicho kisa chenyewe
Maneno, kiburi, dharau, hashauriki, ni yeye na simu, simu na yeye muda wote yuko insta anawafuatilia ma superstar hadi anasahau majukumu yake
 
Maisha yakuishi kumbembeleza mwanamke kama mtihani nilishafaulu.Chunguza chanzo nini,kama kosa sio lako usiogope piga chini sio wako huyo,Utapata mwingine mtakao endana taabia,Msanii anaolewa na msanii mwenzake,Mie wakwanza nilitimua baada ya 5yrs nikaa 2yrs nikaoa mwingine 4yrs nikatimua nikaa 1yrs nikaoa mwingine kwasasa 10yrs niko nae maisha ya raha sana namshukuru Mungu.NB Ukiona mnapishana kila kitu sio NYOTA YAKO
 
Mzee mmoja wa kichaga alikuwa anampa wasaa mwanae wa kiume kwenye harusi yake. Akamwambia "Mwanangu mimi sitaki kupindisha maneno. Nakuambia ukweli. Ukubali ukatae shauri yako. Akamwambia kwenye ndoa yako ukiona vituko vimezidi cheki mfukoni mwako au katika account yako ya benki.Ukiona mfuko uko vizuri na benki uko vizuri na bado vituko haviishi ujue wewe ndio tatizo.

Lakini ukiona mfukoni hauna kitu na benki hauna kitu na vituko haviishi tafuta hela. Ukishindwa muache mtoto wa watu aende. Kama ni wako atarudi. Kama sio wako sio wako tu hata ukeshe unaomba. Sikubaliani na "conclusion" ya huyu mzee wa kichaga lakini siwezi kumpinga kwa sababu ni mzee na ameona mengi.
Binafsi nmemuelewa na naamin changu ni changu tyu
 
Kopi and paste
 
Ongea naye kwa kina ikishindikana washirikishe Wazazi wa pande zote mbili na viongozi wa Dini.
 
Mi niliamua kuwa na nyumba 2, naaga nasafiri mkoani kumbe niko hapa hapa mjini, kila weekend niko home, hii imepunguza kelele
 
Maneno, kiburi, dharau, hashauriki, ni yeye na simu, simu na yeye muda wote yuko insta anawafuatilia ma superstar hadi anasahau majukumu yake
Sasa huyo Kwa hizi tabia likely pia anapakuliwa, na kama pia kazi za nyumbani anafanya zote house girl, angalia je chumbani kwenu umakini wa usafi ukoje, anafanya regularly? anapiga pasi nguo zako, aina hii dawa yao ni taarifa zifike Kwa wazazi wake aibu ya kifamilia ndio inanguvu ya kumbadilisha tabia, kushatakia Kwa wakwe sijajua kanuni ikoje ila ndio jibu zito la kumshtua. Everytime unamuongelesha record mazungumzo ushahidi wa majibu kwenye family matters ni msingi wanabishaga hao.
 
Mnakaa chini unamuelekeza anachofanya si kizuri, na kumvumilia. Wanawake wote tuna vituko, vinatofautiana tu....na sio makusudi ndivyo tulivyoumbwa.

Muhimu kuwa na mke ambae anarekebishika akirekebishwa.

Ndoa ni zaidi ya hilo....japo hilo ni sehemu muhimu ya ndoa.
Maneno kuntu sana haya
 
Back
Top Bottom