Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Mzee mzima ile pisi kali inakuzingua eeh ?

Wadada hawa wa sasa wengi wao ni jeuri.ni wachoyo sijui hata ni nini kimetokea.

Vumilia
 
Waga ni vituko gan anaanza ndo upelekea kuamua kuchukua maamuzi flan
So sema kituko gan haswa anafnya ili usaidiwe kwenye hilo tukio
 
Mimi nadhani mambo ya 50 50 ndo yanaleta shida sana, hvyo mwanaume unapo oa hakikisha uanakua mwanaume kweli kwani sie wanawake hua tunatabia ya kupima upepo tukitest tukiona tunaweza kuwaendesha basi tunafanya hvyo.

Ni wajibu kwa mwanaume asimamie abc zake anazotaka na kutimiza wajibu wake kwenye ndoa na mke ajua kabisa mume wangu ananipenda na anataka hivi na vile na nikicross huu mstari mume ndo itakua limit yake. Kwa kufanya hvi ninaamini mke hatosumbua na heshima itakuepo nawe mume pia utamuheshimu mke
Umeongea ukweli binafsi imenikuta, kiuhalisia mimi ni mpole sana sasa kuna mwanamke nilikua nae kwenye mahusiano akaanza kuchukulia personality yangu kama mwanya wa kuniona mdhaifu fulani hivi ilifika hatua nikashindwa kuvumilia nikamwacha sasa hivi naona anataka kurudi anauliza habari zangu kwa marafiki zangu akijua nipo kiwanja fulani lazima aje akiniona amekua akinichangamkia sana ila tayari nipo na mwingine kama binadamu nae ana madhaifu yake ni visa visa vya kike si unajua wanawake muda mwingine wanamis tu drama za hapa na pale ila analekebishika nikamwambia hiki sitaki harudii tena sio pasua kichwa kama mtangulizi wake
 
Falsafa ya ndoa.
0 - 5yrs. = mahaba niue niponde kama kokoto. In short ni honeymoon phase, mpka miguu utakandwa. Pia hapa wale mafisi hawakosekani, wataendelea kumsumbua wife lakini most times unakuta kashika msimamo. Pia ndo kipindi anakuchunguza kama zile ahadi ulizokua unaweka unazitimiza maana wanawake wenyewe wanaamini kwenye ndoto na sio reality. Pia atakua msaada mkubwa kujitahidu msaidiane kufikia malengo.
5-10yrs - hapa ndo hua kisebengo kinaanza. Maana kipindi hiki ndo unakuta tayari ana katoto kamoja maximum viwili, pia kazini unaeza kuta kapandishwa cheo na mshahara juu (usisahau linapokuja suala la pesa, kwa mwanamke ni changu changu, chako chetu). Pia hiki kipindi ka dharau ndo kanakua kazito maana anaanza kuamini anaeza kutoboa yeye mwenyewe na akalea watoto because uwezo upo. Pia anaanza kuona ananyimwa uhuru n.k. kama anakula vzur anaanza kupendeza zaidi, na hapa wanakuja mafisi wakubwa (ze mubabaz). Hiki kipindi ni kigumu na ukikivuka tunasema ni nusu ya safari.
10-15yrs - hapa wenge hua linakata. Akicheki ndani watoto hata watatu tayari, pia jua lishaanza kuzama, hayuko marketable kama zamani. Hapa wanarudi kwa spidi kubwa kujitahidi kuleta maendeleo makubwa ndani ya familia ili msizeeke kiugumu n.k. heshima itakua 50% lakn utajihisi kama mko pamoja kwenye utaftaji n.k
15 - 20yrs - katika kipindi hiki hua mwanamke anakubali yaishe. Mtakapokua mmefikia hapo ndo anaona bas tena. Kama mko apeche aroro, atakubali tu hvo hvo. Hakuna tena maximum struggle, ni kujitahd kumaintain kilichopo. Heshima inakua 25% in short mwanaume huna jipya. Lawama hazikosekani kua ulichezea maisha na wanawake zako n.k. yapasa moyo mgumu
20 - 25yrs - hapa ndo kipindi most men unahangaika na magonjwa yasioambukiza kama presha na kisukari. Kipindi hiki pia watoto wamekua a.k.a tayari wamekua ugali i.e wako tayari. Hapa mwanamke anageukia watoto na kuanza kuwaonyesha upendo uliokithiri ukiunganishwa na lawama nyingi kwako ili yeye aonekane zaidi. Kwahyo usipoangalia hapa unabaki mwenyewe yeye na watoto mahaba ndindindi.. kama kawaida mwanaume unakaza moyo.
25-30yrs - most times japo ni ajabu hiki ndo kipindi ndoa nyingi zinavunjika. Mwanaume anastaafu anapata fungu lake. Anaanza kulichezea kama hana akili nzuri maana anaona sasa hv yuko mboga hakuna wa kumbabaisha. Usisahau pia wife hapa pia anaeza kua anazichota kwa spidi kubwa. Mwanaume anajiona kama kijana na yeye hakosi totoz. Mwanamke anatumia hiki kama kigezo cha kuona anaonewa. So hapo ndo safari za kwenda kwa watoto zinakua nyingi. Mwanaume unabaki mwenyewe unahangaika yeye yuko kwa watoto anazunguka na kulelewa.
30 - 35 yrs - uzee tayari, uko mwenyewe maana wife unamuona kwa manyato. Watoto tayari wamekutenga unabaki huelewi kipindi. Kama upendo bado upo hapa mtazeeka nae kama watu mnaofahamiana, yaani hakuna vurugu kila mtu anamjua mwenzake kiundani. Tofauti na hapo unakula ngumi ya ndoige, wana tunakula mpunga, tunakufukia chini tunakusahau.
Neno langu sio sheria. Kila mtu amuombe Mungu ampe rehema
You are good at observing umeandika vitu kweli nmeviona sehem nyingi.
 
Awali changamoto zinapoanza unapaswa kutambua chanzo kwanini amekuwa hivyo.
Unapotambua kama ni suala la upande wako au wake, ikishakuwa mmeoana ina maana mnao uwezo wa kuzungumza maana kwenye kuoa ama kuolewa sio tena nafsi ya mimi au wewe ni sisi, zungumza nae.
Ikiwa ameshindwa kubadilika, lipeleke jambo hilo kwa mshenga au wazazi wa mkeo na wako na anza kwa mzazi wa kike.
Ikishindikana na hapo uamuzi ni wako
1. Kuangalia kama jambo haliathiri maisha yako mpuuze, atapoona ulifuatili ni rahisi kuacha.
2. Kuwa mkali kwake, ukiwa umkosoi na jambo lina kuumiza utapata msongo, mzingue na wewe ila sio kwa kuhatarisha maisha yake.
3. Omba umrudishe kwao, kama yupo tayar kubadilika, atajifunza wakat akiwa mbali nawe.
4. Mpe talaka. Kama amefikia kukutishia maisha, hiyo ni hatari, sio kila atakaye kutoka usema.
Tujifunze sio kila tatizo la mke linasababishwa na yeye, mengine ushinikizwa hata na familia yake, mashoga, maisha, kupata mwanaume mpya, kuchoka, uigaji, vipimo vya mapenzi nk
Upo utofauti mkubwa kwa wanawake na wanaume, mwanaume hawezi kwenda dukani kununua kiatu akiwa peku ila mwanamke anaweza, na ndio maana anapomtapika mwanaume ni rahisi kuishi maisha ayapangayo ndani ya nyumba ya mwanaume aliye muoa(amejihifadhi tu akisubiri kuchukuliwa na mwenzie).
 
Mzee mmoja wa kichaga alikuwa anampa wasaa mwanae wa kiume kwenye harusi yake. Akamwambia "Mwanangu mimi sitaki kupindisha maneno. Nakuambia ukweli. Ukubali ukatae shauri yako. Akamwambia kwenye ndoa yako ukiona vituko vimezidi cheki mfukoni mwako au katika account yako ya benki.Ukiona mfuko uko vizuri na benki uko vizuri na bado vituko haviishi ujue wewe ndio tatizo.

Lakini ukiona mfukoni hauna kitu na benki hauna kitu na vituko haviishi tafuta hela. Ukishindwa muache mtoto wa watu aende. Kama ni wako atarudi. Kama sio wako sio wako tu hata ukeshe unaomba. Sikubaliani na "conclusion" ya huyu mzee wa kichaga lakini siwezi kumpinga kwa sababu ni mzee na ameona mengi.
Ni Africa tu mzee akizeeka hata Kama alikuwa tahira ujanani Basi maneno yake ya uzeeni watayachukulia kwa umakini


Hakuna uhusiano wowote Kati ya kuishi kwingi nakupitia mengi


At my age niliwahi mwambia baba yangu kabla hajafariki kuwa nilichopitia kwenye mahusiano yangu toka nimekuwa mkubwa am sure hajawahi pitia nilichokiona na matukio tofauti kwa wasichana wangu
 
Ndoa za Kimasikini shida yao ni pesa tu!? Je Ndoa za kitajiri shida yao inakua Nini!!??
Hata huyo mwanamke ameolewa na tajiri sababu ya pesa.

90% ya ndoa za kimasikini huvunjika sababu ya njaa.
 
Back
Top Bottom