Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Maneno, kiburi, dharau, hashauriki, ni yeye na simu, simu na yeye muda wote yuko insta anawafuatilia ma superstar hadi anasahau majukumu yake
 
Maisha yakuishi kumbembeleza mwanamke kama mtihani nilishafaulu.Chunguza chanzo nini,kama kosa sio lako usiogope piga chini sio wako huyo,Utapata mwingine mtakao endana taabia,Msanii anaolewa na msanii mwenzake,Mie wakwanza nilitimua baada ya 5yrs nikaa 2yrs nikaoa mwingine 4yrs nikatimua nikaa 1yrs nikaoa mwingine kwasasa 10yrs niko nae maisha ya raha sana namshukuru Mungu.NB Ukiona mnapishana kila kitu sio NYOTA YAKO
 
Binafsi nmemuelewa na naamin changu ni changu tyu
 
Kopi and paste
 
Ongea naye kwa kina ikishindikana washirikishe Wazazi wa pande zote mbili na viongozi wa Dini.
 
Mi niliamua kuwa na nyumba 2, naaga nasafiri mkoani kumbe niko hapa hapa mjini, kila weekend niko home, hii imepunguza kelele
 
Maneno, kiburi, dharau, hashauriki, ni yeye na simu, simu na yeye muda wote yuko insta anawafuatilia ma superstar hadi anasahau majukumu yake
Sasa huyo Kwa hizi tabia likely pia anapakuliwa, na kama pia kazi za nyumbani anafanya zote house girl, angalia je chumbani kwenu umakini wa usafi ukoje, anafanya regularly? anapiga pasi nguo zako, aina hii dawa yao ni taarifa zifike Kwa wazazi wake aibu ya kifamilia ndio inanguvu ya kumbadilisha tabia, kushatakia Kwa wakwe sijajua kanuni ikoje ila ndio jibu zito la kumshtua. Everytime unamuongelesha record mazungumzo ushahidi wa majibu kwenye family matters ni msingi wanabishaga hao.
 
Mnakaa chini unamuelekeza anachofanya si kizuri, na kumvumilia. Wanawake wote tuna vituko, vinatofautiana tu....na sio makusudi ndivyo tulivyoumbwa.

Muhimu kuwa na mke ambae anarekebishika akirekebishwa.

Ndoa ni zaidi ya hilo....japo hilo ni sehemu muhimu ya ndoa.
Maneno kuntu sana haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…