Nini ufanye mkeo anapoanza vituko ndani ya ndoa?

Mzee mzima ile pisi kali inakuzingua eeh ?

Wadada hawa wa sasa wengi wao ni jeuri.ni wachoyo sijui hata ni nini kimetokea.

Vumilia
 
Waga ni vituko gan anaanza ndo upelekea kuamua kuchukua maamuzi flan
So sema kituko gan haswa anafnya ili usaidiwe kwenye hilo tukio
 
Umeongea ukweli binafsi imenikuta, kiuhalisia mimi ni mpole sana sasa kuna mwanamke nilikua nae kwenye mahusiano akaanza kuchukulia personality yangu kama mwanya wa kuniona mdhaifu fulani hivi ilifika hatua nikashindwa kuvumilia nikamwacha sasa hivi naona anataka kurudi anauliza habari zangu kwa marafiki zangu akijua nipo kiwanja fulani lazima aje akiniona amekua akinichangamkia sana ila tayari nipo na mwingine kama binadamu nae ana madhaifu yake ni visa visa vya kike si unajua wanawake muda mwingine wanamis tu drama za hapa na pale ila analekebishika nikamwambia hiki sitaki harudii tena sio pasua kichwa kama mtangulizi wake
 
You are good at observing umeandika vitu kweli nmeviona sehem nyingi.
 
Awali changamoto zinapoanza unapaswa kutambua chanzo kwanini amekuwa hivyo.
Unapotambua kama ni suala la upande wako au wake, ikishakuwa mmeoana ina maana mnao uwezo wa kuzungumza maana kwenye kuoa ama kuolewa sio tena nafsi ya mimi au wewe ni sisi, zungumza nae.
Ikiwa ameshindwa kubadilika, lipeleke jambo hilo kwa mshenga au wazazi wa mkeo na wako na anza kwa mzazi wa kike.
Ikishindikana na hapo uamuzi ni wako
1. Kuangalia kama jambo haliathiri maisha yako mpuuze, atapoona ulifuatili ni rahisi kuacha.
2. Kuwa mkali kwake, ukiwa umkosoi na jambo lina kuumiza utapata msongo, mzingue na wewe ila sio kwa kuhatarisha maisha yake.
3. Omba umrudishe kwao, kama yupo tayar kubadilika, atajifunza wakat akiwa mbali nawe.
4. Mpe talaka. Kama amefikia kukutishia maisha, hiyo ni hatari, sio kila atakaye kutoka usema.
Tujifunze sio kila tatizo la mke linasababishwa na yeye, mengine ushinikizwa hata na familia yake, mashoga, maisha, kupata mwanaume mpya, kuchoka, uigaji, vipimo vya mapenzi nk
Upo utofauti mkubwa kwa wanawake na wanaume, mwanaume hawezi kwenda dukani kununua kiatu akiwa peku ila mwanamke anaweza, na ndio maana anapomtapika mwanaume ni rahisi kuishi maisha ayapangayo ndani ya nyumba ya mwanaume aliye muoa(amejihifadhi tu akisubiri kuchukuliwa na mwenzie).
 
Ni Africa tu mzee akizeeka hata Kama alikuwa tahira ujanani Basi maneno yake ya uzeeni watayachukulia kwa umakini


Hakuna uhusiano wowote Kati ya kuishi kwingi nakupitia mengi


At my age niliwahi mwambia baba yangu kabla hajafariki kuwa nilichopitia kwenye mahusiano yangu toka nimekuwa mkubwa am sure hajawahi pitia nilichokiona na matukio tofauti kwa wasichana wangu
 
Ndoa za Kimasikini shida yao ni pesa tu!? Je Ndoa za kitajiri shida yao inakua Nini!!??
Hata huyo mwanamke ameolewa na tajiri sababu ya pesa.

90% ya ndoa za kimasikini huvunjika sababu ya njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…