Mwanza ni unlimited au ArushaKwa mim ambaye nimetoka morogoro nipo tarime kikaz nalazimika kuagiza toka Moro ambako ndio mwenyej au labda niingie mtandaon
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanza ni unlimited au ArushaKwa mim ambaye nimetoka morogoro nipo tarime kikaz nalazimika kuagiza toka Moro ambako ndio mwenyej au labda niingie mtandaon
Alikuwa anasimamia kituo kimoja isipokuwa vingine alikuwa akienda kwa dharula. Lakini usiku wa tukio hakuwa kikazi. Japo naona wizara ya afya wametoa ripoti kwamba alikuwa akielekea kazini jambo ambalo sio kweli. Ukifika nyamongo ukasema alikua anaenda kazini usiku ule watakushangaa mno.Kuna mahali nimeskia alikua anasimamia vituo vitatu, je hilo lina ukweli?
Kama ni kweli, je Kati ya hivyo vituo hakuna kilichopo uelekeo wa huko alipokua anaenda huo usiku?
Mkuu samahani kaa hutojali. Unaweza ukataja maeneo ambako hayo matukio yalitokea? Maana mgodini watu kupigwa risasi na askari sio issue kabisa na huemda umeenda nyamongo wakati matukio ya risasi yamepungua kwa kiasi kikubwa sanaHuku nyamongo, kuna shida kubwa sana, ndani ya mwaka huu, wameshauawa watu zaidi ya kumi,kuna dada alikutwa amepigwa risasi, kuna wengine wawili walichomwa na visu kwenye uke katika matukio tofauti,wakafa kwa kupoteza damu nyingi.. kuna mwingine aliuliwa mgodini kwa kupigwa risasi, kuna mwingine alikutwa amejinyonga, lakini watu wanasema kuwa alipigwa na mume wake mpaka akafa,.. kuna wengine waliuliwa wawili kwa wakati mmoja.... Kuna mwingine aliuliwa kwa kusingiziwa kuwa ni mwizi, kumbe hakuwa mwizi..... Na katika matukio hayo yote ni mawili tu, watu walikamatwa, na walikamatwa kwa sababu za kisiasa, vinginevyo wangekuwa mtaani...
Watoto wa kike wanatahiriwa, na watu wanafanya sherehe adharani, hamna polisi anayewakamata..huku, kutembea na bastola ni ubishoo, kwa hiyo matumizi ya silaha ni ya kiholela kabisa
Polisi wapo, lakini RUSHWA ndio imewatawala,,, yaani huku wageni tunaishi kama tupo sudani, au afriganistani,.. so sad kwa kweli
Alikuwa anasimamia kituo kimoja isipokuwa vingine alikuwa akienda kwa dharula. Lakini usiku wa tukio hakuwa kikazi.
Duuu!!!Mwanza ni unlimited au Arusha
Kijiji cha Kaselya, Tarafa ya Ndago, wilaya ya Iramba (SINGIDA)Mkuu,
Mazishi yalifanyika wapi?
Jenga hoja mkuu. Matusi hayasaidii. Tukio ninalozungumzia ni lile la kuukuta mwili wa marehemu na hata aliyetoa msaada wa kwanza kumpeleka hospital ni ndugu yangu.Pimbi wewe ulishuhudia kwa macho yako wakati akikatwa na kupigwa
Mazingira ya safari ndio yanathibitisha hakuwa anaenda kazini mkuu. Na mkewe ambaye ndiye waliishi nae angelikuwa na nguvu ya kusema angesemaNilichotaka ni kufahamu tu kama kuna kituo chochote anachokisimamia (anaenda kwa dharula) kipo uelekeo aliopatwa na mauti.
Suala la kuwepo kikazi sisi naamini hatuwezi kuthibitisha ama kupinga kwasababu tunafahamu daktari yupo kazini muda wote.
Mazingira ya safari ndio yanathibitisha hakuwa anaenda kazini mkuu. Na mkewe ambaye ndiye waliishi nae angelikuwa na nguvu ya kusema angesema
Jamaa yawezekana alikua anakula wake za watu au mke wa mtu.Polisi wachunguze na watoe taarifa ya uchunguzi.Dah tarime sio mahali pa kufanyia kazi hata kidogo
Hwri tu waajiriwe wa hukohuko tu. Wasichukue watu wa mikoani bwanaIt is very painful
![]()
Daktari Kituo cha Afya Nyangoto auawa kikatili
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyang’oto kilichopo Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini, Dk Isack Sima ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka kituo chake cha kazi...www.mwananchi.co.tz
Yaani waajiri wa hukohukoo aiseeDah tarime sio mahali pa kufanyia kazi hata kidogo
Basi tuseme baadhi yao sio wote mfano mm kila mwaka nafanya biashara ya viazi kule kabwe a bunchali tena nalala vijijini kwa wakuriya nakula ugali na kuku samaki sangara satoWw ni mkurya???
Ilikuwaje akauwa bila kosa?Ina maana hao jamaa walikuwa wana shida gani nae?Hakuna tukio liliniuma huko TARIME kama Wakurya kumuua huyu Mwalimu asiyekuwa na hatia yoyote
Tena kwa kumchoma Mkuki shingoni
Sasa nani atakayehitaji kwenda kufanya kazi huko?
View attachment 2612898
Walitaka huyo Mwalimu awape pesa, Mwalimu akasema hana hela, only that wakamuuaIlikuwaje akauwa bila kosa?Ina maana hao jamaa walikuwa wana shida gani nae?
Basi hauwezi ukawa na taarifa sahihi za tukio la kuuawa, kwa sababu haujalishuhudia.Toka taarifa ya tukio hadi kuaga
Ulidhan???Mkuu, nilidhani unamaanisha youkurian
It is very painful
=====
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto kilichopo Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini, Dk Isack Sima ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka kituo chake cha kazi usiku akirejea nyumbani.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele ambaye amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kumtaka mwandishi kumtafuta baadaye jioni kwa ufafanuzi zaidi.
Dk Sima ambaye inadaiwa aliuawa Mei 3 zilizopita, taarifa zilizosambaa mitandaoni leo Mei 6, 2023 zimeeleza kuwa juzi alishinda kazini akihudumia wagonjwa hadi usiku.
“Ni kawaida yake kujitoa hata muda wa ziada. Wakati anarudi nyumbani, alikutana na watu waliosimamisha pikipiki yake na kumshambulia kwa mapanga. Amekatwa kichwani, mgongoni, mikononi, miguuni yani hata haielezeki. Ameuawa kinyama,” kilieleza chanzo hicho.
Imeelezwa kuwa Dk Isack baada ya kuhitimu shahada ya udaktari Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francisko cha Afya na Sayansi Shirikishi (SFUCHAS) na mafunzo kwa vitendo aliajiriwa kituo cha afya Nyangoto kata ya Nyamongo, Tarime vijijini ambako amefanya kazi kwa miaka miwili kama Mganga Mfawidhi.
Taarifa zinazotolewa na wananchi wa eneo hilo wanamzungumzia Dk Sima kama kijana aliyefanya kazi usiku na mchana, “Hata ukimpigia simu usiku atawasha pikipiki kuja kukuhudumia.”
Kufuatia tukio hilo, Wizara ya Afya imesema inafuatilia kwa kina na aitatoa taarifa rasmi.