Ninyi wakurya wa Nyamongo kwa nini mnaua Daktari kijana kama huyu?

Ninyi wakurya wa Nyamongo kwa nini mnaua Daktari kijana kama huyu?

Kuna mahali nimeskia alikua anasimamia vituo vitatu, je hilo lina ukweli?

Kama ni kweli, je Kati ya hivyo vituo hakuna kilichopo uelekeo wa huko alipokua anaenda huo usiku?
Alikuwa anasimamia kituo kimoja isipokuwa vingine alikuwa akienda kwa dharula. Lakini usiku wa tukio hakuwa kikazi. Japo naona wizara ya afya wametoa ripoti kwamba alikuwa akielekea kazini jambo ambalo sio kweli. Ukifika nyamongo ukasema alikua anaenda kazini usiku ule watakushangaa mno.
 
Huku nyamongo, kuna shida kubwa sana, ndani ya mwaka huu, wameshauawa watu zaidi ya kumi,kuna dada alikutwa amepigwa risasi, kuna wengine wawili walichomwa na visu kwenye uke katika matukio tofauti,wakafa kwa kupoteza damu nyingi.. kuna mwingine aliuliwa mgodini kwa kupigwa risasi, kuna mwingine alikutwa amejinyonga, lakini watu wanasema kuwa alipigwa na mume wake mpaka akafa,.. kuna wengine waliuliwa wawili kwa wakati mmoja.... Kuna mwingine aliuliwa kwa kusingiziwa kuwa ni mwizi, kumbe hakuwa mwizi..... Na katika matukio hayo yote ni mawili tu, watu walikamatwa, na walikamatwa kwa sababu za kisiasa, vinginevyo wangekuwa mtaani...
Watoto wa kike wanatahiriwa, na watu wanafanya sherehe adharani, hamna polisi anayewakamata..huku, kutembea na bastola ni ubishoo, kwa hiyo matumizi ya silaha ni ya kiholela kabisa
Polisi wapo, lakini RUSHWA ndio imewatawala,,, yaani huku wageni tunaishi kama tupo sudani, au afriganistani,.. so sad kwa kweli
Mkuu samahani kaa hutojali. Unaweza ukataja maeneo ambako hayo matukio yalitokea? Maana mgodini watu kupigwa risasi na askari sio issue kabisa na huemda umeenda nyamongo wakati matukio ya risasi yamepungua kwa kiasi kikubwa sana
 
Alikuwa anasimamia kituo kimoja isipokuwa vingine alikuwa akienda kwa dharula. Lakini usiku wa tukio hakuwa kikazi.

Nilichotaka ni kufahamu tu kama kuna kituo chochote anachokisimamia (anaenda kwa dharula) kipo uelekeo aliopatwa na mauti.

Suala la kuwepo kikazi sisi naamini hatuwezi kuthibitisha ama kupinga kwasababu tunafahamu daktari yupo kazini muda wote.
 
Mwanza ni unlimited au Arusha
Duuu!!!


Gharama zitakua kubwa sana alaf kuagiza maku usiyoijua ni bonge la kamar inaweza ikawa tofaut na mikato yako


Bora kutafuta mgeni mwenzako muangalie namna ya kubadilishana virus
 
Aiseeee hakuna kazi za watu records management huko jaman wakuu nafaa njaa mwaka wa kumi bila hata ajira
 
Nilichotaka ni kufahamu tu kama kuna kituo chochote anachokisimamia (anaenda kwa dharula) kipo uelekeo aliopatwa na mauti.

Suala la kuwepo kikazi sisi naamini hatuwezi kuthibitisha ama kupinga kwasababu tunafahamu daktari yupo kazini muda wote.
Mazingira ya safari ndio yanathibitisha hakuwa anaenda kazini mkuu. Na mkewe ambaye ndiye waliishi nae angelikuwa na nguvu ya kusema angesema
 
Kwanza pole kwa familia ila jamii hii hautakiwi kuishi kinyonge kabisa,pia mademu usiweke uhusiano nao ni vema kupiga siku moja afu ukasepa ila vijana wa mkoa wa mara wana wivu sana sio wa ku share kwenye mahusiano kabisa.
 
Ww ni mkurya???
Basi tuseme baadhi yao sio wote mfano mm kila mwaka nafanya biashara ya viazi kule kabwe a bunchali tena nalala vijijini kwa wakuriya nakula ugali na kuku samaki sangara sato
 
Toka taarifa ya tukio hadi kuaga
Basi hauwezi ukawa na taarifa sahihi za tukio la kuuawa, kwa sababu haujalishuhudia.

Hilo la kuuawa umehadithiwa kama ilivyo mimi na ukweli utategemeana na muhadithiaji ambaye na yeye hawezi kuwa na taarifa sahihi isipokuwa kama alishuhudia tukio likitekelezwa.
 
Mkuu, nilidhani unamaanisha youkurian
Ulidhan???
JamiiForums790734876.jpg
 
It is very painful
=====

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto kilichopo Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini, Dk Isack Sima ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka kituo chake cha kazi usiku akirejea nyumbani.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele ambaye amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kumtaka mwandishi kumtafuta baadaye jioni kwa ufafanuzi zaidi.

Dk Sima ambaye inadaiwa aliuawa Mei 3 zilizopita, taarifa zilizosambaa mitandaoni leo Mei 6, 2023 zimeeleza kuwa juzi alishinda kazini akihudumia wagonjwa hadi usiku.

“Ni kawaida yake kujitoa hata muda wa ziada. Wakati anarudi nyumbani, alikutana na watu waliosimamisha pikipiki yake na kumshambulia kwa mapanga. Amekatwa kichwani, mgongoni, mikononi, miguuni yani hata haielezeki. Ameuawa kinyama,” kilieleza chanzo hicho.

Imeelezwa kuwa Dk Isack baada ya kuhitimu shahada ya udaktari Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francisko cha Afya na Sayansi Shirikishi (SFUCHAS) na mafunzo kwa vitendo aliajiriwa kituo cha afya Nyangoto kata ya Nyamongo, Tarime vijijini ambako amefanya kazi kwa miaka miwili kama Mganga Mfawidhi.

Taarifa zinazotolewa na wananchi wa eneo hilo wanamzungumzia Dk Sima kama kijana aliyefanya kazi usiku na mchana, “Hata ukimpigia simu usiku atawasha pikipiki kuja kukuhudumia.”
Kufuatia tukio hilo, Wizara ya Afya imesema inafuatilia kwa kina na aitatoa taarifa rasmi.
 

Attachments

  • IMG_9905.MP4
    8 MB
Back
Top Bottom