Nipeni Urais wa Tanzania muone namna gani CCM wametuchelewesha!

Kura yangu nàkupa, unagombea kupitia chama gani?
 
Bahati mbaya hakuna Sera ya mgombea binafsi Tanzania
 
Utakua rais wa machawa wote…Enhee Mwenyezi Mungu Akusaidie….Ameen
 
Unaweza kuigeuza hii nchi kuwa ULAYA ndani ya miaka 3 tu.

Unaweza kuita kila tajiri huko duniani, akaja akajenga majumba marefu, ghorofa, barabara urembo za kulipia na madaraja na ya nakshi.

issue ni kwamba, wananchi wako wanapata manufaa gani??

Kupiga picha kwqenye majengo na kurekodi video za kujisifia halafu wanarudi nyumbani.

kUNA NCHI YA mWALIMU nYERER HAIKUJENGWA HIVYO.

Nenda Kenya kajionee maghorofa halafu nenda Kibera, Pipeline estste, mathere kaone wakenya halisi wanavyoishi.
 
Nchi gani ya mwalimu nyerere unayoisema? Ya hawa wananchi walioachwa wanaishi kwenye nyumba za tembe na wanavaa nguo za viraka? Wananchi walioachwa wanapanga foleni kununua vitu kama sabuni?

Umeenda Kenya if hivi karibuni na kuona wanavyo transform hayo maeneo yaliyojengwa hovyo kwa ajili ya hao wananchi wa kawaida?

Ona kinachofanyika Kenya alafu ujione mlivyo nyuma.
 
Uzalendo mtu akiwa apeche akilambishwa asali anaanza kutuambia tuhamie burundi.
Kuna kipindi nilijaribu kwa mzalendo wa kweli, aisee Yaliyonikuta ni matusi tu na kejeli kutoka kwa watoto wa vigogo wa CCM.

Tanzania hakuna uzalendo wa kweli. Hao ni wachumia tumbo tu wao na watoto wao..
 
Umewahi kwenda nje ya nchi??

Aunni mbwekaji tu.

Walikuwa wanaishi kwenye nyumba za tembe zilizojengwa wapi??

Hao wananchi hawakuwa wanamiliki ardhi na mashamba???

Sisi tulikula mahindi ya Yanga na kuvaa viraka mwaka 1975, na baada ya vita ya Kagera hivi unajua wakenya wengi mpaka sasa bado wanaandamana kwasasabu ya bei ya Unga???

Unajua leo mwaka 2025 bado kuna wakenya wananunua pumba wanasaga na kupika ugali??

Dar es Salaam ni kubwa mara mbili kuliko Niarobi, ila check hao wakenya wa Nairobi wa kawaida wanavyoishi. Watu Nairobi wanaishi mpaka nyumba za mabati.


View: https://youtu.be/iFcG7roY_dE
 
Tanzania hakuna watu hata masikini kabisa wanaoishi hivi. Na hii ni Nairobi.

Hapa sijataja Kibera amabayo ni maarufu.



View: https://youtu.be/Z5po3zN8PBE
 
Nyerere alijenga nchi (Kuunganisha watu, kulinda nchi, kuacha raslimali za nchi)

Waliobaki wanapaswa kujenga uchumi wa watu, WATANZANIA.

Utakuwa ni upumbavu kuita wazungu, wachina na waarabu waje kujenga majengo makubwa ya kupia picha halafu watu wabaki watumwa tu.
 
N kuna mambo huyajui. Unabonga tu.

Mimi naishi mpakani na Kenya. Wakenya wengi wanakuja kupata matibabu Tanzania kwasababu ya gharama za Kenya.

Na siku hizi tuna Jakaya Kikwete Hospitatali ya moyo, wakenya na majirani wanajaa.

Hytuipendi CCM, ila tunaipenda nchi yetu na ukweli uko wazi, kuna mambo hata wakenya wanayatamani Tanzania.
 
Acha uzwazwa wewe! Wewe unaishi mpakani mimi Kenya naenda kila siku na nina biashara huko
 
Unajiona ulivyo zwazwa? Vita ya kagera ilikuwa mwaka 1975?

Rwanda wamepigana vita hadi kuuana! Wananchi wao wanakula mahindi ya Yanga? Wananchi wao wanapanga foleni kununua bidhaa?

Msisingizie vita vya Kagera kana kwamba wote waliopigana vita wamekuwa maskini wa kutupwa.

Nyerere alikuwa na sera mbovu za kiuchumi na ndizo zilizotufubaisha hadi leo full stop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…