Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Nipo Mtwara, serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa. Nimepamiss Dar Es Salaam!

Kusema mtwara maji shida kwamba wanategemea maji ya mvuo ni uongo

Usafiri kusema shida uongo usafiri mkubwa wa mtwara ni bodaboda popote unapo enda ni buku up buku jero kwa usafiri wa haraka

Viwanja vipo vingi sana ujatembea kuna leopard pili msimbati ukienda utatamni kwenda kila siku

Chakula kuwa shida ni uongo sema huna hela ni kweli vitu viko juu sana ila pesa yake kuipata sio ngumu kama unajua kutafuta pesa ila kama unategemea mshahara mtwara hapakufai toka

Kusema saa tatu watu hamna ni kweli watu wa mtwara wanapenda kutulia sana hasa nyakati za usiku mwisho saa moja kutokana na alshababu kuvamia wanaotoka msumbiji ndio maana now mtwara ukitaka kutembea tembea na batua ya utambulisho wa mtaa wako ukikutwa na polis usiku unabebwa kama ulivyo unahisiwa wewe ni alshababu so watu wanakaa majumbani kwasababu
Vingi alivyosema ni uongo tatizo lake haijui mtwara na hajatembea, eti anasema hadi huduma za kifedha ni shida!. Huyu alikuja na dar es salaam yake kichwani
 
Kuna watu wa aina ya mleta mada wao wakiamua kukataa jambo wamelikataa.

Huyu anaonyesha tangu alipochaguliwa akafanye kazi mtwara akili yake tayari ilishakataa kwenda mtwara hata kabla hajagusa mtwara.

Hapo Kila kitu anachopitia anakiangalia kwa jicho la negativity. Mtu wa aina hii hawezi kuona Jema akiamua kukataa.

Kuna jamaa yeye hawapendi wachaga,ikatokea ametembelea Moshi,alikuwa anatukana Kila kitu na kukandia Kilimanjaro. Mtu anachukia hadi ukungu wa asubuhi eti haoni watu!!
😂😂😂 Kwanini alikuwa hawapendi wachagga walimfanyaniii? Ila ndo anachukia mpaka ukungu .... Chuki promax 😂
 
Vingi alivyosema ni uongo tatizo lake haijui mtwara na hajatembea, eti anasema hadi huduma za kifedha ni shida!. Huyu alikuja na dar es salaam yake kichwani
Nyamaza.. kwanza lako hulijui en your supporting nonsense,,get out my site
 
Mimi naungana na shemeji kusema “utazoea tu”. Itakuchukua muda ila kuna siku utashangaa umeshapazoea kabisa.
atazoea tu. mbona mpapura, mikindan maji yanatoka vizur tu. na viwanja gan unataka ? mbona kwa lipaje pako vizur na sijajua we umekaa wap shangani beach maj yanatoka vizur. kushinda njaa mtwara uongo tena wa mchana. Manda ( wali) mtwara bwana wewewee bhaa.umejaa kila mahali. kama labda huna hela kama unayo nenda police mess beach ukale pweza
 
Nyamaza.. kwanza lako hulijui en your supporting nonsense,,get out my site
Mimi nipo mtwara, acha kufanganya watu, unajifanya kushangaa stendi ya mkanaled ila hushangai jalala la mbagara, hiyo saa tatu unavyosema barabara I akuwe nyeupe wapi huko? Wahedi wewe
 
atazoea tu. mbona mpapura, mikindan maji yanatoka vizur tu. na viwanja gan unataka ? mbona kwa lipaje pako vizur na sijajua we umekaa wap shangani beach maj yanatoka vizur. kushinda njaa mtwara uongo tena wa mchana. Manda ( wali) mtwara bwana wewewee bhaa.umejaa kila mahali. kama labda huna hela kama unayo nenda police mess beach ukale pweza
Maji yanatoka ila ni ya shida sasa unabisha nini mkuu!! Maji yenyewe yamejaa chunvi koo!
Sometime unarudi kazini usiku like saa 3 kama huna cha kupika ndani huwezi pata chakula hata cha kununua..
 
Mimi nipo mtwara, acha kufanganya watu, unajifanya kushangaa stendi ya mkanaled ila hushangai jalala la mbagara, hiyo saa tatu unavyosema barabara I akuwe nyeupe wapi huko? Wahedi wewe
Ooh please 😄 unatetea kwenu am sorry
 
Mimi nipo mtwara, acha kufanganya watu, unajifanya kushangaa stendi ya mkanaled ila hushangai jalala la mbagara, hiyo saa tatu unavyosema barabara I akuwe nyeupe wapi huko? Wahedi wewe
Mkuu mtwara ni pazuri kuliko Mbagara au ni jalala tu?
 
Sifa mojawapo ya binadamu ni kuwa na uwezo wa kuzoea mazingira, Just wait and you will adapt to your new surroundings
Tangu nifike Mtwara miezi kadhaa iliyopita, mambo ninayokutana nayo sikuyategemea kabisa. Picha inaanza wakati nakuja kuripoti, ile nafika bus stand ya Mkanaredi naambiwa hapa ndiyo Manispaa ya Mikindani na ndiyo mjini.

Sikuamini! Mr. akanitia moyo na kuniambia nitazoea mazingira. Nikasema, "Sawa, maadam ni mjini, kitu cha msingi ni huduma."

Tukachukua lodge (na lodge zenyewe maji hayatoki, wanategemea maji ya mvua... yani ni tafrani tupu!). To cut a long story short, maisha ya Mtwara ni magumu kwenye nyanja zote! Maji ni shida, bei ya vitu iko juu sana kuliko hata Dar es Salaam, na miundombinu hafifu inafanya usafiri kuwa wa tabu.

Huduma za kifedha ni chache na ziko mbali, yani kulala au kushinda njaa ukiwa na hela mfukoni ni kitu cha kawaida sana hapa!

Ikifika saa 3 usiku, barabarani ni nyeupe kabisa—huoni mtu, na maduka yanafungwa mapema. Viwanja vipo, lakini The Shooters ndicho kiwanja pekee nilichoelewa, na nikiwa hapo najihisi kama niko Dar es Salaam.

Serikali ni kama imeususa kabisa huu mkoa!
 
Kwa sisi ambao tumetembea sehemu nyingi hii nchi,karibia Kila sehemu kunafanana fanana. Mabadiliko ni machache mno mkoa kwa mkoa. Na mtwara imepazidi sehemu nyingi tu siyo kubaya kihivyo.

Kuna dada yeye ametokea kupachukia Dodoma vibaya mno. Ukimsikia anavyopaponda Dodoma unaweza sema huko mahali ni kuzimu na wanaoishi huko ni mashetani.

Dodoma hii hii ambayo Kuna nyuzi kibao humu ndani zinapasifia Kuna/kumejengeka.
huyu aki enda shinyanga ata pigana 😆🤣
 
Back
Top Bottom