Nipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, uliza chochote kuhusu Kigoma utajibiwa

Nipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, uliza chochote kuhusu Kigoma utajibiwa

Kigoma iko burundi au
Hapana, Kigoma haipo Burundi, kutoka Kigoma hadi Burundi ni karibu km 230, usafiri wa gari unachukua karibu masaa manne.

Muhange na Muhange juu ni vijiji viwili vilivyoko takriban kilometa 46 magharibi mwa mji wa Kakonko mkoani Kigoma, hapo Muhambwe ndio mpakani na Burundi ambako katika kipindi cha miaka mingi kumekuwa na soko linalowavutia wafanya biashara kutoka Burundi na Tanzania.

image1024x768.jpg

Kijiji cha Muhambwe, mpakani
 
Mambo VP?embu niambie hapo KIBIRIZI wanauzaje?Mchele pia bandari ya kibirizi imekamilika au imebaki kama mwenda zake alivyo iacha?
Kalya ndiko wanalima sana mpunga ila kwa sasa bei ya Mchele ni sh 1000 - 1500/= kwa kilo hapa Kibirizi.

Bandari ya Kibirizi bado inaendelea kujengwa, ma engineer ndio hao
158475222_2959780914240937_706231754268105094_n.jpg
 
Ukiwa unataka vitu vya ndani kama furniture elctronics,,,kwa kigoma unachukulia wapi?
Furniture zinatengenezwa hapa hapa, na zipo zinazoagizwa Dar es salaam kupitia njia ya gari moshi. Kikawaida mizigo mingi ilikuwa inapitia Kigoma kisha ndio inasambazwa kwenda Congo na Burundi. Lakini kwasasa kuna Bandari ya Karema inavuka kwenda Congo na pia baadhi ya vitu Wacongomani wanakwenda kuchukulia Mkoani Mwanza, hivyo Kigoma imeuwawa kinamna yake.
 
Mwitongo hotel, Kigoma, Tanzania

View attachment 1988335

Karibuni Kigoma,
Mkoa wa Kigoma uko magharibi mwa. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

View attachment 1988349

Uliza chochote kuhusu Kigoma, utajibiwa.
Je ni kweli kuwa wamanyema wakija Dar hujifanya wakongo na wakienda Kigoma hujifanya watu wa pwani? Je ni kweli kuwa Khalifa Hamis ni Mrundi anayetumia uislam kuishi Tanzania?
 
Nasikia Kigoma kipindi Cha mvua Kuna radi za hatari...ukiwa mgeni unaweza geuza kesho yake ulipotoka ni kweli?
Inasemekana ni kutokana na kima kikubwa cha maji ya ziwa Tanganyika, labda wataalamu wa mambo ya majira na hali ya hewa watajua zaidi
 
Back
Top Bottom