Nipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, uliza chochote kuhusu Kigoma utajibiwa

Nipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, uliza chochote kuhusu Kigoma utajibiwa

Hapana, Kigoma haipo Burundi, kutoka Kigoma hadi Burundi ni karibu km 230, usafiri wa gari unachukua karibu masaa manne.

Muhange na Muhange juu ni vijiji viwili vilivyoko takriban kilometa 46 magharibi mwa mji wa Kakonko mkoani Kigoma, hapo Muhambwe ndio mpakani na Burundi ambako katika kipindi cha miaka mingi kumekuwa na soko linalowavutia wafanya biashara kutoka Burundi na Tanzania.

View attachment 1988429
Kijiji cha Muhambwe, mpakani
Mhhhhhh, labda useme kigoma mpaka bujumbura ndo kuna umbali ila kigoma - manyovu mpakana na Burundi mbona karibu sana
 
Je ni kweli kuwa wamanyema wakija Dar hujifanya wakongo na wakienda Kigoma hujifanya watu wa pwani? Je ni kweli kuwa Khalifa Hamis ni Mrundi anayetumia uislam kuishi Tanzania?
Si kweli, Wala wamanyema hawawezi kujifanya ni Wakongo labda huyo mmanyema awe ni mtu aliyewahi kuishi Congo na anakifahamu Kicongo. Kuhusu Khalifa Hamisi bado sijapata mtririko wa nasaba yake ilivyo.
 
Mwitongo hotel, Kigoma, Tanzania

View attachment 1988335

Karibuni Kigoma,
Mkoa wa Kigoma uko magharibi mwa. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

View attachment 1988349

Uliza chochote kuhusu Kigoma, utajibiwa.
Kwanini wenyeji wakigoma wengi ni wafupi na wamekomaa mtu ana miaka40 ila anaonekana kama miaka 28
 
Kwanini wenyeji wakigoma wengi ni wafupi na wamekomaa mtu ana miaka40 ila anaonekana kama miaka 28
Sio wote, ni baadhi ya watu kutokana na maeneneo husika au familia zao zilivyo, Kwa mfano wapo waha ni wafupi na weusi na pia wapo waha ni warefu, na hivyo hivyo kuna wamanyema wafupi weusi, na pia wapo warefu weusi.
 
Back
Top Bottom