Nipo mwambao wa Ziwa Tanganyika, uliza chochote kuhusu Kigoma utajibiwa

Mhhhhhh, labda useme kigoma mpaka bujumbura ndo kuna umbali ila kigoma - manyovu mpakana na Burundi mbona karibu sana
 
Je ni kweli kuwa wamanyema wakija Dar hujifanya wakongo na wakienda Kigoma hujifanya watu wa pwani? Je ni kweli kuwa Khalifa Hamis ni Mrundi anayetumia uislam kuishi Tanzania?
Si kweli, Wala wamanyema hawawezi kujifanya ni Wakongo labda huyo mmanyema awe ni mtu aliyewahi kuishi Congo na anakifahamu Kicongo. Kuhusu Khalifa Hamisi bado sijapata mtririko wa nasaba yake ilivyo.
 
Kwanini wenyeji wakigoma wengi ni wafupi na wamekomaa mtu ana miaka40 ila anaonekana kama miaka 28
 
Kwanini wenyeji wakigoma wengi ni wafupi na wamekomaa mtu ana miaka40 ila anaonekana kama miaka 28
Sio wote, ni baadhi ya watu kutokana na maeneneo husika au familia zao zilivyo, Kwa mfano wapo waha ni wafupi na weusi na pia wapo waha ni warefu, na hivyo hivyo kuna wamanyema wafupi weusi, na pia wapo warefu weusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…