Nipo njiapanda kwenye ndoa yangu mpya. Naomba mnishauri mliooa 🤔

Je kama makubaliano yalikuwa ni tununue kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba ya familia unaona wazo la kuandika jina la mtoto tena wa kambo ni sahihi?
Suala la mwanamke kuchangia hela nyingi sio hoja maana wote wanajenga familia moja.
Mwanamke kutoa pesa kubwa ni hoja man.Otherwise na wewe logic yako ya kujenga familia moja haina nguvu tena

Uwiano huko hivi 200,000:900,000(mwanaume) 700,000:900,000(mwanamke) nani mwenye mali hapa(hoja ilikuwa umiliki mambo ya kujenga familia hii hoja alikuwa bado hajasema)
 
Umechangia laki 2 halafu unataka uandikwe wewe? Tafuta hela, nunua kiwanja uandike jina lako. Hiyo laki 2 umemsaidia anunue kiwanja chake.
Haya ndo yana sababisha ndoa za siku hizi kujaa migogoro isiyo isha.
Watu mmeoana kwa lengo la kujenga familia moja sasa hayo mambo ya kuanza kununua mali za kujitegemea kila mtu yanatoka wapi?
Wanandoa hawawezi kuwa na ndoto mbili tofauti alafu ukategemee hiyo ndoa idumu.
 
Dah mwamba unajua kupatanisha. Yani kutoka m2 hadi laki9!😀

Halafu nimependa hapo unaposema, tuandike jina la TOTO LAKE, 🤣🤣

Sasa ushauri, laki mbili yako fanya kama umehonga tu maana ni ndogo sana kwenye hiyo 9. Kiwanja hicho hata baba mtoto kitamhusu maana kina jina la mwanae😆
 
Uyo ni mbishi yaani haambiliki ila ananifurahisha kwenye kupeana utamu tu😋
Kama ushajua hivyo kula utamu tu basi, mambo ya maendeleo cheza kwa umakini wa hali ya juu. Laki mbili ni hela plus muda wa kutafuta eneo na bargaining uliyofanya kuwa kama umetoa msaada tu. Hicho kiwanja mwache aandike jina analotaka. Ila bro kuanzia hapo kuwa na mpango wa kufanya mambo yako nje yake kwa umakini wa hali ya juu sana.
 
Hapo hakuna ndoa, jamaa anaenjoy free utamu tu
 
Tuchukua box zako mbili achana na hiyo habari.
 
Sasa laki 2 ndio upandishe kisukari... Potezea!?

Siku nyingine kiwanja cha laki 9, we sema 1.5 akisema anatoa 1.2 we ongezea 3 unakubali, akitoa 1.2, unaenda kulipa laki 9 mia 3 unaweka mfukoni, ukitumia akili vizuri, mjanaja anakuwa mshamba. Hizi mbinu za kivita mdogo wangu.. Nishatumia sana ujanani.
 
Mbona mali anazo tafuta mwanaume tena kwa %100 huwa zinawekwa chini ya himaya ya familia nzima?
Kama makubaliano yao yalikuwa ni kununua kiwanja kwa ajili ya familia basi hoja ya mwanamke kuchangia hela nyingi haina mashiko maana kila mwana ndoa ana jukumu la kuchangia maendeleo ya kifamilia kulingana na nafasi na kipato chake kwa sababu wote ni wanufaika wa hiyo familia.
 
She has allready choose side kua chake ni chake na chako ni chenu sasa wewe fanya hivi

1 Mruhusu aandike majina yake au ya mtoto wake vyovyoye anavyo taka

2. Tafuta kiwanja kingine, Nunua andika majina yako na yeye asijue

3. Tafuta mwanamke mwingine asie na mtt acha ujinga wa kujifanya u can fix what others left
 

Uko sahihi mkuu.

Mwanamke kaonesha ubinafsi mkubwa kua kwakua yeye katoa hela kubwa sasa hicho kiwanja aandikwe mwanae tafsiri yake sio cha ke wala me ni cha third party.

Sasa na jamaa akinunua kiwanja aandike mama yake uone kama huyo mwanamke hajasema tuachane
 
Asee huu unakuwa uzembe wa mwanaume.Mali ambayo unatafuta mwanaume kuweka umiliki kwa familia uongo.

Wanawake ni unpredictable na sheria zinakuwa upande wao sana.Ndio maana umiliki wa mali ni bora wapewe watoto au umiliki wewe kitu chako.
 
Ndoa za wanawake kuaona zinakuwepo? Suala la usagaji litaisha lini Duniani. Nilipoona title nikajua ni mwanaume. Kuja soma mwandiko na sauti ya kike kabisa nimeshangaa wanawake kutaka oana au kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
 
Issue sio laki 2. Idea tu ya kusema kiwanja kiandikwe kwa jina la mtoto wa nje ni ya kibinafsi, Imekaa ki defensive zaidi na tayari ni redflag demu anajiandaa for something big ahead
 
Issue sio laki 2. Idea tu ya kusema kiwanja kiandikwe kwa jina la mtoto wa nje ni ya kibinafsi, Imekaa ki defensive zaidi na tayari ni redflag demu anajiandaa for something big ahead
Yaani kenge kama huyo unamuonesha umamba, vyake unakula, ye mwenyewe unamla, akidhani anakula vyako kumbe anatumia vyake.

Nishatumia sana mbinu hii kwa wanawake wajinga wajinga.
 
Asee huu unakuwa uzembe wa mwanaume.Mali ambayo unatafuta mwanaume kuweka umiliki kwa familia uongo.

Wanawake ni unpredictable na sheria zinakuwa upande wao sana.Ndio maana umiliki wa mali ni bora wapewe watoto au umiliki wewe kitu chako.
Kwani ww leo ukioa mwanamke ukanunua kiwanja na ukajenga nyumba ya kuishi si itahesabika ni mali ya familia nzima hata kama mwanamke hajachangia hata mia?
Huu upumbavu wa kuoa mwanamke alafu akifika ndani anaanza kupambania ndoto zake badala ya ndoto za familia ndo kumesababisha ndoa za siku hizi kujaa migogoro isiyo isha.
 
Man leo hii nikaweka mke ndani, nikajenga nyumba ambayo mwanamke hajatoa senti moja chafu ajue kama kuna watoto tutapata wote wao ndio wamiliki.Otherwise nyumba na kiwanja vitakuwa vyangu na hakuna mjadala.

Lakini ikitokea kama ya huyu mleta mada.Honestly hicho kiwanja kitakuwa chake na umiliki atapanga yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…