Nipo njiapanda kwenye ndoa yangu mpya. Naomba mnishauri mliooa 🤔

Nipo njiapanda kwenye ndoa yangu mpya. Naomba mnishauri mliooa 🤔

Katafute hela wewe mwanaume mpenda kitonga.

Umechangia laki mbili tu, Halafu unataka kiwanja kiandikwe jina lako!!

Unapenda dezodezo, We bwana weee! yatakushinda!!
 
Ukiandika mtoto ina maana Baba mtoto ata husika kwa hilo leo au mbeleni, wewe utakuwa kando na hauna hoja.

Mwambie lazima Jina lako liandikwe pia, hapa hata mkizaa watoto wako watakosa neno hapo.

Akili yako inavyotaka fata basi.. Nakuona una bidii unamfaa maishani. Ila mapenzi sijui kama anayo ya kweli eeeeeh utajiju
Atoe laki mbilijina lake lionekane??
 
Kwani ww leo ukioa mwanamke ukanunua kiwanja na ukajenga nyumba ya kuishi si itahesabika ni mali ya familia nzima hata kama mwanamke hajachangia hata mia?
Huu upumbavu wa kuoa mwanamke alafu akifika ndani anaanza kupambania ndoto zake badala ya ndoto za familia ndo kumesababisha ndoa za siku hizi kujaa migogoro isiyo isha.

Na hapo unakuta.

1 Rent anakipa jamaa, Kana kaa bur
2. Matumizi home, Ana clear jamaa kana kula bure
3. Mambo yake madogo madogo ana clear jamaa so hela zake zote kanazo pata kanasave kama hivo hapo unakuta kametoa hela zake zote kiasi cha kwamba kesho mtoto wake akikohoa tu atakae wajibika ni huyo mshkaji.

Nimeona mara nyingi sana, Mwanamke anamshahara Wa laki 8, Mwanaume mshahara wa laki 9. Mwanaume anachukua mkopo anajenga nyumba lakini mwanamke anchukua mkopo ananunua gari lake la kuendea kazini.

Hii inatokea tu endapo Me hujielewi
 
Andika jina la mwanamke mine assume mnao mpango wa kuzaa pamoja.
Btw nani anabeba majukumu ya nyumbani ka kodi ya nyumba, chakula,mavazi na matibabu?.
Hata akiandika jina la meanamke haisaidii maana mwanamke atakua na mammlaka ya kubadiri jina lake kwenda kwa jina la mtoto bila pingamizi la mtu yoyote
 
Unataka jamaa aongeze pesa kwanini? Swali langu je mwanaume ndo angekuwa ametoa 7, je mwanamke naye angetakiwa kuongezewa pesa?
Yes, kama wanataka umiliki wa pamoja si watoe share sawa? Hivi wanaume wa siku hizi mnajielewa kweli? Mwenzie atoe laki7 zoote hizo afu wamiliki sawa? Maana linapokuja suala la kudhulumika mwanamke anakuwaga victim kiasi kikubwa, huyo kijana kama hajawa na hela ya kumiliki vitu kama kichwa cha familia aachane na hiyo mambo
 
Umechangia laki 2 halafu unataka uandikwe wewe? Tafuta hela, nunua kiwanja uandike jina lako. Hiyo laki 2 umemsaidia anunue kiwanja chake.
Wavulana wa sasa ukiwashauri hivo hawakuelewi, sijui uanaume umekwenda wapi! Aibu naona mimi alafu anajiita mwanaume
 
Unataka jamaa aongeze pesa kwanini? Swali langu je mwanaume ndo angekuwa ametoa 7, je mwanamke naye angetakiwa kuongezewa pesa?
Ukute najibishana na mtoto haujui uanaume ni upi akimpa mwanamke afu3 wakizinguana anaidai😆 baki na mawazo yako
 
Ukute najibishana na mtoto haujui uanaume ni upi akimpa mwanamke afu3 wakizinguana anaidai😆 baki na mawazo yako
Kwanini wanawake mko entitled na kuhudumiwa kama walemavu vile?
 
Kwanini wanawake mko entitled na kuhudumiwa kama walemavu vile?
Wewe kama huna hela tulia, wanaume wanajua majukumu yao ni yapi kwenye jamii, mwenye hela unajua hata kama mkewe mfanyakazi, mfanyabiashara, hata haulizagi habari za kuchangia majukumu
 
Andika jina la mtoto achana na mambo ya ujenzi.. Fanya kama umempa mhindi
 
Wewe kama huna hela tulia, wanaume wanajua majukumu yao ni yapi kwenye jamii, mwenye hela unajua hata kama mkewe mfanyakazi, mfanyabiashara, hata haulizagi habari za kuchangia majukumu
Hahaha haya bana, kila la kheri
 
Back
Top Bottom