Jeep wrangler
JF-Expert Member
- Jan 7, 2024
- 1,794
- 3,350
kuwa mkweli...ugomvi wenu ulianzaje.Naweza kusema nilijichanganya Sana kwa huyu mwanamke
Ni mwanamke ambaye nimefunga nae ndoa na tuna watoto watatu
Kutokana na mwenzangu kuwa mwajiriwa tumekua tukiishi mbalimbali japo sio Sana
Kwa miaka mingi nimeonesha Hali ya kumpenda lakini baadae tukaanza kuingia kwenye migogoro ambayo ilisababishwa na yeye kuchepuka waziwazi
Ilifika kipindi akanitamkia amepata mwanaume mwingine nimwache aendelee nae, kwa kweli niliumia Sana kwa kauli zake ukizingatia ni mke wa ndoa na nimetoka nae mbali
Nikapiga moyo konde nikampotezea but ndoa hatujavunja Bado Ila mawasiliano Kati yetu hakuna zaidi ya miezi minne
Siku za nyuma nilikua naongea na watoto wangu kupitia simu ya mama yao, lakini kwa situation iliyotokea na Hali yetu ya mahusiano ilivyo mbaya Kati yangu na mama yao,moyo wangu unakua mgumu Sana kuinua simu kumpigia mama yao ili niweze kuongea na watoto wangu
Kiukweli nimetokea kumchukia Sana huyu mwanamke Hadi kupiga simu yake niongee na watoto wangu Nashindwa.
Nipo tayari kwa Sasa nilaumiwe na watoto wangu kwa kutowasiliana nao na sina njia mbadala ya kuwasiliana nao na siwezi kuanza kumpigia mama yao ambaye tumechuniana zaidi ya miezi minne Sasa.
Ushauri wenu tafadhali, najiskia vibaya kutowasiliana na wanangu Bora wangekuwa wakubwa ningeenda kuwachukua kibabe.
je alikufumania au alikuhisi unachrpuka?
ni vigumu mke akuonyeshe dharau kubwa kiasi hiki bila sababu ya msingi