Nisaidieni kujua kwanini huyu kaka kaniganda kwa miaka minne

Nisaidieni kujua kwanini huyu kaka kaniganda kwa miaka minne

Mdada aliezaa nae keshaolewa
Fanya unalolisikia moyoni mwako na siyo kwa kutaka kumuhurumia kama anavyotaka yeye,huku ukijua kuwa furaha ya ndoa itakuwa yako na machungu ya ndoa ni yako mwenyewe na ikishafungwa ni pingu isiyofunguka.

Mwenye kusuka ama kunyoa ni wewe mwenyewe,na inavyo onekana hauko tayari kulea mtoto ambaye siyo wako kitu ambacho alitakiwa kukupa taarifa mape kuwa ana mtoto na anataka akuoe ili uamue wewe mwenyewe kama ukaolewe hivyohivyo.

Ushauri wangu kwako mwambie kuwa kwa kuwa wewe unamtoto wa nje ya ndoa na Mimi ninaomba unisubiri kwanza nitafute mtoto wa nje ya ndoa nikipata mtoto wa nje ya ndoa ndio tuoane,wewe uje na mtoto wako wa nje ya ndoa na Mimi nije na mtoto wangu wa nje ndoa hapo tutakuwa sawa.
Mdada aliezaa nae keshaolewa
 
Habari zenu Wana Jf naomba nieleze kwa ufupi ...Mimi ni binti WA kike ila Kuna mkaka nilikiwa nae kwenye mahusiano nikiwa sekondari ila nlimuacha baada ya kugundua alinificha kuwa alikuwa na mtoto

Mara kadhaaa tangu kuachana nae amekuwa akinitafuta kwa miaka minne tokea 2020 na kusem kuwa anatka kunioa ila kila akinitafuta namwambia sipo Tyr kwa ndoa ...nikmwambia sitaki ndoa anakubali kabisa hatnisumbua tena ila baada ya siku kadhaa bado anarudi na lile lile swala lake la kunioa ..
Je huyu mkaka atakuwa amemaanisha kunioa au anataka kuniigiza Cha kiume?!
Niulize kwanza
JE bado unamtunuku penzi?
Km unamtunuku, anakujali?
Km mnatunukiana, je unampenda?

Tuanzie apo kwanza
 
Back
Top Bottom