Nisaidieni kuzimua ubongo wa huyu mwanamke

Nisaidieni kuzimua ubongo wa huyu mwanamke

Bado matukio hayajakolea huyo atairudisha tena na atachapwa matukio mpaka akili itakaa sawa.Kwa sasa wewe jali biashara zako tu.
 
Mpe namba zangu ... mwambie turbo charging ipo .......ufundi mpaka peponi atafika akiwa duniani
 
Huyo sio mama mwenye nyumba yangu?? Ana nyumba za kupangisha,Ana Bars kadhaa,mwanaume wake Ana miaka 33,bi mkubwa anakaribia 50s,Ana wajukuu wawili,

Mwenye nyumba anapigwa,ananyanyaswa na kibenten,anadhalilishwa Hadi huruma,aliwahi kumuibia vitu vya ndani vyote,akatoroka after week akarudi kamsamehe,Mara ya mwisho months ago kampiga nusu ya kumuua,bi mkubwa kasema ITS OVER,akamfukuza ..

Last week anasema anamuonea huruma james Hana pa kukaa anadhurura,leo nimemuona James asubuhi kapitia geti la dharura..haha Maza karogwa au jamaa Ana d*ck Kama ya Podrick Payne
 
Salute wakuu

Kuna dada ni rafiki yangu na amekua akinishirikisha mambo yake mengi ya ndani.

Huyu dada aliachwa na jamaa yake ila kile kibuti cha jamaa kidogo kiondoke na roho ya dada,aliteseka,alikonda ila baada ya muda akakaa sawa,akanenepa,akapendeza na mwenyewe akawa anadai kwa sasa anawekeza nguvu kujiboresha yeye na maisha yake kwa ujumla
na kweli kuna hatua kapiga kiuchumi na hata ukikaa nae alikua mtu wa kuongelea big dreams.

Yaani ni mwanamke fulani hivi ukipiga nae story unajifunza vitu ila cha kusikitisha juzi tena ananiambia karudiana na jamaa na anahisi jamaa hana mapenz nae.Namwambia kama unahisi jamaa hana mapenzi na wewe si umuache, anadai amejaribu ameshindwa hivyo anaomba mimi nimshauri afanyaje ili aweze kumuacha jamaa.

Kwa sasa ukikaa nae haongelei tena issue za maana,ni kumlilia tu huyo jamaa.Mind you ni mwanamke mwenye hela zake na ajabu kuna foreigner fulani alimpenda sana huyu dada ila dada kamtosa anadai hisia zake ziko huko alikoachwa.Kuna saa nahisi ana shida kichwani mana kwa maelezo yake ni wazi jamaa hamtaki na hata yeye anajua.

Binafsi sijui chakumshauri nisaidieni wakuu.Tena nahisi akipewa ushauri wa maneno makali labda nikimpa asome anaweza kuzinduka na kukukubaliana na reallity 2kuwa huyo jamaa is gone.
Focus na masuala yako mkuu, hao walipokutana hukuwepo, Leo hii uajitia mshauri mkuu, anyway umemshauri aachane na huyu bwana wake, wewe ndio utakuwa naye? Je wanapokuja kupatana tena aibu inakuwa kwa Nani?
 
Achana na kitu hisia za mapenzi...

Mwenyewe zilinitesa sana...

Yule mwamba popote alipo Nampa maua yake jamani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kifupi huyo dada huwezi kumsaidia ni mpaka aamue mwenyewe kumpotezea huyo jamaa...

Usije ukamlazimisha kuingia nae kwa mahusiano, maana utajutraaa.

Ndio ninachoona unakitafuta hapo.
Nini kilikusaidia kumsahau huyo mwamba mkuu?
 
Waswahili wanakwambia 'wapendanao wakigombana chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune'.

Nafsi iliyopenda haishauriki. Na hapa unachohitaji hasa kusikia ni kwamba umtongoze, ummiliki wewe. Usithibutu.

Kama una thamini sana uwepo wake kwako basi kuwa rafiki wa kumliwaza pale atakapohitaji kuliwazwa, mengine muachie mwenyewe awe muamuzi. Huwezi juwa, katika kumliwaza kwako anaweza aka fall kwako na kumsahau jamaa ila USIFOSI.
 
Back
Top Bottom