Dodoma leo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 1,336
- 1,658
Kila tatizo Huwa Lina utatuz wake, hebu eleza kwanini uliacha Kazi Unaweza saidiwa na wadau hapa ukarudisha Kazi yako. Jpo asilimia kubwa MTU kusema uliacha Kazi Kwa matatizo ya kifamilia ni ngumu kueleweka. MM naamin Kazi yako hyo ukitaka kupambana unaipta lkn Elza why uliacha..
Proffessionally mimi ni mwalimu, masomo ninayofundisha ni Kiswahili na Historia. Nilibahatika kuajiriwa serikalini mwaka 2013. Kutokana na matatizo ya kifamilia nilikazimika kuacha kazi 2019, matatizo yamekuwa yakiniandama bila suluhisho na nimejaribu kutafuta ajira sehemu mbali mbali bila mafanikio.
Kwa sasa nipo tayari kufanya kazi yoyote, iwe sheli, barmen au hata kuhudumia mahotelini nipo tayari ndugu zangu. Familia inanitegemea nikiwaangalia watoto wangu huwa najifungia ndani na kutoa machozi. Najua wapo humu wenye uwezo wa kunisaidia kwa hili. Pia kama nitamkwaza mtu nitaomba kusamehewa, kichwa na akili yangu havipo sawa kwa sasa.
Asanteni