Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Wamiliki wengi wa magari hawako realistic, wanaigiza maisha na wanasema ukweli nusu nusu.

Ukitaka ujue ukweli wa ubora wa magari pita karakana za kutengeneza magari mitaani, tazama, uliza na kudadisi kuhusu magari mbali mbali kisha utapata majibu.
 
Reactions: Cyb
Wamiliki wengi wa magari hawako realistic, wanaigiza maisha na wanasema ukweli nusu nusu.

Ukitaka ujue ukweli wa ubora wa magari pita karakana za kutengeneza magari mitaani, tazama, uliza na kudadisi kuhusu magari mbali mbali kisha utapata majibu.
Ni kweli ila kwa mfano garage zote za hapa Arusha Matoyota ndiyo yamejaa huko....
Ina maana haya matoyota ni mabovu kuli brands nyinginezo..?
 
Ni kweli ila kwa mfano garage zote za hapa Arusha Matoyota ndiyo yamejaa huko....
Ina maana haya matoyota ni mabovu kuli brands nyinginezo..?
Ndio maana yake. Na ukienda kwenye hizo garage hukuti Nissan imelala au benz, utakuta tu za Toyota hadi zimeotea majani kwa chini
 
Kwa million 15 labda utafute ya mtu mkononi ila kwa kuagiza, TRA wana ufala wao wamefanya sasa hivi itakubidi uongeze kama million 3 hapo kwenye bajeti ndipo utaweza kuitoa bandali. Ila hadi kiasi hicho ulichonacho unaweza agiza wakati ipo njiani uwe unajikusanya hela ya bandari, tra, na clearance.

Ni gari nzur mimi pia najikusanya niuze kibaby walker hiki nichukue hiyo nivimbe nayo mjini. Hizo prado tutanunua baadae maana watu wenye roho mbaya wameshika uchumi kwa sasa.
 
Labda haujatazama vema barabarani but hizi gari zipo nyingi kwa sasa na kuhusu spare zinapatikana vema tu na hata ukikosa hapa tz kuagiza ni rahisi sana kwasasa. Pia wanadealer wa nissan hapa tz nadhani.

Hii aliyopost hapo sio body ya Nissan Dualis, bali ni body ya Nissan Qashqai iliyobandikwa jina la dualis kwenye plate.

Nitakiwekea picha ujue tofauti ya bodi ila zote ni gari moja ni sawa sawa n kusema Iphone 7 na Iphone 7 plus......
 
Haya asante mwanachi kutoka kijiji cha Nissanians.....
 
Safi. Umeelezea vema sana na ungekuwa karibu nikununulia japo Pepsi big.....


Safi sana wewe unayajua magari ya sasa na unafuatilia. Safi sana kijana
 
Sio kweli hiyo milioni 12 - 14 sio kweli hebu kacheki na source ya details zako upya.....
 
Unanunua gari ili uuze au utumie? Kuna wanaokaa na magari miaka hata 8.

Kichwa chako kiko sawa?
Nane kidogo sana. Nina mjomba wangu alinunua Suzuki escudo, tokea 2000 yupo nayo hadi sasa hesabu ni miaka mingapi sasa!
 
Ni gari nzuri ina power na speed ila mafuta inameza haswa.
Sio kweli.... Wewe unajua gari inayomeza mafuta.....?!

Mimi natumia passo ya piston tatu ila mafuta unywaji wake haiifikii hiyo Nissan dualis.

Niulize kwann mtoto wa dada nikuelezee....
 
Sahihi kabisa.... Umeongea ukweli kabisa.
 
Ila jamaa wewe kweli ni Car enthusiast wa ukweli. Umepambana hadi umesolve tatizo. Wewe hakuna gari itakuja kukupasua kichwa tena kama umeweza kuvumilia hiyo kash kash ya murano.

Safi sana. Big up kwako
 
Sasa hizo gharama zote si ungeagiza mpya tu?
Mahaba mama... Sisi wanaume magari huwa yanatuteka akili sana na hatukubali kirahisi yatushinde.

Nikikuhadithia kisa cha rafiki yangu aliekuwa anahangaika kutengeneza Subaru yake utasema nyie wanaume mnavichaa na magari yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…