Nitaifichaje hii aibu ili niweze kurudisha heshima yangu

Mimi nilijua tu kuwa utakuja kusema huku jf enhee je wale wengine?
 
Waombe tu msamaha ndugu wote unaofikiria uliwakosea, naamini watakusamehe na pia acha muda ufanye yake, binadamu Wana tabia ya kusahau baada ya muda fulani naamini watasahau na mambo yatakuwa sawa, ila USIRUDIE kunywa pombe kama imekukataa
 
Pole
Ila nmecheka eti ukawaambia unawapenda
Anyway binadamu tumeumbiwa kusahau watasahau na maisha yataendelea
 
Ahsante ndugu
 
Sawa ndugu ahsante pia kwa ushauri ila pia niligombanisha wanawake wawili
 
 
Hapana sio mimi
Oohh...pole sana yatakwisha mkuu!!omba Toba Kwa Mungu uwe na amani,watu watasahau tu.

Huenda pia ndiyo njia ya kufanya uache pombe kabisa hata kama haukuwa mnywaji kihivyo...😊
 
Kipindi ni mchanga kwenye sekta ya ulevi hiyo ilishanikuta sana , dawa ya wamatumbi ukishafanya vituko kama hivyo ni kufuata biashara zako tu , watazungumza mwishowe wakiona upo bize na mishe zako wataanza kujipendekeza wenyewe tu.
 
Kawaida tuu mkuu,Bora umegundua Hilo!jipe moyo na heshimu maamuzi Yako.
 
Pole sana, binadamu tumeumbiwa kusahau.
Hilo litapita tu na litaondoka vichwani mwa watu. Lipe muda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…